Nini kinazuia CHADEMA na CCM wasikae mezani kuondoa huu mzozo?

Nini kinazuia CHADEMA na CCM wasikae mezani kuondoa huu mzozo?

Assalam alaykum
Kila mtu anafahamu kuwa nchi inapita kwenye mapito magumu mno kutokana na mzozo wa vyama hivi na kutunishiana misuli CCM wanatumia dola huku CHADEMA wakiwekeza katika harakati na madola makubwa ya dunia
Hali hii inatuvuruga sana kiuchumi na kisiasa na kimahusiano ya dunia

Swali langu ni je
Nini kinawafanya makundi haya yssikae kuleta suluhu kwa mstakabali wa nchi

..Ccm wanaogopa wakienda kwenye maridhiano wataumbuka kwa kulazimika kutekeleza yale ambayo wamekuwa wakiyapinga, au wakiyakwepa, kwa muda mrefu.

..kwa mfano, maridhiano yatasababisha genge la watekaji lijulikane ni kina nani, na wachukuliwe hatua. Pia maridhiano yatalazimisha Tume ya uchaguzi irekebishwe, mahakama ziwe huru, Katiba iandikwe upya.

..Sasa Ccm inaogopa matokeo ya maridhiano kwasababu yatafukua mambo mengi mabaya waliyotufanyia wananchi kwa muda mrefu.
 
Assalam alaykum
Kila mtu anafahamu kuwa nchi inapita kwenye mapito magumu mno kutokana na mzozo wa vyama hivi na kutunishiana misuli CCM wanatumia dola huku CHADEMA wakiwekeza katika harakati na madola makubwa ya dunia
Hali hii inatuvuruga sana kiuchumi na kisiasa na kimahusiano ya dunia

Swali langu ni je
Nini kinawafanya makundi haya yssikae kuleta suluhu kwa mstakabali wa nchi
CCM haina mgogoro na Chadema. Wanakaa kusuluhisha nini?
 
Niwe tu mkweli bila serikali kusema na kuhakikisha wamewajibishwa wale wote waliotoa amri ya kuua, na wale walioua watu october 29, huwezi kuona chadema wameridhiana na hao jamaa. tuko hapa labda muwaloge wapoteze kumbukumbu
 
Swali langu ni je
Nini kinawafanya makundi haya yssikae kuleta suluhu kwa mstakabali wa nchi
Hili kweli ni swali unalohitaji msaada kulijibu?

Wewe hujui kuwa Samia na Genge lake (nasita sana kuihusisha CCM kama chama, kwa sababu sasa hivi haipo) wapo madarakani kwa mabavu, na nia ni kuendelea hivyo hivyo.
Hili hulijui, au unatafuta tu kupotezea watu muda kujibu swali unalojuwa jibu lake ni nini?
 
Assalam alaykum
Kila mtu anafahamu kuwa nchi inapita kwenye mapito magumu mno kutokana na mzozo wa vyama hivi na kutunishiana misuli CCM wanatumia dola huku CHADEMA wakiwekeza katika harakati na madola makubwa ya dunia
Hali hii inatuvuruga sana kiuchumi na kisiasa na kimahusiano ya dunia

Swali langu ni je
Nini kinawafanya makundi haya yssikae kuleta suluhu kwa mstakabali wa nchi


Lazima kuwe na mpatanishi wa kuaminika na wote kutoka nje ya Tanzania bila hivyo ni kujidanganya. Pili nimlazima kuwe na katiba mpya
 
Hiyo issue usiirahisishe hivyo kama vile ni ugomvi wa CHADEMA na CCM

Hili ni jambo kubwa. Ni watawala na watawaliwa

Wanaotoa idhini ya kutawaliwa wamepokwa mamlaka yao na watawala wameota mapembe

Ni ugomvi kati ya haki na udhalimu

Hili jambo usilidogoshe
Umejibu vyema sana, lakini tazama huyo huyo aliyeuliza swali alivyoelewa maelezo haya yanayojitosheleza kabisa
Hata kama ndivyo kwani hayazungumziki
Unayo matatizo gani ya kuelewa yaliyoandikwa, au ni ulaghai ule ule wa ki-Samia unauweka kazini?
 
CCM walifanya maridhiano karibu mara tatu na upinzani Zanzibar ni kipi walichokiheshimu? Nafikiri kilichobaki vyama vya upinzani ni kupigania uhuru upya kwani CCM ni zaidi ya mkoloni
Samia anatumia 'script' ile ile iliyozoeleka.
Sina hakika kama atafanikiwa.
Haya yanayomkabili hana uwezo wa kuzima akili za watu.
 
1:Kiburi
2:ujeuri
3:maslahi 4:visasi
5:kukosa ukomavu wa kisiasa 6:Elimu 7:udini 8:kukomoana 9:Uonevu
Namba 5 ina make sense zaidi 😳 !
Hata mashuleni na mavyuoni watu wengi wanasoma lakini wanaoelimika kutokana na masomo yao ni wachache 🙄 !

Na kingine wale ma Genius think tank waliwadharau nao wakaamua kukaa pembeni kama watazamaji !
 
Samia anatumia 'script' ile ile iliyozoeleka.
Sina hakika kama atafanikiwa.
Haya yanayomkabili hana uwezo wa kuzima akili za watu.

Samia hana anachokiamua hapo huyo ni robot aliyewekewa program na gengi linaongozwa na Godfather wa Msoga
 
Back
Top Bottom