Nini kinazuia CHADEMA na CCM wasikae mezani kuondoa huu mzozo?

Umesema kwa uchungu sana
 
Huu ni wazimu ama uendawazimu?

Hivi CCM huwa mnapata wapi ujasiri wa kuwabagaza watanzania kwa kisingizio kwamba kuna tatizo kati ya CHADEMA na CCM?

Tatizo ni CCM kulazimisha mambo yasiyokubaliwa na wananchi na wala tatizo siyo CHADEMA na CCM.
 
Ccm walizoea kuburuza vyama vya upinzani, na cdm wamegoma kuburuzwa na ccm.
 
Ccm ndiyo tatizo wanajua kabisa kuridhiana na CHADEMA ndiyo mwanzo wa safari yao ya kuondoka madarakani na hawako tayari kwa hilo, wanajua kabisa Chama chao hakina tena sera wala mvuto kwa wananchi kama ilivyo CHADEMA, wao hawako tayari kwa maridhiano ya ukweli bali wanataka maridhiano ya maigizo ili waonekane na jumuiya za kimataifa kuwa wanalinda demokrasia kumbe ni wauaji wakubwa wa misingi ya kidemokrasia na amani ya kweli
 
Upo upande unaobeba vichwa vya kenge badala ya vichwa vya binaadamu
 
CCM NI WAPUMBAVU SANA MKUU, LAKINI NITAKUJIBU KWA KIFUPI ANAEVUNJA UTULIVU/AMANI NI....

1. Anayeteka watanzania Wenzetu akina Soka, Polepole, Mdude, Chaula nk.

2. Anayepiga watu Risasi Akina TUNDU LISSU, SATIVA AKWILINA MAWAZO NK

3. Anayezuia haki ya Kikatiba ya Mikitano ya Vyama vya siasa.
(Kushiriki mikutano ya hadhara na Mikutano ya ndani.

4. Anayezuia Maandamano ambayo ni haki ya kikatiba ya Tanzania.

5. Anayezuia na Kupora Haki ya watanganyika ya kuchagua kiongozi wanaye mtaka.

6.Anayeficha Kila aina ya mikataba, Bandari, Ardhi, Dhahabu, Gesi nk.

7. Anayekandamiza uhuru wa vyombo vya Habari

CCM WAMETUONA WATANGANYIKA NI MALOFA SANA


AMKENI WATANGANYIKA.
 
for sure!

ibara za katiba ya nchi zimesiginwa kwelikweli. Hasa ibara ya 3 na ya 8. Ya 20 (1) pia

kutawala kwa kutegemea mitutu ya bunduki ni upumbaf

Bwana wa mabwana Atafanya jambo soon!!!!
 
TZunachohitaji ni maridhiano lisu atolewe hata kama ikiundwa serikali ya nusu mkate na haya ndiyo maelekezo ya jumuia na serikali za kimataifa
 
Ccm wanamfanya mtanzania Kama kitega uchumi Chao kwahiyo Kila mwenye mawazo mbadala kwao ni mhaini anastahili kifo shida ndio hiyo
 
HIVI ILE TUME YA UCHUNGUZI IMEFIKIA WAPI KAZI YAKE ?
 
Kwanza tujue kati ya CCM na CHADEMA nani anajali huo uliouita "mustakabali wa nchi". Baada ya hapo tuendelee na Mjadala!
 
Uenyekiti wa CHADEMA Taifa ulipobadilishwa tu, papo hapo Tanzania mpya ikaanza kunukia!
 
kwa taarifa za siri nilizonazo ccm ba chadema wanaongea kwa siri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…