Tulifeli kwa sababu msimamizi mkuu alishindwa kazi yake ya kusimamia. Enzi ya nyerere watu wakikosea au wakihujumu badala ya kuadhibiwa alikua anawabsdilishia ofisi/idara. Niliwahi kusikia tanzania tulinunua ndege ambayo baadae ilionekana kuwa mbovu. Wakati huo waziri wa mawasiliano na uchukuzi alikua Augustine Mwingira, alisimamia mchakato wa manunuzi ikiwa pamoja na kwenda ulaya kushughulikia ununuzi huo. Walicholeta kikawa uozo, na nyerere hakumwajibisha Mwingira na wenzake. Huo ni mfano mmoja tuu kuonyesha nyerere alivyofeli na kutufelisha.
Tulifeli kwa sababu msimamizi mkuu alishindwa kazi yake ya kusimamia. Enzi ya nyerere watu wakikosea au wakihujumu badala ya kuadhibiwa alikua anawabsdilishia ofisi/idara. Niliwahi kusikia tanzania tulinunua ndege ambayo baadae ilionekana kuwa mbovu. Wakati huo waziri wa mawasiliano na uchukuzi alikua Augustine Mwingira, alisimamia mchakato wa manunuzi ikiwa pamoja na kwenda ulaya kushughulikia ununuzi huo. Walicholeta kikawa uozo, na nyerere hakumwajibisha Mwingira na wenzake. Huo ni mfano mmoja tuu kuonyesha nyerere alivyofeli na kutufelisha. Unaposema tungekua na rais mwingine nchi haingekua na utulivu unajidharau mwenyewe na kutudharau Watanzania kuwa nyerere asigezaliwa (au angefariki angali mtoto) hatungeweza kujisimamia. Hivi nchi zote zenye utulivu na ustawi ni nyerere aliwasimamia? Jaribu kufiri vingine kuwa nyerere ndiye aliasisi kufeli kwetu, hata yeye mwenewe alikiri. Mfano katiba hii ya ovyo tuliyonayo ilitungwa yeye akiwa kiongozi mkuu. Miaka ya 1980-1985 alipoona siasa zake zinafeli, akaamua kukaa kando kidogo. (Kumbuka aliendelea kuwa na ushawishi hata kutuamulia nani anafaa kuwa kiongozi na nani hafai). Kwa sababu ya mfumo alioucha kuendelea kumtukuza yeye, kukosa vyombo huru vya kumchambua uongozi wake- mazuri yasewe, mapungufu na mabaya yasemwe,tumebakia tuu kumwona kama alikua masihi.