Mkuu
Eiyer, shukrani. Unasema binadamu ni muunganiko wa
mwili na roho, sawa ni mtazamo mmoja wapo lakini kitu cha ziada sana katika kutafakari hapa si suala la "binadamu ni nini" bali ni kipi hasa kinafanya mtu fulani ajione/ajitambue/ajihisi/ejielewe etc., kwamba ni yeye katika mjumuisho wote wa vitu vinavyoonekana na visiivyoonekana lakini vinavyoelezewa kama sehemu ya mtu.
Umetaja mwili + roho lakini kwa fikra thabiti zilizowazi za kinadharia zinaweza kutuonesha jinsi mwili wa mtu usivyo centre kwa kuwa ukipewa mwili wa mtu mwingine bado ule u-wewe wako utakuwa haukuondoka na mwili wako wa mwanzo. Ni fikra ngumu kidogo lakini zinaelezeka na zinaweza kuwa conceived na kukubalika. Hili linaondoa hoja yako kwamba lazima mwili wako na roho yako viwe vile vile ulivyozaliwa navyo ili uwe wewe. Kivipi? Nitaelezea kidogo kuhusu mwili.
Tunajua kwamba kuna maendeleo makubwa katika fani ya utabibu ambapo suala la kubadilishwa viungo vya mwili kwa kuwekewa vya mtu mwingine (organ transplants) si ajabu wala si geni tena. Viungo muhimu kabisa katika mwili wa binadamu kama moyo, mapafu, figo, ini, ngozi na vinginevyo vinapandikizwa katika mwili wa mtu mwingine na kufanya kazi kama kawaida. Pia majimaji katika mwili kama damu, maji etc pia yanaweza kubadilishwa na kuwekwa mengine na mtu huyu akaishi. Mwili mzima (kiwiliwili) kubadilishwa ni jambo lililo njiani na ni katika miaka miwili jambo hili linatarajiwa kufanyika katika utabibu kama litafikiwa kipitishwa na jamii. Linapingwa sana jambo hili lakini tayari kuna neurological surgeons na scientists wameweka wazi tafiti zao na majaribio ya uwezekano na jinsi ya kufanya operation hizi za ajabu kidogo.
Kwa hiyo kitu hiki kama kimefikia mahali hapo basi hatuna budi kudadavua katika fikra kwamba katika watu wawili wanaofanyiwa operation hii (1) Anayetoa kiwili-wili (mwili mpaka shingoni) na (2) Anayetoa kichwa, ni nani hasa atakuwa ni yule mtu baada ya operation hii. Kwa kuwapa identity watu hawa tuseme bondia na mwanasoka wanafanyiwa operation hii, kiwili-wili cha bondia na kichwa cha mwanasoka, nani atakuwa huyu mtu baada ya operation? majibu ya wengi yanaweza kuwa labda mwana soka kwa kuwa ndiye mwenye kichwa.
Lakini kabla hatujaanza kudhani tumemaliza mtihani huu twende mbele kidogo. Ikiwa operation hii itawezekana basi pia mbadilishano wa sehemu hizi kuu za mwili zitakuwa zimewezekana (Mfano kichwa na kiwiliwili). Hivyo Bondia na mwanasoka waki-swap vichwa, nani haswa atakuwa bondia na nani mwanasoka baada ya full body transplant operations hizi? Kwa maana hapa tutakuwa na kichwa cha mwanasoka chenye mwili wa bondia wenye mikono iliyokomaa kwa kutupa masumbwi na pia kichwa cha bondia chenye mwili wa mwanasoka wenye miguu yenye vigimbi na tayari kupiga chenga na dana-dana.
Utambulisho wa asili wa watu hawa au ule utu wao unasimamia wapi kwenye vichwa au miili yao? Kama ni vichwa basi hoja yako ya mwili tutakuwa tumeipunguza mpaka kubakiza kichwa na kama ni kiwiliwili basi hoja yako itakuwa imeondolewa kichwa kama sehemu muhimu ya wewe ni nani. Hivyo je unaweza kusema ni kichwa na roho ndio ndio kinamfanya mtu awe yeye?
Lakini kichwa pia si kiungo ambacho hakina organs zinazoweza kubadilishwa na katika nadharia tayari viungo na sehemu muhimu kichwani vinaweza kuondolewa na kupandikizwa vingine. Pua, macho, masikio, ulimi etc ni baadhi ya viungo vinavyoweza kuwekewa mbadala kinadharia na tafiti halisi ziko tamati wakati baadhi ya viungo tayari sehemu zake kuu zinaweza kuondolewa na kupandikizwa za mtu mwingine mfano cornea transplants ambapo corneal ya jicho iliyoathiriwa inatolewa na kupandikizwa ya mtu mwingine (organ donor). Hii ni wazi baada ya muda si mrefu jicho zima litawezekana kupandikizwa la mtu mwingine na pia viungo vingine kichwani. Unaweza kusema basi vyote zi muhimu katika kubeba ule "u-mimi na u-wewe wa mtu" kama ubongo lakini nitaelezea thought experiments zenye kuuweka kwenye mizani na kusambaratisha hoja ya ubongo kama ndiyo sehemu iliyo utu au centre ya mimi au wewe ni nini.
CC JingalaFalsafa neo1