Nini kinafanya uwe wewe? Ubongo? Mwili? Roho? Ufahamu wako?


🙂 Hapo kwenye highlight, hii nadharia inakuwa na changamoto kutoka kwa mhusika mwenyewe sio wale wanaomuona. Nina maana yeye mwenyewe, mwanasoka akiamka kutoka katika hiyo operation atakuwa au atajiona ni yupi? kichwa chake katika mwili mwingine au mwili katika kichwa kingine? Ndio wazo hili linapoegemea.
 

mkuu Monstgala kwa mtazamo wangu nazani huyu jamaa atajiona ni mwanasoka (kichwa) mwenye mwili mwingine lakini atakuwa na changamoto ya kupungukiwa U-YEYE

.made in mby city.
 
Last edited by a moderator:
mkuu Monstgala kwa mtazamo wangu nazani huyu jamaa atajiona ni mwanasoka (kichwa) mwenye mwili mwingine lakini atakuwa na changamoto ya kupungukiwa U-YEYE

.made in mby city.

Kama huyu mtu atajiona mwanasoka kwa kuwa kichwa ni cha mwanasoka (previously) basi mtu huyu u-yeye wake uko kichwani na kwa mtazamo wako tunafikia hitimisho la "u-mimi" upo kichwani au kichwa ndio hasa "u-mimi" wa mtu. Lakini nimetoa mifano ya viungo vilivyopo kichwa vyaweza kubadilishwa pia kwa maana hiyo wewe katika kichwa unamaanisha central part ni ubongo? kwamba huu sasa ukienda kwa mwingine (through organ transplant) na "u-mimi" utaenda nao?!! Au kiungo gani hasa kinashikilia "u-mimi" katika kichwa?
 

mkuu Monstgala
u-yeye wa huyo mtu unategemea central part yake ambayo ni ubongo in whatever the case
mf; mwili wa mwanasoka tuuache vile-vile na mwili wa bondia nao uwe vile-vile ila huyu bondia tukambadilishia ubongo tu kutoka kwa mwanasoka ila viungo vingine vyooote tukaviacha vile-vile basi perceptions za huyu mtu((let's call him NEW)) zitakuwa ni za mwanasoka na si bondia tena, kwani mwili, processes na systems zote za huyu NEW zitakuwa tayari controlled na ubongo wa mwanasoka
kumbukumbu na ufahamu wake utakuwa ni wa mwanasoka,
kwa upande wa challenges, NEW ata-face challenges nyingi zikiwemo za kimazingira ya mwili wake huo mpya

nirekebishe mkuu

.made in mby citu.
 
Last edited by a moderator:
Jibu hapa ni ubongo maana ufahamu upo kwenye ubongo
 
Jibu hapa ni ubongo maana ufahamu upo kwenye ubongo

Mkuu, ufahamu au data zote katika ubongo nazo zinaweza kufutika au kufutwa. Je "ufahamu" ukifutwa yule mtu huyu pia atakuwa kafutwa "u-yeye" kama yeye na identity yake? Mfano mzee mmoja kafikisha miaka tisini na saba na kutokana na uzee akapoteza kumbukumbu zote na ufahamu hasa aliokuwa zamani. Sasa mzee huyu hajitambui wala hajui jina lake hata kuongea pia hajui tena. Huyu mzee watu wake wakimwangalia wanaona ni mtu yule yule lakini yeye akiwaangalia anaona watu ambao hawajui na sehemu aliyopo na kila kinachoendelea hakitambui na pia hakumbuki chochote katika maisha yake. Hii ni dhahiri kwamba ufahamu na kila kitu ulicho-experience na kujifunza kinaweza kupotea pia kwa namna moja au nyingine mfano ugonjwa au ajali. Je ufahamu ndiyo haswa "u-mimi" wangu?

Kuna brainwashing programs ambazo mtu anaweza kuaminishwa vitu fulani na kuondolewa vile alivyokuwa navyo mwanzo katika memory zake. Kinadharia tunaweza kwenda mbali katika kuangalia possibilities za "u-mimi" au identity ya asili ya mtu inakuwaje ikiwa ufahamu utahamishwa.
 
Monstgala; nakunukuu "Mkuu, ufahamu au data zote katika ubongo nazo zinaweza kufutika au kufutwa. Je "ufahamu" ukifutwa yule mtu huyu pia atakuwa kafutwa "u-yeye" kama yeye na identity yake? Mfano mzee mmoja kafikisha miaka tisini na saba na kutokana na uzee akapoteza kumbukumbu zote na ufahamu hasa aliokuwa zamani. Sasa mzee huyu hajitambui wala hajui jina lake hata kuongea pia hajui tena. Huyu mzee watu wake wakimwangalia wanaona ni mtu yule yule lakini yeye akiwaangalia anaona watu ambao hawajui na sehemu aliyopo na kila kinachoendelea hakitambui na pia hakumbuki chochote katika maisha yake. Hii ni dhahiri kwamba ufahamu na kila kitu ulicho-experience na kujifunza kinaweza kupotea pia kwa namna moja au nyingine mfano ugonjwa au ajali. Je ufahamu ndiyo haswa "u-mimi" wangu?


=ndio
=ndio
Bila ufahamu siwezi kujitambua kwamba ni mm. ko u mimi wangu upo kwenye ufahamu ambao ndo ubongo
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nimekusoma......

Hii iko hivi kwa mtazamo wangu....

Hapa naona kama kuna mambo mawili

1:Sisi ni nani
2:Ni kitu gani kinatufanya tujitambue,tujijue na kujielewa ili tuweze kujibainisha na vilivypo kwa maana vinavyoonekana na visivyoonekana

SISI NI NANI

Swali hili linaweza kujibiwa na namna zaidi ya moja lakini kwa namna maelezo yako yanaonesha kuwa unalenga ile "sisi" ambayo inajitegemea hata kama mwili upo au haupo au umebadilishiwa mwili mwingine,kwa maana hii ni kwamba hapa mkuu unazungumzia ile nguvu iliyoko ndani yetu ambayo ndio inayoweza kuufanya mwili uwe na uhai na nguvu hii wengi huiita majina tofauti tofauti lakini kwa wengi hufahamika kama roho na sio nafsi,nafsi ni muunganiko wa mwili na roho.Sasa basi kwa maana hiyo ni kuwa sisi kwa maana ya nguvu inayoratibu miili yetu ni roho kwasababu hata ukihamisha mwili bado utaendelea kubalki wewe tu

Hata unapozeena bdo unaendelea kubaki wewe tu,hata ukibadili jinsia bado utaendelea kubaki wewe tu kwasababu kile kinachokufanya uwe wewe bado kipo ndani ya huo mwili haijalishi kichwa kimebadilishwa au laa,haijalishi umewekewa mwili wa chura au laa

KINACHOTUFANYA TUJITAMBUE,KUJIELEWA N.K

Hapa napo kunahitajika maelezo mazuri ili kuelewa na nitajitahidi kuandika kwa uwezo wangu wote,hapa kuna kumbukumbu na 'ufahamu",sijui kama nitaeleweka lakini wacha niendelee maana hili kidogo ni suala gumu kuelezea

Unapobadilishiwa mwili kama mfano wako unavyosema hapo juu na baadae ukazinduka utaona kuna kitu hakiko sahihi kwenye mwili wako lakini hiyo haitaondoa ukweli kuwa bado ni wewe [roho] utaona kuwa una mwili wa mcheza bondia lakini kumbukumbu zinakueleza kuwa wewe ni mchezaji wa kandanda,kwa maana hii ni kuwa kinachotufanya tujielewe na kujibainisha na vilivyopo kuwa sisi ni nani katika mkabala wa mazingira ni kumbukumbu

Lakini kuna ile hali ya kujijua kuwa wewe ni binadamu na una hadhi au "hali" fulani,hii inatokana na ufahamu,ili uweze kujua kuwa wewe ni binadamu na una hadhi fulani unapaswa uwe na ufahamu wa hilo ili uweze kujijua hivyo,bila ufahamu huwezi kujitofautisha na kunguru au mbuzi,yaani ile hali ya kujithibiti na kujua "mimi hadhi yangu sio kama mbuzi".....

CC: Mtambuzi .....!!
 

Mkuu asante sana kwa kuiweka hoja yangu katika maelezo mazuri zaidi na labda kutoka angle ya pili ambayo inafanya hoja iwe wazi au ieleweke zaidi. Nakubaliana nawe moja kwa moja katika elaboration yako hasa katika sisi ni nani na pia jinsi tunavyoweza kujitambua kotoka ndani kwa wakati wowote hata pale viungo vyetu na mawazo yetu yanapohamishwa au kuingiliwa. Hiyo hali fulani inayobakia kuwa hasa nguzo kuu ya sisi au mimi au yeye kwa namna ile ile tangu mtu anapozaliwa mpaka anapozeeka regardless of changes of the body, brain, data etc. Hata kaitika mifano ya kifikra ya ku-swap mwili, ubongo na hata data zile katika ubongo bado hali hii inabaki kuwa utambulisho sahihi wa asili wa mtu na hata utambuzi wa ndani kwa mtazamo wa mtu huyo mwenyewe.

Kama "hali" hii ndio roho basi kwa falsafa na fikra za wazi zilizo thabiti hali hii ni msingi mkuu wa u-mimi na kukataa kwamba hali hii haipo ni kukosa fikra au kujizuia kufikiri au simply denial. Huu ndio mtazamo wangu. Atasema mtu kirahisi kwamba hakuna roho lakini atashindwa kuielezea hali hii ni nini hasa na labda itapewa jina tofauti kwa kutegemea na mtazamo wa jamii na makundi tofauti lakini ni wazi hali hii ndio msingi wa "u-mimi" (inner perception) wa mtu au "u-yeye" (outer perception) wa mtu.
 

Mkuu Blackman, asante kwa kuweka wazi mtazamo wako ambao ni wa msingi kabisa. Kwamba ufahamu ndio haswa nguzo ya u-mimi wangu au u-yeye wa mtu fulani. nami napenda kukupeleka hatua ya mbali zaidi katika kufikiri ili uupime ufahamu katika hatua za majaribio ya kifikra na uone kama unabakia pale pale kwa perception hii uliyonayo.

Kuna wazo moja la kufikirika ambalo linaweza kuipima hoja yako ya "ufahamu" wa mtu.

Likoje jaribio hili?

Mtaalam mmoja wa falsafa anaiweka nadharia hii katika jaribio la wazo la kusafiri kwa teletransporter. Katika wazo hili error inatokea na ufahamu unakuwa katika sehemu mbili tofauti yaani katika miili miwili kwa wakati mmoja, kivipi?

Teletransportation inatafsiriwa katika wikipedia kama njia ya kinadharia ya kusafirisha maada au nishati kutoka sehemu moja hadi nyingine bila kuingilia nafasi au mpangilio uliyopo kati ya kile kinachosafirishwa. Kwa maana hiyo kama jiwe likisafirishwa kwa njia hii kutoka point A mpaka point B, mpangilio wa atoms, protons na electrons unaounda elements za jiwe lile hautaathiriwa bali utapangwa vile vile pasipo kukosa hata particle moja pale unapofika point B. Hii ina maana jiwe litatokea vile vile kama lilivyokuwa katika point A.

Kwa binadamu nadharia hii ina maana tutaweza kusafiri kwenda popote kwa muda mfupi kabisa kwa kuwa utaingia chemba hii (point A) alafu utatokea chemba nyingine iliyoko sehemu yoyote Duniani(point B) yenye mfumo wa usafiri huu. Huyu mwanafalsafa kwa kuisoma nadharia ya usafiri huu na ufanyaji kazi wake basi akaweka jaribio hili la error ndogo inayoweza kutokea na jinsi inavyoleta changamoto katika hoja ya "ufahamu" kama nguzo ya u-mimi.

Error hii inakuwa hivi, ni mwaka 2430 (future) mtu mmoja katika jiji la Dar es salaam anataka kwenda Tokyo kwa teletransporter. Kaenda katika kituo chenye chamber pale ubungo na kalipia huduma na kaingia chamber. Yule mhudumu pale kabonyeza mashine na baada ya dakika mbili mtu huyu kajiona bado yuko pale pale. Kinachotakiwa au kwa kawaida mtu huyu anatakiwa kuwa Tokyo baada ya mhudumu kubonyeza kitufe husika. Particles na information zote zinamfanya mtu huyu awe yeye zinakuwa scanned na kuwa "deleted completely" mara baada ya information na particle arragement 100% sawia kuwa formed katika destination chamber (point B). Kitendo cha mtu kuwa point B akiwa na hali ile ile ikiwemo njaa, emotions kumbukumbu, alama, mawazo na kila kitu kama kilivyo ni matokeo ya perfect information kuwa retrieved kule anakotokea kwa extreme speed.

Kwa hiyo kilichotokea hapa ni error katika part ya ku-delete particles na information za mtu huyu katika point A (Dar es salaam chamber) ndio maana mtu huyu bado anajiona yupo pale pale baada ya process hii ya teletransport. Mtu huyu anamuuliza mhudumu pale, "Nini kimetokea mbona bado niko hapa hapa?" Mhudumu anamwambia "Nadhani ni error kidogo maana katika screen yangu hapa naona tayari uko Tokyo na umetoka katika chamber unaelekea nje!" Mhudumu anaendelea; "ila haina tabu ingia tu tena kwenye chamber na tuta-delete kila kitu kwa kuwa tayari uko Tokyo hivyo hairuhusiwi kuwa sehemu mbili kwa wakati mmoja" Hapo sasa!!, mtu huyu hii ni kama death sentence, aingie chamber awe deleted? maana mwili na ufahamu wake uko replicated na tayari "yeye" mwingine yuko Tokyo. Mtu huyu anaanza kukimbia huku akilia lakini anakamatwa na walinzi anaburuzwa kwenda chamber ili awe deleted.

Kimsingi ni procedure ile ile ambayo ndiyo inafanyika ila sasa inaonekana kwa uwazi au katika vipengele nini kinatokea na ni ngumu kukubali kwa sasa maana the instant procedures zimecheleweshwa kidogo kwa error hii.

Hii ni paradox, na fear inayoainishwa hapa ni sababu kuu ya kukuonesha "ufahamu" si wewe maana ikitokea data zile zile zinazokufanya ujitambue au ufahamu, zihamishwe sehemu mbili katika wakati mmoja "ubinafsi" utakuwa umegawanywa mara mbili na hata mtu yule angeulizwa pale katika chamber kwamba basi yule yeye aliyeko Tokyo (point B) ndio akamatwe awe deleted angesema YES, niacheni mimi delete huyo na pia yule wa Tokyo angepewa choice hiyo naye angesema please delete huyo aliyeko Dar es salaam (point A)


U-mimi ni zaidi ya ufahamu.
 
hamna ufaham ndo u-mimi.
huo mfano uliotolea hapo chini kati mtu aliyeko chamber A na B ni kwamba hata ufaham wangu ukiucopy na kumpa mtu mwingine yaan tukawa 2 wenye ufaham wa aina 1, tabia zetu zitaendana kwa kila kitu
ila u-mimi kila mmoja atajiona ni yeye maana ufaham upo ndani yake na hakuna kiunganishi kati ya mmoja na mwingine[eg blutooth or WI-FI]
mimi najiona ni mimi coz ufaham upo ndani yangu hata kama angekuwepo mtu mwenye ufaham kama wangu bado ufaham wangu hautomtambua maana ufaham hauna macho
na nitaendelea kujitetea mimi kwa maana ufaham unanambia ni mimi wala sio sisi
 
Monstgala
hamna ufaham ndo u-mimi.
huo mfano uliotolea hapo chini kati mtu aliyeko chamber A na B ni kwamba hata ufaham wangu ukiucopy na kumpa mtu mwingine yaan tukawa 2 wenye ufaham wa aina 1, tabia zetu zitaendana kwa kila kitu
ila u-mimi kila mmoja atajiona ni yeye maana ufaham upo ndani yake na hakuna kiunganishi kati ya mmoja na mwingine[eg blutooth or WI-FI]
mimi najiona ni mimi coz ufaham upo ndani yangu hata kama angekuwepo mtu mwenye ufaham kama wangu bado ufaham wangu hautomtambua maana ufaham hauna macho
na nitaendelea kujitetea mimi kwa maana ufaham unanambia ni mimi wala sio sisi
 
Last edited by a moderator:
Haswaaaa mkuu hii ndivyo ilivyo na ndio maana wale ambao wakana uwepo wa nguvu hii [roho] wanaonekana kama hawatafakari kabisa...

Mkuu tupo pamoja ......!!
 
Mmmh! Hii mada! Mi nahisisi ukichanganya bondia na mwanasoka hapo utapata kitu chengine. Ikimaanisha yule mwenye kichwa cha bondia hatoweza kufanya kama alivyokua coz mwili unakua hauna mafunzo. hiyo ni sawa na yule mwenye kichwa kichwa cha soka atakavyoshindwa kusakata kabumbu kutokana na ule mwili wa bondia.

Mimi kama mimi siwezi kusema mtu ni ubongo or mwili or roho peke yake! but naweza kusema mtu ni ubongo na "uti wa mgongo" Hivyo vitu vinaathari kwa roho na mwili pia.

Uti wa mgongo ndio unaleta balance na uwezo wa mwili kufanya kitu fulani ubongo just unathink how utendaji wa jambo hilo utakavyokua. ubongo unaweza ukawaza sawa sawa but utekelezaji ukashindikana kutokata na controler of body 'uti wa mgongo' kutoweza kufanya hivyo!!! hii naifananisha na straiker mwenye uchu wa magoli but akapata nafasi na kushindawa kuact as he wish.

Hivyo basi mtu atakaeekewa kichwa cha soka na mwili wa bondia usishangae kudevelop kitu kingine tofauti na hivyo viwili.
 
Blackman, Katika thought experiments nilizoainisha, ufahamu au data katika ubongo ni temporary na zinaweza hamishwa sehemu hii na ile hivyo kama itatokea kuwa replicated basi tayari wewe pia unaweza kuona wazi udhaifu wa hoja hiyo kwa msingi kwamba unaweza kupotoshwa na ufahamu wako kwa kuwa tu hautatambua vinginevyo. Tunapotengeneza scenario hizi katika fikra tunajaribu kuangalia kitu kwa picha ya "uwezekano" kwamba hata mtu akiwa replicated kila kiungo yakiwemo macho yatafanya kazi kwa namna ile ile ya kawaida. Unaposema "ufahamu hautomtambua kwa kuwa hauna macho unakuwa umeenda nje sana na sasa unauchukulia ufahamu kipekee kama mtu. Hapana hizi ni systems na tunaposema ufahamu ukahamishwa tuna maana utafanya kazi pale ambapo utaungwa katika mwili mwingine wenye kila kitu kinachohitajika ili ufahamu ule uwe katika hali ya kawaida hapa nina maana ya organs zote za fahamu ziwepo.
 
Last edited by a moderator:

Ukinisoma vizuri naposema ubongo nakuwa naongelea system ile ya ubongo ikiwemo spinal cord. Katika full body transplant ingawa haijafanywa bado lakini surgical procedures lazima zihusishe kuhamishwa kwa ubongo mzima ukiwa na spinal cord kama njia rahisi ya ku-ensure ufanyaji kazi wake kwa ufanisi baada ya operation. Njia ngumu ni kuikata spinal cord na kujaribu kuiunga na kipande cha ya yule organ donor. Ni mifano katika fikra bado ila inapelekea concept sahihi katika hoja ya mada hii.

Kudevelop kitu kingine tofauti na hivi viwili itamaanisha third and fourth person out of the swap!! Hii haiko sahihi kama utaangalia vizuri hii mifano. Information za huyu na za yule zitabaki kuwa information za aina mbili kamwe haziwezi kutokea za mtu mwingine wa tatu na wa-nne out of nowhere. Katika experiments hizi data za watu hawa hazichanganywi bali zinabadilishwa kutoka kwa huyu kwenda kwa huyu and vice-versa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…