CHADEMA kujizuia kushiriki uchaguzi ndiko kumefanya maandamano ya 29/10 yafanikiwe lengo lake la kuzuia uchaguzi. Kumbuka lengo lake lilikuwa ni kuzuia uchaguzi. Kuhusu kesho yasipofanikiwa..... lengo ni maandamano yasiyo na kikomo. Hata yasipofanyika kesho watu walivyokasirishwa na mauaji aliyofanya Samia basi SIKU YOYOTE chochote kinaweza kutokea. Majeshi na polisi hawataweza kukaa mitaani kila siku. Kuhusu ku-share madaraka: CHADEMA wameshaombwa sana (tangu machafuko ya uchaguzi) waingie kwenye serekali ya mseto na wakakataa katakata. Hata leo kulikuwa na juhudi za kuwaomba. Na mwisho: Hata kama kwa miujiza, Samia ata-survive mpaka 2030, basi CCM hawatathubutu kuvuga uchaguzi kama walivyofanya. Kwa kifupi Tanzania haitakuwa tena kama ilivyokuwa. Woga umeshaondoka kwa wananchi na hawatakubali tena uchaguzi wa kiini macho. Kwa kifupi huu ni mwanzo wa mwisho wa CCM.