Nkwesa Makambo
JF-Expert Member
- Aug 26, 2011
- 4,763
- 1,319
Mkuu hapa huwa nabakia kutoelewa kitu kama roho (soul) ndio inakufanya wewe uwe wewe hapo ubongo unanafasi gani maana kitu kinachomfikilisha mtu ni ubongo kwa maana hiyo tuamini kuwa ubongo ndio Roho.
Mkuu hapa huwa nabakia kutoelewa kitu kama roho (soul) ndio inakufanya wewe uwe wewe hapo ubongo unanafasi gani maana kitu kinachomfikilisha mtu ni ubongo kwa maana hiyo tuamini kuwa ubongo ndio Roho.
Mkuu hapa huwa nabakia kutoelewa kitu kama roho (soul) ndio inakufanya wewe uwe wewe hapo ubongo unanafasi gani maana kitu kinachomfikilisha mtu ni ubongo kwa maana hiyo tuamini kuwa ubongo ndio Roho.
NAFSI ni KIITIKIO cha Ubongo na Mwili, yaani kiitikio cha Mental and Physical body. Ndio maana tunasemwa maiti imekosa nafsi (imekosa kiitikio cha ubongo na mwili kwa ujumla) Na hicho kiitikio ndio UMIMI na UWEWE wako (NAFSI).
Pia, ile hali ya kuitikia mental na mwili, ndio tuitacho Uhai.
Anaita sasa!
hakika kuna baadhi ya vitu ni tofauti kwa nfano katika matendo unaweza kuta watoto wa familia moja waliolelewa malezi mamoja ila wana character tofauti hii inaonesha kuwa tabia ya mtu ni haihusiani na experience katika maisha kwwa namna yeyote kuna kitu tofauti na ufaham na uelewa ambacho kina control matendona maamuzi ya binadam unaweza kuta mtu anajua alifanyalo ni baya na la hatari ila anatenda na hata kua na amani asipotenda hilo alitendalo na inafikia hatua kwa wengine hawezi jutia matokeo ya yatakayomkuta juu ya lile alitendalo kigezo cha kutumia akili katika kushape na kuishi vile tupendavyo kimeshindwa kwani mara nyingi tunaghairi bila logic reason na mwishowe tunaamua kutumia defence mechanism
ukija kuangalia kwa upande mwingine kuna kitu kinaitwa iman hiki sijui kinasimamia wapi katika analysation yako Monstagla maana imani kwa upande mwingine huwa inatufanya tuwe vile tulivyo na huwa tunajenga philosophy zetu za maisha kupitia iman ingawa pia experiens huja kuidistub iman kwa namna moja au nyingine kwa hiyo ukitaka kudifine who we are nadhani huwez kutumia kitu kimoja ni vitu vingi katika ushirikiano wako ndio inafanya tuwe vile tulivyo
Mkuu sajumo , nimevutiwa na mfano wako wa watoto wawili katika familia moja waliolelewa na wazazi wale wale. Tangu mtoto ana-develop ubongo tumboni kwa mama yake tayari ubongo ule unaanza kufanya kazi kubwa. Ukiachilia mbali upande wa ubongo unaohusika na kuendesha mwili mfano mapigo ya moyo, kubalance joto na kupumua, pia upande mwingine wa ubongo hasa ubongo wa mbele unaendelea kuzalisha neurons ambazo hizi hukusanya information nyingi sana kwa ajili kiumbe kuzitumia katika mazingira yake. Information zisizo na umuhimu hufutwa au hufutika kwa kukosa kurudiwa-rudiwa lakini baadhi ya information hujikita na kuwa na nguvu zaidi. Utaona mtoto aliyezaliwa siku chache anakuwa anaitambua sauti ya mama yake na kutulia pale anapoisikia hii ina maana anaweza kuwa kaisikia na kuizoea sauti hii ambayo tayari imejikita katika kumbukumbu ndani ya ubongo wake.
Pamoja na mazingira kuchangia uelewa na character ya mtu kwa kiasi kikubwa lakini si kigezo pekee. Mfano kuna genes ambazo hizi ni codes zenye nguvu ambazo tayari mtoto anazirithi kutoka kwa wazazi wake wawili nusu-nusu. Codes hizi (DNA) zina information muhimu ambazo ndizo huendesha mpangilio mzima wa mwili uweje na pia ubongo utafuata codes hizi za msingi katika ku-develop lakini kwa yale ambayo mtu atajifunza itakuwa ni matokeo ya mazingira kwa kiasi kikubwa.
Lakini pia viumbe vina uwigo mpana wa kufanya uchaguzi, kipi utunze katika ubongo na kipi usitunze. Katika hili hata mapacha wa kufanana (identity twins) waliokulia katika mazingira ya aina moja na wanaofanya kila kitu kwa pamoja bado hawawezi kuwa sawa kutokana na mfumo wa ubongo unapelekea uchaguzi binafsi. Mfano kwa dakika moja tu mapacha hawa wameletewa chai katika vikombe vinavyofanana. Ingawa kunywa kikombe cha chai kwa kawaida ni kama kitu kisicho kisicho na complication lakini ubongo wa kila mmoja katika tendo hili la kunywa chai utakuwa na ishara za umeme zaidi ya bilioni na baadhi zitatunzwa na nyingine zita-decay kwa muda mfupi.
Katika ishara hizi kila moja ni choice na hivyo mwisho wa siku experience ya chai katika kikombe inaweza kuelezewa kwa namna tofauti sana na mapacha hawa na hii ni kwa maelezo tu lakini implicit knowledge inayokuwa imetunzwa ubongoni itatofautiana kwa asilimia kubwa na pia kuna ishara zitakazofanana. Information ipi itunzwe na ipi ifutwe itategemea vigezo kadhaa pia ikiwemo previous experience ambayo hii ita-link ya yale uliyowahi kuyatunza mwanzo (mfano ladha, harufu etc) na pia mara ngapi ishara hizi zitajirudia au kuwa na kitu kingine cha kushikilizia ili iweze kudumu.
mkuu Monstgala hi mada tata sasa...nadhani kwa mfumo wa maswali au mjadala hautakidhi haja ya uelewa wetu,kumbuka si watu wengi saana tunaweza kuelewa mantiki ya hii kitu maana hata kujitambua kwenyewe huwa tunachelewa kujitambua.
hivyo hata mjadala utakuwa unapwaya..mfano ni ile mada yako ingine ya aliens.nadhani nayo uliileta kwa mfumo wa maswali,mjadala haukuwa mkubwa kama watu walivyotegemea..
unaweza kuta watu hatufahamu,hivyo hata maswali tunayouliza sio sahihi,au ni maswali mepesi kwenye hoja nzito na complex one.
ombi langu ni kuwa kama hutajali ungetufundisha kwanza afu baada ya hapo watu watauliza tutakuwa na maswali sahihi kuhusu na mjadala utapanuka zaid mkuu
ahsante saana mkuu Monstgala
Mkuu neo1, Nitajaribu kuelezea majaribio ya kinadharia kwa concept tofauti za mwili, ubongo, na ufahamu ili kufafanua zaidi. Majaribio haya ya kifikra yana-eliminate nadharia hizi tatu ingawa kwa njia ya kuweka mifano ambayo ni ndani ya fikra tu lakini iliyoegemea kwenye misingi ya ukweli.
Nijuavyo ni kuwa mwili una masikio kwasababu UNAHITAJI kuwasiliana kwa sauti,mwili una ubongo kwasababu UNAHITAJI kufikiri,haya yote yapo kwenye mwili kwasababu ni mwili na ni physicalMkuu ni wazi kuwa watu tunafikiri kwq kutumia ubongo...mtu ukiehakufa na ubongo wako nao unakufa....Roho yako ndio inabaki ikiwa hai...roho is non-physical...
Je kuna uhusiano wowote kati ya akili za kibinadamu na za roho? Km ni ndio, je hii roho huwa inafikiri kwa kutumia ubongo upi???
Km jibu ni hapana, uhusiano wangu na roho yangu unatoka wwpi???
Mkuu neo1, Nitajaribu kuelezea majaribio ya kinadharia kwa concept tofauti za mwili, ubongo, na ufahamu ili kufafanua zaidi. Majaribio haya ya kifikra yana-eliminate nadharia hizi tatu ingawa kwa njia ya kuweka mifano ambayo ni ndani ya fikra tu lakini iliyoegemea kwenye misingi ya ukweli.
Wanyama na wadudu walio hai au wenye vitikio vya ubongo na mwili pia wana hii nafsi? Kumbuka pia kuna viumbe wasio na ubongo lakini wako hai. Kwa mantiki hii inakuwa vigumu kuiona hii nafsi kama kitu kinachosababisha mwitikio wa ubongo na mwili pekee. Consciousness ni kitu kingine kikubwa ambacho ni wazi kinaweza kukosekana kwenye viumbe wengine ingawa wanaweza kuwa na mwitikio wa ubongo na mwili. Au sijakuelewa vizuri?
BKinachomfanya binadamu anakuwa kama alivyo ni zaidi ya kitu kimoja
Binadamu ni muunganiko wa mwili na roho kwa maana ya binadamu hai au mfu
Utu wa mtu unatokana na ubinadamu wake
Namna mtu anavyoyaona maisha na kuyatafsiri kunatokana na malezi yake ....!!
Mkuu Eiyer, shukrani. Unasema binadamu ni muunganiko wa mwili na roho, sawa ni mtazamo mmoja wapo lakini kitu cha ziada sana katika kutafakari hapa si suala la "binadamu ni nini" bali ni kipi hasa kinafanya mtu fulani ajione/ajitambue/ajihisi/ejielewe etc., kwamba ni yeye katika mjumuisho wote wa vitu vinavyoonekana na visiivyoonekana lakini vinavyoelezewa kama sehemu ya mtu.
Umetaja mwili + roho lakini kwa fikra thabiti zilizowazi za kinadharia zinaweza kutuonesha jinsi mwili wa mtu usivyo centre kwa kuwa ukipewa mwili wa mtu mwingine bado ule u-wewe wako utakuwa haukuondoka na mwili wako wa mwanzo. Ni fikra ngumu kidogo lakini zinaelezeka na zinaweza kuwa conceived na kukubalika. Hili linaondoa hoja yako kwamba lazima mwili wako na roho yako viwe vile vile ulivyozaliwa navyo ili uwe wewe. Kivipi? Nitaelezea kidogo kuhusu mwili.
Tunajua kwamba kuna maendeleo makubwa katika fani ya utabibu ambapo suala la kubadilishwa viungo vya mwili kwa kuwekewa vya mtu mwingine (organ transplants) si ajabu wala si geni tena. Viungo muhimu kabisa katika mwili wa binadamu kama moyo, mapafu, figo, ini, ngozi na vinginevyo vinapandikizwa katika mwili wa mtu mwingine na kufanya kazi kama kawaida. Pia majimaji katika mwili kama damu, maji etc pia yanaweza kubadilishwa na kuwekwa mengine na mtu huyu akaishi. Mwili mzima (kiwiliwili) kubadilishwa ni jambo lililo njiani na ni katika miaka miwili jambo hili linatarajiwa kufanyika katika utabibu kama litafikiwa kipitishwa na jamii. Linapingwa sana jambo hili lakini tayari kuna neurological surgeons na scientists wameweka wazi tafiti zao na majaribio ya uwezekano na jinsi ya kufanya operation hizi za ajabu kidogo.
Kwa hiyo kitu hiki kama kimefikia mahali hapo basi hatuna budi kudadavua katika fikra kwamba katika watu wawili wanaofanyiwa operation hii (1) Anayetoa kiwili-wili (mwili mpaka shingoni) na (2) Anayetoa kichwa, ni nani hasa atakuwa ni yule mtu baada ya operation hii. Kwa kuwapa identity watu hawa tuseme bondia na mwanasoka wanafanyiwa operation hii, kiwili-wili cha bondia na kichwa cha mwanasoka, nani atakuwa huyu mtu baada ya operation? majibu ya wengi yanaweza kuwa labda mwana soka kwa kuwa ndiye mwenye kichwa.
Lakini kabla hatujaanza kudhani tumemaliza mtihani huu twende mbele kidogo. Ikiwa operation hii itawezekana basi pia mbadilishano wa sehemu hizi kuu za mwili zitakuwa zimewezekana (Mfano kichwa na kiwiliwili). Hivyo Bondia na mwanasoka waki-swap vichwa, nani haswa atakuwa bondia na nani mwanasoka baada ya full body transplant operations hizi? Kwa maana hapa tutakuwa na kichwa cha mwanasoka chenye mwili wa bondia wenye mikono iliyokomaa kwa kutupa masumbwi na pia kichwa cha bondia chenye mwili wa mwanasoka wenye miguu yenye vigimbi na tayari kupiga chenga na dana-dana.
Utambulisho wa asili wa watu hawa au ule utu wao unasimamia wapi kwenye vichwa au miili yao? Kama ni vichwa basi hoja yako ya mwili tutakuwa tumeipunguza mpaka kubakiza kichwa na kama ni kiwiliwili basi hoja yako itakuwa imeondolewa kichwa kama sehemu muhimu ya wewe ni nani. Hivyo je unaweza kusema ni kichwa na roho ndio ndio kinamfanya mtu awe yeye?
Lakini kichwa pia si kiungo ambacho hakina organs zinazoweza kubadilishwa na katika nadharia tayari viungo na sehemu muhimu kichwani vinaweza kuondolewa na kupandikizwa vingine. Pua, macho, masikio, ulimi etc ni baadhi ya viungo vinavyoweza kuwekewa mbadala kinadharia na tafiti halisi ziko tamati wakati baadhi ya viungo tayari sehemu zake kuu zinaweza kuondolewa na kupandikizwa za mtu mwingine mfano cornea transplants ambapo corneal ya jicho iliyoathiriwa inatolewa na kupandikizwa ya mtu mwingine (organ donor). Hii ni wazi baada ya muda si mrefu jicho zima litawezekana kupandikizwa la mtu mwingine na pia viungo vingine kichwani. Unaweza kusema basi vyote zi muhimu katika kubeba ule "u-mimi na u-wewe wa mtu" kama ubongo lakini nitaelezea thought experiments zenye kuuweka kwenye mizani na kusambaratisha hoja ya ubongo kama ndiyo sehemu iliyo utu au centre ya mimi au wewe ni nini.
CC JingalaFalsafa neo1