Nini kitafuata ikiwa maandamano ya D9 hapo kesho hayatofanikiwa?

Tarehe 28 mliropoka hivi hivi
 
Maria Kawaongoza vibaya vijana wa Gen-Z, maandamano ya October 29 yalishafanikiwa sana, ilitakiwa kusafiria hayohayo.
Maandamano ya kesho yakifeli yataharibu mafanikio makubwa ya october 29
This is very true.Yale maandamano yalitosha kabisa ili kuwapa Serikali nafasi ya kushughulikia kero.Kesho watu hawataandamana na ni itakuwa ushindi kwa makabaila na mafisadi.Tatizo Maria ana mihemuko .
 
Kabisa.Wanaogopa kesi za uhaini.Hivyo maandamano hayana viongozi on the battle field.
 
Mbona maandamano yashafanikiwa ni sisi kuamua kesho tuhitimishe au tuwaache wale sungusungu waendelee kujianika juani then tuwa pige na butwaa next time
 
Kwanza kabisa hayotokaa yafanikiwe .Maana Gen Z hawana kiongozi .Maandamanao ya Shaghala bagala. Pili kesho watu hawatoki .Mark my words.
Nakubalina nawe, hakutakuja kuwa na manufaa yoyote zaidi sana ya kupotezewa muda, kuwekwa kwenye shinikizo, kupata hasara, misongo ya mawazo, uharibifu na mbaya zaidi maisha ya watu yanapotea!
 
Nakubalina nawe, hakutakuja kuwa na manufaa yoyote zaidi sana ya kupotezewa muda, kuwekwa kwenye shinikizo, kupata hasara, misongo ya mawazo, uharibifu na mbaya zaidi maisha ya watu yanapotea!
Eti mtu anatamka "tutoke wengi"Yeye yupo huko Calfornia saafi kabisa.Kwenda tu pale Washington alijificha kwenye gari. Hakushuka.Halafu manyumbu yanadanganyika na mtu kama huyo.Binafsi simkubali Samia ila kwa vile ana power,miaka 5 si mingi.
 
Maandamano yanayoendeshwa na wapumbavu fulani wako nje ya nchi
Waje hapa waingie rodini kama kufa na wao wafe ndio tujue wana machungu
Asilimia kubwa ya uchochezi inatoka kwa wabongo mafisi wanaoshi nje ya nchi, huku wakiwachochea watoto wa masikini wakafe
 
This is very true.Yale maandamano yalitosha kabisa ili kuwapa Serikali nafasi ya kushughulikia kero.Kesho watu hawataandamana na ni itakuwa ushindi kwa makabaila na mafisadi.Tatizo Maria ana mihemuko .
D9 haina tatizo, ujumbe umefika waandamane wasiandamane.
 
Refer Maandamano ya Kenya 2007.Kulikuwa na Raila Ondinga na wenzake na kulikuwa na sababu za msingi.
Acha uongo Odinga yupi aliandamana? Kule hakukua na maandamano ilikua ni kukatana mapanga kwa ukabila na zaidi ilikua kalenjin vs Kikuyu ndio maana Ruto na Kenyatta ndio walidakwa.

Unadhani hawa Gen Z wangebeba mapanga si mngewaita magaidi ila wakibeba wakenya 2007 mnaita ni maandamano na sio vurugu?

Unafiki tu umewajaa
 
msako mkali wa kupiga shoti waliokua wanahamaisha
 
Hii ni politics maandamano yakifanikiwa ni sababu ya kampeni ya No reforms no election ila yakifeli pia hawana hasara maana hawakuanzisha. So either way it's a win for them. Hii hasira ya wananchi vs CCM inaongeza tu support kwa chadema bila moja kwa moja CCM kuwashutumu kuanzisha maandamano otherwise msajili angekifuta.

Siasa ni akili hasa unapopambana na chama dola
 
CHADEMA kujizuia kushiriki uchaguzi ndiko kumefanya maandamano ya 29/10 yafanikiwe lengo lake la kuzuia uchaguzi. Kumbuka lengo lake lilikuwa ni kuzuia uchaguzi. Kuhusu kesho yasipofanikiwa..... lengo ni maandamano yasiyo na kikomo. Hata yasipofanyika kesho watu walivyokasirishwa na mauaji aliyofanya Samia basi SIKU YOYOTE chochote kinaweza kutokea. Majeshi na polisi hawataweza kukaa mitaani kila siku. Kuhusu ku-share madaraka: CHADEMA wameshaombwa sana (tangu machafuko ya uchaguzi) waingie kwenye serekali ya mseto na wakakataa katakata. Hata leo kulikuwa na juhudi za kuwaomba. Na mwisho: Hata kama kwa miujiza, Samia ata-survive mpaka 2030, basi CCM hawatathubutu kuvuga uchaguzi kama walivyofanya. Kwa kifupi Tanzania haitakuwa tena kama ilivyokuwa. Woga umeshaondoka kwa wananchi na hawatakubali tena uchaguzi wa kiini macho. Kwa kifupi huu ni mwanzo wa mwisho wa CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…