Watu wengi wanatamani kufanya biashara wengine wana mitaji kabisa sababu unakuta yeye ni mtumishi hela sio swala la kuuliza ila when it comes to starting a business anajikuta anasita sita au kupatwa na uoga na jakamoyo!
Ijapokuwa kujiajiri na biashara ndio kitu ambacho kinaaminika kuleta utajiri katika maisha ya raia. Ni kipi kinakufanya au kilikufanya uogope kufungua biashara?
Binafsi mtazamo wangu kwa ujumla ninavyoona, uko hivi:
- Kwanza kuanzisha biashara ni kitu ambacho kitakupa jukumu zima la kufikiri wewe mwenyewe asilimia 100. Wakati ajira ukishapewa majukumu yako, umemaliza. Kampuni haipati faida, imepigwa fine, TRA wamefunga account wewe hujui hilo, unachotaka ni mshahara wako.
When it comes to business kufikiria solutions kunakuhusu. Na hakuna asiyejua namna kufikiria ilivyo kazi nzito.
- Kitu kingine ni ukosefu wa subra ( patience ).
Biashara mara nyingi siyo kitu unachoweza kuanzisha leo tu kesho ukawa Fred Vunjabei.
It takes lots of time, learning, failures, experience, trial and errors, mara njia hii, kesho ile.
Kuna vitu unaweza kuvisikia tu, lakini ukivifanya unakuta hali ni tofauti. Sasa ni either utafute njia yako upya au ukate tamaa.
- Jambo jingine ni uelewa wa watu kuhusu biashara, uwekezaji na uchumi bado uko chini sana.
Binafsi naamini hata mfanyakazi bado ni mfanyabiasha kwasababu anauza muda wake kwa masaa 8 kwa siku possibly na masaa mengine ya OT. Kwahiyo hapa ni suala la skills na negotiation if at all unajua kampuni unayofanyia kazi inakutegemea unaweza kuwapangia wakulipe vipi ( hili lipo sana kwa wachezaji wakiwa kwenye peak )
- Kitu kingine ni risk taking. Kuna watu wakipoteza hata laki tu, wanalia mpaka kamasi zinatoka. Ni ngumu sana kusema atafanya biashara anayohisi atapoteza. Hivyo ataendelea tu kusubiria biashara isiyo na risk miaka yote au kumbe hata haipo.
- Lastly, ni tamaa, ubinafsi, Kukosa uaminifu, na SifaMagu. Aisee nadhani mtu aliyefanikiwa kuwaroga wabongo kwenye mambo haya ALIFANIKIWA ASILIMIA 100.
Alituweza kikamilifu.
Siku zote mafanikio huwa hayakai mbali na ushirikiano ndio maana hakuna kitu kigumu mnooo kukifanya kama ushirikiano.
Kwetu sisi ukiwa na kimtaji chako unakomaa mwenyewe miaka nenda rudi hakikui, ukisema umpe mtu aunganishe mkuze mtaji anapotea na pesa yako. Mkisema kukopa wabongo hawaheshimu kabisa mikataba na makubaliano.
- Wengine hawako tayari kufanya biashara halali na kusubiri. Wanatafuta mafanikio ya haraka. Na hawa ndio wahanga wakubwa wa pyramid schemes.
Kwahiyo hizi ndio challenge kubwa zinazofanya watu kwa ujumla wanashindwa kuanzisha biashara.