Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Nini kitatokea baada ya Magufuli kustaafu Urais?

Hahaaaa
Hata nawe Kalamu1 hujui mbinu za madikteta? Kama ni kujibu angemjibu Ndugai. Badala yake Ndugai kapita bila kupingwa. Msema tawire namba moja.
Keisi atapewa mkoa. Nkamia, Mwanri(Mungu amshukuru Magu), Kangi/Nabali(Magu zaidi ya Yesu) wote mikoa 2025. Sasa hivi wanaonekana wamepigwa chini. Anafanya political distancing. Gelesha tu. DAB atawaunganisha. Political logistics!
Kila mkoa na wake. Maandamano yasiyokoma wiki nzima. Badala ya mwenge, haya moto. Anaombwa na wananchi kuendelea. Political mobilization. Makanisa na misikiti ya mteule wa Mungu yatafunga na kuomba.
Hitimisho bungeni. Ndugai anatangaza. Wananchi wamlazimisha rais kuendelea. Ingawa kwa shingo upande amekubali. Kasikia kilio cha wananchi. Kaitika. Tanzania, Tanzania nakulove!
 
Aisee
Ana hulka zote za kidikteta na ulevi wa madaraka. Ikitokea akakubali kweli kuiheshimu Katiba, basi tutatakiwa kufanya sherehe kila mtu kwa nafasi yake.

Maana ndani ya huu utawala wake, kama sisi watumishi wa umma; cha moto tunakiona. Ila lolote linaweza kutokea. Ni rahisi sana kwake kuendelea kubakia madarakani kupitia Bunge lililojaa mamluki wake kubadili kifungu cha sheria cha ukomo wa Urais,

Lakini pia kupitia ushawishi wa baadhi ya wananchi wenye njaa kuwezeshwa posho kidogo na hivyo kuingia mitaani kufanya maigizo ya maandamano ya kumtaka aendelee kubakia madarakani. Halafu na yeye atajitokeza kwenye vyombo vya habari na ile sura yake ya uongo ya upole na unyenyekevu, huku akijifanya ameguswa sana na hivyo kuamua kusikiliza sauti za Wanyonge za kumtaka kuendelea na utawala wake wa kibabe!

Mungu atuepushie mbali hii dhahama. Miaka 10 ya kudhulumiwa, kuteswa, kuuwawa, kutengwa, kubaguliwa, kudharauliwa, kukejeliwa, kutukanwa hadharani, kunyanyaswa, kuonewa, na kila aina ya uovu; INATOSHA!!
 
Atagombana na mrithi wake kwa kuwa hana kifua cha kuvumilia vijembe vya Wapambe wa Rais ajae.

Cyprian Musiba wa Awamu ya 6 atakuwa anam provoke nae 'atajaaa'.

JK alitumia busara na subira ya hali ya juu sana kukwepa kuchonganishwa na Mrithi wake, sijui kama Yeye atakuwa na hicho kifua kama cha Jk
Nawe kwa kumfagilia Mkwere mwenzako hujambo,nadhani kwako hakuna moja baya kwa Jakaya.
 
Akiondoka Magu,magaidi watakuja nchini kwa kasi kubwa.
Business as usual itarejea.
Kina Faiza,Ritz,Bigshow watakuja tena jf kwa kasi kubwa
 
Mi ninachojua huyu jamaa harudi kamwe akimaliza muhula wake...
Umekijuaje na umekijulia wapi? Eleza tutakueleza nasi pia. Jiulize anapendwa kama Nyerere? Ana maadui wangapi nchini tena aliotengeneza mwenyewe?
 
Ana hulka zote za kidikteta na ulevi wa madaraka. Ikitokea akakubali kweli kuiheshimu Katiba, basi tutatakiwa kufanya sherehe kila mtu kwa nafasi yake.

Maana ndani ya huu utawala wake, kama sisi watumishi wa umma; cha moto tunakiona. Ila lolote linaweza kutokea. Ni rahisi sana kwake kuendelea kubakia madarakani kupitia Bunge lililojaa mamluki wake kubadili kifungu cha sheria cha ukomo wa Urais,

Lakini pia kupitia ushawishi wa baadhi ya wananchi wenye njaa kuwezeshwa posho kidogo na hivyo kuingia mitaani kufanya maigizo ya maandamano ya kumtaka aendelee kubakia madarakani. Halafu na yeye atajitokeza kwenye vyombo vya habari na ile sura yake ya uongo ya upole na unyenyekevu, huku akijifanya ameguswa sana na hivyo kuamua kusikiliza sauti za Wanyonge za kumtaka kuendelea na utawala wake wa kibabe!

Mungu atuepushie mbali hii dhahama. Miaka 10 ya kudhulumiwa, kuteswa, kuuwawa, kutengwa, kubaguliwa, kudharauliwa, kukejeliwa, kutukanwa hadharani, kunyanyaswa, kuonewa, na kila aina ya uovu; INATOSHA!!
Daaa Mkuu usilize watu.
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?

Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Wewe umesikia wapi kuwa atastaafu? Huyo atafia madarakani.
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?

Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
Uchumi utaimarika kwa kuwa watu watamiliki uchumi.

Kwanza nani kakuambia Rushwa/Ufisadi umepungua? Suala la Ufisadi au Rushwa kwa awamu hii inategemea umetokea mkoa gani na una itikadi ya chama gani!
 
Uchumi utaimarika kwa kuwa watu watamiliki uchumi.

Kwanza nani kakuambia Rushwa/Ufisadi umepungua? Suala la Ufisadi au Rushwa kwa awamu hii inategemea umetokea mkoa gani na una itikadi ya chama gani!
Hata Kama ipo imepungua mno
 
Hata Kama ipo imepungua mno
Wala haijapungua, ila unaweza kusema imepungua kwa sababu mfumo wa serikali hii ni tofauti na zamani.
Sasa hivi huoni au husomi tena zile habari za uchunguzi kuhusu Rushwa au Ufisadi, sasa hivi anayeweza kusema habari za Ufisadi ni Rais na kwa uchache sana Waziri Mkuu au Makamu wa Rais.

Hukuti habari za Rushwa kwenye vyombo vya habari, ila ukweli Rushwa ipo sana.
 
Enzi hizo tukisoma miaka ya sabini tulikaririshwa kwamba Nyerere akija kuacha urais nchi itakumbwa na vita ni hatari.

Fikra za kipumbavu kama hizi hufagiliwa na watu wenye akili finyu za waabudu sanamu kwamba mtu fulani kwao ndio Mungu.

Hata wachina zamani wakati wa utawala wa kidikteta wa Mao Zedong waliokaririshwa hivyo hivyo.

However, no one is indispensable anywhere. Magufuli will go and Tanzania will flourish.
 
1. Miradi mingi ambayo aliianzisha itasimama

2. Chattle kitabaki kijiji kama zaman tena enzi za nyerer kabisa

3. Uwanja wa chattle utakuwa eneo la kuchezea mpira na matamasha ya dini

4. Viongozi wengi wataonyesha uhslisia wa kipindi cha mzee magufuli..

Ntakuja baadae kidogo.. Naenda kwenye uzi wa kula tunda kimasihara
5.Raisi atarudi magogoni na serikali yote itarudi posta mpya kama zamani,na yale majengo ya mji wa serikali yatageuzwa historical sites
 
Habari wadau wa JF siasa.

Nimekuwa nikiwaza Sana sura ya nchi na hali ya nchi hii baada ya Rais Magufuli kumaliza mihula yake miwili. Je nchi itakuwaje kirushwa na kifisadi, kiuchumi, kisiasa, kimaendeleo nk?

Ajaye atakuwaje na atatupeleka wapi na jamii ya Kitanzania kipindi hicho kitakuwaje?
HALI ITAKUWA NGUMU SANA. MAANA INABIDI TUANZE KUJENGA UPYA UMOJA, UPENDANO NA MSHIKAMANO WA KITAIFA. NA WATU WENGI WATAKUWA WAMEACHIWA MAJERAHA MENGI SANA AMBAYO KUYAPONYA NI KAZI KUBWA.
 
Back
Top Bottom