Nini kinaikumba Japan? Mwakani India inaipiku na kuwa Taifa la tatu lenye uchumi mkubwa Ulimwenguni

Wewe jua japan kuwa juu ni mpango wa mungu.............haiwezekani watu bilioni na usheeeeee uwapambanishe na watu milion sijui kumi na kitu sijui ishirini na kitu harafu watoke msuli sawa.......wewe mwenyewe uogopi??
🚮🚮
 
India bado sana siyo kuipata, hata kuifikia Japan.

Japan hawazaliani kama nzi, tofauti na wachina na wahindi.

Kinachotokea hapo ni sawa na familia yenye watu 5, kwa mwaka wanapata milioni 100, halafu kuna familia ya machokraa ina watu 50, halafu kwa mwaka wanapata milioni 110, halafu familia ya machokoraa inatamba kuwa imeizidi hiyo familia ya watu 5.

Japan's GDP per capita is much higher than India's:

  • Nominal GDP per capita
    In 2024, Japan's nominal GDP per capita is USD $33,138, while India's is USD $2,698.
    Hali ya mwananchi wa India ni aheri ya mwananchi wa Botswana au Namibia. Ndiyo maana wahindi na wachina unawaona wanazurura hovyo Dunia nzima kuhangaika ili wapate chochote maana nchini kwao maisha ni magumu kupindukia.
    Chuo kikuu kile cha ST Joseph waliajiri lecturers toka India kwa mshahara wa dola 500 kwa mwezi.


 
kwani kuna umuhimu gani kunapoongezeka pato la taifa ikiwa wananchi ni dhofu hali!!!

serikali zijitahidi kupunguz kodi,misaada ya nje na ijikite kuwaongezea thamani watu wake kwa kuwapa elimu.
Kati ya mataifa ambayo maendeleo ya wananchi wake, mwananchi mmoja mmoja, ni duni kabisa, ni pamoja na India na Bangladesh.
 
Hoja ni GDP in aggregate sio per Capita.

Na Cha muhimu Kwa Nchi ni hiyo GDP aggregate maana inakupa jeuri ya kukoroma.

Mambo ya per Capita ni distribution tuu nothing else
 
1. India ni Manzese iliyochangamka hata ikiipita China haibadilishi ukweli kuwa kife standards za raia wake ni mbovu kuliko.
2. Life standards za Wajapan na ustaarabu wao ni bora kuliko.

3. Kupitwa kwao ni mambo ya GDP ambayo kimsingi haimsaidii mwananchi mmoja mmoja kama hapa kwetu tunaambiwa uchumi unakua lkn umasikini ndio unazidi kwa wananchi
 
Na hapa ndio nakubali kama kwa miska 40 japan ilikuwa ni inchi ya 2 kwa uchumi duniani..........basi haina sababu ya kuwa wengi .........china na india walikuwa bilioni kira mmoja lakini ngono ndio ilikuwa kipaumbele chao na sio teknolojia wala maendeleo............wingi ni hasara japan itabaki kuwa juu kwa ubunifu na sayansi ya hali ya juu.....tokea dunia iumbwe hawa viumbe bila kupigwa nuclear na hayo matsunami ingekuwa no 1 duniani kwa uchumi
 
Zanzibar ni ndogo kweli lakini wanachojua ni kufi.........ra..........na tu................nakuibia tnganyika resources zao..........japan padogooo lakini walishawai mpaka kuibamiza china kijeshi na bado wanaibamiza kiteknolojia
 
makete sababu sio uzazi, ila ni vijana kuhamia mijini (mbeya, vyawa, tunduma, kyela, makambako, dar n.k) hivyo vijiji vinabaki na wazee na vijana wachache mno!

kule kuna vijiji utakuta wanaume under 50 wanaitwa vijana, na wenyewe hawazidi 20 kijiji kizima[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huwezi kuwa U.S vassal state ukatoboa. Japan na South Korea wanaiabudu sana Marekani

Angalia Ujerumani na nchi za Ulaya sasa hivi uchumi wao ulivyozorota
 
Ndio hayo hayo tu; ndio maana nikasema, sio muda mrefu Makete nayo itakuja kujifuta auto yenyewe. Mhe Bashe wakati vita vya Ukraine vimeanza na NGANO kua deal ni kama alitakaga kuanzisha mashamba ya ngano kule; sijui ile plan iliishia wapi. To me, that was more than genius
 
Hoja ni GDP in aggregate sio per Capita.

Na Cha muhimu Kwa Nchi ni hiyo GDP aggregate maana inakupa jeuri ya kukoroma.

Mambo ya per Capita ni distribution tuu nothing else
Lakini siku zote ubora wa maisha na quality ya services huwa ni Per capita. Ndiyo maana nchi kama Norway, Sweden, Finland, Kuwait, Qatar wananchi wake wanafurahia ubora wa maisha, huku wachina wakitangatanga kwenye mataifa mbalimbali wakiishi maisha duni kabisa mpaka ya kuishi kundi kama mbuzi kwenye chumba kimoja!!
 
Sawa ila Nguvu ya Nchi ni GDP
 
Huwezi kuwa U.S vassal state ukatoboa. Japan na South Korea wanaiabudu sana Marekani

Angalia Ujerumani na nchi za Ulaya sasa hivi uchumi wao ulivyozorota
Kama Japan, South Korea, Ujerumani na Ulaya hawajatoboa ni nchi gani sasa duniani waliyotoboa??
 
Pia Japan imejaa wazee! Mambo ya uzazi wa mpango usio na mpango umejibu.
Mbaya zaidi, Japanese wanajiona watu maalumu hawana utamaduni wa kukaribisha wageni - ni wabaguzi.
Mbona wenye uzazi wa mpango ulio na mpango hawajaifikia Japan??
Mbona sisi Tumekaribisha Wachina, Wahindi na Waarabu lakini hatujaenda popote??
 
Cha ajabu Kwa Human development index Japan wako juu ya India.
Yani Japan unaishi maisha bora mara mia ya India.
 
Sio kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…