Mashaxizo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 6,707
- 3,346
Ukinisoma vizuri naposema ubongo nakuwa naongelea system ile ya ubongo ikiwemo spinal cord. Katika full body transplant ingawa haijafanywa bado lakini surgical procedures lazima zihusishe kuhamishwa kwa ubongo mzima ukiwa na spinal cord kama njia rahisi ya ku-ensure ufanyaji kazi wake kwa ufanisi baada ya operation. Njia ngumu ni kuikata spinal cord na kujaribu kuiunga na kipande cha ya yule organ donor. Ni mifano katika fikra bado ila inapelekea concept sahihi katika hoja ya mada hii.
Kudevelop kitu kingine tofauti na hivi viwili itamaanisha third and fourth person out of the swap!! Hii haiko sahihi kama utaangalia vizuri hii mifano. Information za huyu na za yule zitabaki kuwa information za aina mbili kamwe haziwezi kutokea za mtu mwingine wa tatu na wa-nne out of nowhere. Katika experiments hizi data za watu hawa hazichanganywi bali zinabadilishwa kutoka kwa huyu kwenda kwa huyu and vice-versa.
Mmmh! Itawezekana vipi kutoa ule udude wa ndani ya uti wa mgongo na kuupandikiza kwenye uti mwengine ukizingatia ule uko kama viloli? ukumbuke ukubwa na udogo wa vile vidude unategegemea na umbo la mtu. kwa maana nyengine kunabinadamu wapana (i know unene wa nyama sio issue) na wembaba pia kuna warefu na wafupi. Sasa itakuwaje kukiwa na tofauti hizo? let say mtu mfupi and/or mwembamba atawekwaje vile vigololi vya mtu mpana and/or mrefu?
Siwezi kusema haiwezekani at all coz wakitumia operation hiyo kwa watu wanaolingana umbo inaweza ikawezekana but risk ya hali ya juu mtu kufumuliwa uti wa mgongo. Sijui unaliongeleaje hilo.
But if wakifanikiwa kupandikiza kichwa na vilololi vya uti wa mgongo mtu husika ni huyo mwenye kichwa na vigololi vyake vya uti wa mgongo. let say yule mwanasoka atahitaji mazoezi tu ya mwili kuendelea na kabumbu kama alivyokua ikiwa mazoezi hayatomletea matatizo kutokana na uperation alizofanyiwa.