Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Kwanza kabisa naomba Mungu atujaalie tusifike hata mwaka mmoja kabla ya hili janga kutuondokea. Mungu mwenyewe ndie anaejuwa vya kuliondosha. Mungu ana njia nyingi!
 
Najua mkuu.
Hiyo ilikuwa wakati huo; subiri wakati husika.
Hata nawe Kalamu1 hujui mbinu za madikteta? Kama ni kujibu angemjibu Ndugai. Badala yake Ndugai kapita bila kupingwa. Msema tawire namba moja.
Keisi atapewa mkoa. Nkamia, Mwanri(Mungu amshukuru Magu), Kangi/Nabali(Magu zaidi ya Yesu) wote mikoa 2025. Sasa hivi wanaonekana wamepigwa chini. Anafanya political distancing. Gelesha tu. DAB atawaunganisha. Political logistics!
Kila mkoa na wake. Maandamano yasiyokoma wiki nzima. Badala ya mwenge, haya moto. Anaombwa na wananchi kuendelea. Political mobilization. Makanisa na misikiti ya mteule wa Mungu yatafunga na kuomba.
Hitimisho bungeni. Ndugai anatangaza. Wananchi wamlazimisha rais kuendelea. Ingawa kwa shingo upande amekubali. Kasikia kilio cha wananchi. Kaitika. Tanzania, Tanzania nakulove!
 

Sasa hivi hakuna uonevu? Watu wanapata haki zao kama inavyopaswa? Lete mrejesho kuhusu malipo ya wastaafu. Unajua lolote kuhusu uendeshaji wa ndege, faida na hasara zake? Sasa hivi wateule wote wamekuwa na viburi, na wanaweza kukufanya lolote na usiwe na popote pale pa kushtaki, huku wakijigamba kuwa serikali haichezewi. Chaguzi zote sasa hivi tunaona zikinajisiwa waziwazi.
 
Duh,
Mmemsema Kikwete muda wote.
Uongozi rais ni miaka 10 tu kwa mujibu wa katiba. Uongozi sio sifa na sidhani km Kuna kiongozi akataka aongoze maboya kama nyinyi.
Kuna siku hata Obama alilia pale Kenya akiuliza kwanini mi Rais wa US?
Kwasababu tu alitaka akale ugali kwa shangaziye akazuiwa.
 
Kwani nini kilitokea baada ya Hayati baba wa taifa na Benjamin ? Nation will press on peace full
 
Madeni mengi kukopa sana tutajua walivyoiba kupitia ikulu wasikaguliwe washirika wake watasaliti kambi ( kama Jafo Nkamia alivyosaliti JK) wasaidizi wengi mahakamani ....visasi wenyewe kwa wenyewe
 
Sioni hata cha ajabu kaongea, ni common sense.
Umechukua mkopo tukakupa ukaenda kusoma udaktari ili ukimaliza uhudumie wananchi we unaenda binafsi kwa ajili ya maslahi si ungeenda akusomeshe huyo mwekezaji.
Ni ukweli mchungu.
Nasema uwongo jamani?
 
SAWA.

Na itafurahisha sana kama hayo uliyoyaeleza yatakuwepo.

Lakini swali gumu ni hili: Yote hayo yatarudi na kusimamiwa na hawa hawa waliojitoa akili na kuimba nyimbo za mfalme sasa hivi?

Mbona huo utakuwa kama muujiza? Viongozi hawa hawa watoke katika kutekeleza kila wanachoagizwa, hadi akili ziwarudi na kuanza kufanya kazi kwa kutumia akili?
Au wote wataondoka na mfalme wao; na hao wapya je, wamejificha mahali wakisubiri wakati wao?

Mkuu, mi nadhani umeipaka bendera yetu rangi nzuri kuliko uhalisia wenyewe. Twende taratibu kidogo kidogo, pengine tutafika huko tunakokupenda sote hatua kwa hatua.
 


NI Katika Maraisi ambao watasahaulika "KABISA".
 
Kama anaweza kutangaza hadharani kuwa hakuna COVID Tanzania.
Hapo sasa!

Mtu ambaye bado anaamini kwa nguvu zake zote kwamba kuna binaadam mahali wanafanya njama kila siku kuwamaliza kabisa binaadam wenzao! Hana hata 'sophistication' na kutafuta njia ya kuwasilisha hayo anayoyaamini yeye kwa anaowalenga kwa njia inayoweza kuwaaminisha upuuzi wa namna hiyo!
 
Mkuu wewe utakuwa mtaalamu wa unajimu kbs, nimeipenda hii hakika Mungu atupe uhai tupate kuyashuhudia haya
 
Mbona unatuogopesha?
 
Huwajui ccm wewe
Wewe ndiye huwajui kabisa ccm! Zanzibar waligwaya Kamando alipotaka kubadilisha katiba aendelee. Jahazi likaokolewa na baba wa taifa.

2015 ccm unayozungumzia ilizikwa rasmi na Twende kupiga kura asiyetaka na abaki. Ccm ambayo haijasema kilichomtokea Mangula hadi leo! Wako pamoja wote hawako wote pamoja! Dhana ya chukua chako mapema ni sasa. Ccm ya watu sio watu wa ccm. Inatumiwa tu kwa maslahi. Hakuna mfia ccm tena.
 
Hata nawe Kalamu1 hujui mbinu za madikteta? Kama ni kujibu angemjibu Ndugai. Badala yake Ndugai kapita bila kupingwa. Msema tawire namba moja...
Mbona tupo pamoja mkuu, au hukuelewa nilichoandika hapo?

Nashukuru wewe umepata muda mzuri wa kufafanua mkakati mzima. Huyu hana mpango wa kutoka hapo alipo kwa hiari yake.
 
Atatengua mengi sana ya jiwe kama biden anavyofanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…