Nini kinakuogopesha kufungua au kufanya biashara?

Nini kinakuogopesha kufungua au kufanya biashara?

best thread ever..
wale wa mil 3 nifanyie biashara gani mnasemaje nyinyi??
 
Hofu kubwa kwasasa - Nahofia kupoteza muda na mtaji kwenye biashara, bila ya kupata faida au kuambila hasara
 
Biashara inahitaji usimamizi. Na hicho ndicho kinacho tufanya wafanyakazi wengi kuogopa. Lakini pia wengi tunakosa wazo bora la biashara.

Na badala yake tunaigana igana tu! Jambo hili huchangia sana kushindwa na kukata tamaa mapema.
Unaweza kuwekeza kwenye biashara ambayo ipo na ina msimamizi tayari. Au ubaweza tafuta mtu mwenye wazo zuri, ukawekeza fedha na muda wako wa ziada kama co founder. Mfano unakuta mtu ni Director mahali ana uzoefu wa kiuongozi na usimamizi. Pesa anazo. Anashindwaje kupata kijana passionate na kuwekeza fedha na kumsaidia usimamizi kwenye biashara ambayo let say ana 49% ya hisa?

Kwanza kijana atapiga mzigo kwa sababu yeye ni majority shareholder na hawezi kujiibia. Pili uzoefu wa co founder utamsaidia sana kijana katika namna ya kuenenda na baadaye kwenye talent hiring.

Nadhani hii ya usimamizi ni sababu isiyo na mashiko kwa karne hii
 
Yes ndio biashara ya wavivu wa kufikiri hio always wanakimbilia kujenga nyumba za kupangisha raia!

Its a good business tho na haina hasara kama utaweka strong and strict management ila inapendeza uifanye on a prime area lasivyo payback period yake inachukua muda mrefu sana! Kwangu hii naiona ni biashara inayowafaa wenye hela ndefu ambaye anaweza akasimamisha floor hata 7-10 kwenda hewani! Ni sehemu ya kutunzia hela ambayo huihitaji kwa haraka!

Ila uzuri wake mwengine ni kuwa inaanza kukupa kodi straightaway ukiingiza mpangaji tu! Hiki ndio watu wanapenda
Hizi sio level zetu. Hebu tuzungumzie biashara za chips na mishkaki nami nipate pate point.
 
Back
Top Bottom