A
Anonymous
Guest
Kwa sasa, karibu kila huduma muhimu kwa watumishi imehamishiwa kwenye mfumo wa e-UTUMISHI (ESS). Kupitia mfumo huo, mtumishi anaweza kuomba likizo, mikopo, uhamisho, kuongeza wategemezi, kupata salary slip, na huduma nyingine nyingi bila usumbufu wa kufuatilia makaratasi kutoka ofisi moja hadi nyingine.
Hata hivyo, jambo moja ambalo bado halijaingizwa kwenye mfumo huo ni masuala yanayohusu uanachama wa vyama vya wafanyakazi. Hili linazua maswali mengi miongoni mwa watumishi. Je, Utumishi Makao Makuu hawalioni tatizo hili, au kuna sababu nyingine inayozuia huduma hii kuwekwa kwenye mfumo?
Hadi sasa, watumishi wanaotaka kujitoa au kuhamia chama kingine cha wafanyakazi wanalazimika kuandika barua na kuzunguka nazo katika ofisi mbalimbali za halmashauri na taasisi zao. Mara nyingi barua hizo hupokelewa lakini hazifanyiwi kazi kwa wakati, huku baadhi ya watumishi wakisubiri kwa miezi kadhaa bila kupata majibu au mafanikio yoyote.
Aidha, kumekuwa na malalamiko kwamba baadhi ya ofisi za vyama husika huwa hazitoi ushirikiano wa kutosha kwa wanachama wanaotaka kujitoa. Wakati mwingine watumishi hukumbana na urasimu mkubwa unaowakatisha tamaa katika kutekeleza haki yao ya kuchagua chama wanachotaka kujiunga nacho.
Kutokana na changamoto hizi, tunaomba Serikali na mamlaka za utumishi zieleze ni nini hasa kinachozuia huduma za vyama vya wafanyakazi kuunganishwa kwenye mfumo wa ESS kama zilivyo huduma nyingine za kiutumishi.
Iwapo hakuna sababu za msingi zinazozuia jambo hili, tunashauri mfumo uweboreshwe ili kumwezesha kila mtumishi kuchagua kwa uhuru chama anachotaka kujiunga nacho, kubaki nacho au kujiondoa kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
Aidha, mfumo unaweza kuweka masharti maalumu yatakayodhibiti mabadiliko ya mara kwa mara ya uanachama. Kwa mfano, mtumishi anapojiunga na chama fulani aweze kubaki mwanachama kwa kipindi maalumu kilichowekwa, kama vile miaka minne, kabla ya kupewa fursa ya kufanya uamuzi wa kuendelea na chama hicho au kuhamia chama kingine. Hii itasaidia kulinda utulivu wa vyama huku ikiheshimu haki ya mtumishi ya kufanya maamuzi kuhusu uanachama wake.
Tunaamini kuwa uwekaji wa huduma hizi kwenye mfumo wa ESS utaongeza uwazi, kupunguza urasimu, kuondoa usumbufu usio wa lazima, na kulinda haki za watumishi wa umma.