Nini kipimo cha Akili?

Nini kipimo cha Akili?

Nakubaliana na wewe mkuu.Lakini hapo inapokuwepo nini kinafanya tuseme unaakili na hapo isipokuwepo au inapokuwa kubwa ni nini kinasababisha haswa. Kwa mfano kwa upande wa darasani mtu akipata maksi nyingi ndo huwa tunamchukulia kuwa. ndo anaakili sana lakini mtu hyo ukimpeleka upande B hawezi kufanya kama darasani na kwa kile alichokishindwa basi watu watamwona hana akili.
Kila akili, ina mahala pake, kutokana na karama.. kuna mtu yake ni darasani ndio upeo wake unaonekana. Mwingine ni michezo...mwingine ni kwenye uwizi...mwingine kutafuta pisi..

Yani ndo talent iyo...au talanta.

Maarifa ni unapoweza kufanya sasa iyo talent ionekane... kuna sehemu hali ya maisha inakufanya lazma maarifa ili talent ionekane, sehemu zingine ni wewe tu kujiachia na talent yako ....maanake kila kitu kipo set.

Sasa akili inatumia ubongo...kama kwa mfano mtu ubongo wake haujakaa fresh...sio kwamba hana akili.... ni sawa na dereva mzuri awe na gari bovu.

Ila pia kuna depression mpaka akili inazima data pande flani za ubongo maanake inapata stress sana...ndo ile ukichaa...hapo ni dereva kaweka gari free kwenye mteremko...kwa iyo kwenye mlima haipandi
 
Nimejaribu kujiulizaa, hivi akili ya mtu huwa inapimwa na nini? Mpaka inafikia mtu anakuambia hauna akili wewe. Maana ukifeli mtihani unaambiwa huna akili je mtihani ndio kipimo cha akili, ukishindwa kufanya jambo fulani pia utaambiwa huna akili🤔, Kwanini?

Hapa kwa upande wangu nachofahamu kuwa kwa upande wa shule mwanafunzi huwa tuna mjaji kwa mitihani na hiyo bado hata kama akifeli sidhani kama itakuwa sawa kusema hana akili, bali atakuwa ameshindwa tu kufaulu kwenye hiyo mitihani maana kwa upande mwengine mtu hawezi kujua masomo yote atajua baadhi tu ya hayo sasa kama ameweza kufaulu kiingereza akashindwa kufaulu hesabu bado utasema hana akili.

Pia kuna mwengine kuhusu masomo hawezi ila kuna kitu ataweza kukifanya nje ya hayo masomo tena akafanya vizuri zaidi bado utasema hana akili? Pia tukija swala la utendaji kitu fulani au kazi fani, utakuta mtu hakufanya kwa uweledi mzuri bado ataonekana hana akili je nisa hihii kusema hana akili au hana uzoefu na uweledi na hilo?😥

So ni nini haswa kipimo cha akili na kwa nini tuseme mtu hana akili?🤔🙏 Ni mawazo yangu yanayoitaji msaada.
AKili ni ule uwezo wako wa kutambua mazingira uliyopo na kuishi kwa namna ya mazingira husika..!! ukienda tofauti na mazingira husika hapo ndo tutakuhesabu kuwa huna akili
 
Kila akili, ina mahala pake, kutokana na karama.. kuna mtu yake ni darasani ndio upeo wake unaonekana. Mwingine ni michezo...mwingine ni kwenye uwizi...mwingine kutafuta pisi..

Yani ndo talent iyo...au talanta.

Maarifa ni unapoweza kufanya sasa iyo talent ionekane... kuna sehemu hali ya maisha inakufanya lazma maarifa ili talent ionekane, sehemu zingine ni wewe tu kujiachia na talent yako ....maanake kila kitu kipo set.

Sasa akili inatumia ubongo...kama kwa mfano mtu ubongo wake haujakaa fresh...sio kwamba hana akili.... ni sawa na dereva mzuri awe na gari bovu.

Ila pia kuna depression mpaka akili inazima data pande flani za ubongo maanake inapata stress sana...ndo ile ukichaa...hapo ni dereva kaweka gari free kwenye mteremko...kwa iyo kwenye mlima haipandi
Hahahaha...Umetisha sana ndugu
 
Akili ni uwezo wako wakujifunza kila siku, ukiona unafanya vitu haviendi halafu haujifunzi jua kuwa huna akili ila ukiona kila moment unayopitia unapata somo fulani basi jua unaakili nyingi sana.
 
Akili hupimwa na changamoto mtu anazotatua na kama atatatua kwa weledi basi huyobana akili ila kama changamoto za maisha za mgalagaza kwa mda mrefu mtu huyo huchukuliwa kama fala au zoba
[emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Wazungu washenzi sana.

Yalikuja na falsafa yao ya kipuuzi ya kuifafanua akili kwa kipimo cha IQ test na upuuzi mwingine ufananio na huo kama vile Shule na ufaulu wa masomo ya hesabu.

Kiujumla akili haina vipimo na mpaka leo hii asikudanganye mtu, hakuna aliyefanikiwa kutoa kipimo sahihi cha akili, maana akili huwa na tabia ya kubadirika, na haina mwisho, hivyo ni ngumu kupima kitu kisichotabirika wala kisicho na limitations.

Ni kama kinyonga kutaka kujua rangi yake halisi, ijapokuwa hana rangi sahihi, hivyo kumconclude kuwa ana rangi ya kijani et sababu huonekana mara nyingi na huo muonekano huo ni uongo na upumbavu.

Kumpia mtu kwa kigezo cha IQ test na masomo magumu, huo nao ni upuuzi vile vile, maana kama nilivyosema, akili ya binadamu hubadirika kulingana na mazingira, mood, hali ya kiafya, na mengineyo,

hata mwanafunzi anayefaulu sana leo hii anaweza kuja kuwa kilaza wa baadae ambaye kwa vigezo vya vipimo vya wanasayansi uchwala, basi mtu huyo ataonekana ana upeo mdogo wa kufikili ama akili, je zile za mwanzoni zilienda wapi?.

Hata yule mwanafunzi unayempima leo hii kwa vigezo vya kumbukumbu na upuuzi kama huu, ukiona kafeli, kumbuka kuwa kuna kesho huwa wanabadirika na kuwa hodari wa kufaulu hizi tests za vipimo, ushahidi mnao, kuna wale mlisoma nao walikuwa vilaza, lkn end of days wakaja kuwa superior wa kufaulu the same way kwa wale waliokuwa wanafaulu na kuja kuwa vilaza, je akili zilienda wapi?

Ukijiuliza hapo utapata kujuwa kuwa, viwango vyao vya ufaulu vilibadirika sababu mbalimbali, mybe, mood ya mwanafunzi, hali ya kimaisha, hali ya kiafya, hizi zote huweza sababisha mtu uwezo wake wa ufaulu kushuka ama kupanda, hivyo hizi haziwezi kuitwa ama kuwa vipimo vya akili[emoji23][emoji23].

Pia akili haipimwi kwa uwezo wa kuvumbua ama kusolve mambo, maana ukimya/utulivu pasipo kufanya jambo lolote nayo ni akili, tena akili ambayo imelala,

Akili ni suala zito ambalo wahuni wa kileo wamekuwa wakilidadavua kwa upendeleo na ubaguzi mkubwa, wakitumia vipimo vinavyowafurahisha wao na kuwabagua wengine.

Huwezi kusema mchina/muisrael ana akili kulko mwafrika wa madongo kuinama huku maporini, kisa kule kwao kuna maendeleo.

Hiyo si akili, kama nilivyosema mwanzo, ukimya na kutothubutu nayo ni akili, akili iliyolala, hivyo, huwezi kumconclude mtu huyo asiyethubutu ama kutatua changamoto fulan kuwa hana akili, kisa hajathubutu, huo ni uongo, ni sawa na kusema mtu fulan hana ugonjwa wa TB kisa hajapima huo ugonjwa na haoneshi dalili za ugonjwa hii sio sahihi wala njia nzuri ya kuhitimisha Afya ya mtu huyo, mpka pale utakapompima na kujua si ndivyo?.

Hivyo hata ktk maisha, kila mtu anakipimo chake sahihi cha kupimwa uwezo wake wa akili, na kwakuwa hakuna ajuaye kiwango chako sahihi cha mipaka ya kufikili kwako, hivyo hawezi hitimisha kwa kukupa percentage fulani za akili, maana hajaingia kichwan mwako kuona viwango vya mwisho vya ufikili.

Acheni kudanganywa na hawa wanasayansi wapuuzi puuzi wanaoibuka na masomo yao ya kihuni kuanza kudadavua mambo ambayo hata wao yamewapita uwezo wa kuyaelezea.

Akili ni uwezo wa mtu kutumia Sense zake vizuri kwa manufaa yake ama jamii yake bila kumuumiza mwingine,

I mean, akili ni uwezo ambao kila mtu anautofauti na mwingine, uwezo huo ndio hukupa kazi ya kutambua mbaya na nzuri, mema na ovu, pia control hisia zako na matumizi sahihi ya milango yote ya fahamu, kuanzia physically sense mpaka spirituals sense.

Niishie hapa nisije wachanganya
 
Pia, kutofanya yale mambo yanayohitaji akili uyafanye, ama fikra zinazohitaji utumie akili kufikiri pasipo kuendeshwa na hisia& shuruti za nukuu zinazokuwekea limitations kwenye kuhoji,

hapa napo mtu afanyaye haya tutamuita mpumbavu, japo huwa tunawaita wasiopenda kutumia akili kufikili wale wapinga ukweli, huwa tunawaita ''hawana akili" hili si sahihi, maana hao wote wana akili, isipokuwa wamejizibia viwango vya kufikili kwa sababu mbalimbali zinazowazuia kuhoji,ama kufikiri nje ya box

Sababu hizo zinaweza kuwa, mapenzi ya upofu, yaan huoni wala husikii maonyo ya watu kuhusiana na ubaya wa huyo umpendaye, pia mahaba ya siasa, mahaba ya dini, mahaba ya itikadi mbalimbal iwe kiuchumi,kijamii, ama kivyovyote vile.

Mtu huyu anapopinga really facts hatakiw kuitwa hana akili, bali aitwe mpumbavu, mjinga, mpuuzi, mshenzi, na matusi mengine yatakayomfaa kumdefine kuendana na uhalisia wake.

Akili ni kutenda na kuishi kulingana na ukweli halisia, na kweli sikuzote ndio Haki na Amani baina ya jamii zote dunian
 
Back
Top Bottom