Umsumbalembe
JF-Expert Member
- Dec 29, 2013
- 944
- 871
CarmalengoKatika kipindi hiki cha mpito nani anakua anasimamia shughuli zote za Vatican?
CarmalengoKatika kipindi hiki cha mpito nani anakua anasimamia shughuli zote za Vatican?
Mimi nikajua ungeanza kuwaombea vifo huku ukitamani nao wafe mapema ili wasije wakafika umri mkubwa wa miaka 88 kama Pope.Hata baadaye kufa sio hasara , hasara ni kwa walionizaa mimi naenda kupumzika milele ni safi tu.
Kufa ni uoga ila ni jambo zuri sana kwa mtu binafsi.Mimi nikajua ungeanza kuwaombea vifo huku ukitamani nao wafe mapema ili wasije wakafika umri mkubwa wa miaka 88 kama Pope.
Maana wangekuwa (kwa mujibu wako) wameishi sana.
Umelewa mkuu, Rudi nyumbani kalale.Utatokea mwisho wa Dunia ijumaa wiki hii nakushauri kama una viakiba vyako sijui vimali hakikisha alhamis haifiki uwe uneshamaliza Kila kitu ijumaa tutakuwa wote tumekufa Dunia nzima.
Kweli aje papa mweusi...Sasa hivi ni zamu yetu TEC kutoa papa, Papa ajae lazima awe mweusi!
Tunataka reforms kwenye mfumo wa upatikanaji wa Pontiff!
No reforms, no Pope!
HaaMalasusa anasemaje?
1..Vipi makadinali wako wangapi jumla?UT ANIMA P. FRANCISCI TUUS REQUIESCAT"
"MAY YOUR SOUL REST IN PEACE POPE Francis'
"Kaka na dada wapendwa ni kwa huzuni kubwa kwamba sina budi kutangaza kifo cha Baba yetu Mtakatifu Francisko. Saa 01.35 asubuhi ya leo, (Jumatatu 21 Aprili 2025),Askofu wa Roma, Francisko, alirejea nyumbani kwa Baba. Imesikika sauti ya huzuni kutoka kwa Kardinal Farrell"
Mwandishi Revocatus J Ng'oja
Katika historia ya ulimwengu, vifo vya viongozi wakuu wa dini vimekuwa tukio la mshtuko na majonzi makubwa kwa waumini wao.
Lakini linapokuja suala la kifo cha Papa wa Kanisa Katoliki, tukio hilo linakuwa zaidi ya majonzi.
Ni mchakato mzima wa kihistoria unaofuata taratibu za karne nyingi zilizopita.
Sasa hebu tafakari hili, Papa Francis amefariki Leo baada ya kulazwa muda mrefu Toka mwanzoni mwa mwezi Feb. Alikuwa anapumulia mashine, hali yake ilikuwa mbaya sana na dunia nzima ilikua inafuatilia kwa ukaribu huku waumini wa Katoliki zaidi ya bilioni 1.5 wakimwombea.
Lakini baada ya kufariki Leo akiwa na miaka 88, unajua kitafanyika?
Baada Papa kufariki mchakato maalumu unaanza ,Tena ni mchakato wa kihistoria ambao umefuatwa kwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita.
Mara tu baada ya kifo Vatican imeingia katika kipindi kinachoitwa Interregnum,ni kipindi ambacho Kanisa Katoliki linakuwa bila kiongozi mkuu.
Mchakato huo unaanza na uongozi wa Vatican kupitia ofisi maalum inayojulikana kama Camerlengo.
Camerlengo inafanya nini?
- 1- Kuthibitisha kifo cha Papa.
Kiongozi wa Vatican humuita Papa mara tatu kwa jina lake rasmi. Ikiwa hataitika, basi kifo chake kinathibitishwa rasmi na ndicho kimefanyika kabala hawajatangaza kifo chake na baadaye ndipo wakatangaza.
Hata hivyo zamani,taratibu zilihusisha nyundo ndogo ya shaba kupigwa kidogo kwenye paji la uso la marehemu, lakini desturi hii ilisitishwa mwaka 1963.
- 2-Kutangaza Kifo Hicho Kwa Dunia,
Habari za kifo cha Papa hutangazwa rasmi kwa kutumia chombo cha mawasiliano cha Vatican. Ndivyo ilivyofanyika.
Makanisa yote hutangaziwa na kengele maalum hugongwa kama ishara ya maombolezo.
3-Kufunga Ofisi ya Papa,
Vitu vyote vya ofisi ya Papa hufungwa rasmi. Pete ya Papa na muhuri wa Fisherman's huharibiwa, kuashiria mwisho wa utawala wake.
- 4-Kuandaa Mazishi,
Mazishi ya Papa lazima yafanyike kati ya siku nne hadi sita baada ya kifo chake. Kisha, kanisa huingia katika siku tisa za maombolezo rasmi.
Baada ya kifo chake, Papa huzikwa katika makaburi ya St. Peter’s Basilica, isipokuwa kama aliacha wosia wa kuzikwa sehemu nyingine.
Baada ya maombolezo na mazishi, Kanisa linaingia katika hatua muhimu zaidi, kumchagua kiongozi mpya wa Kanisa Katoliki.
Mchakato huu unaitwa CONCLAVE.
- 5-Conclave Inavyofanyika,
Ndani ya siku 15 hadi 20 baada ya kifo cha Papa, Makardinali wenye umri chini ya miaka 80 hukusanyika Vatican.
Makadinali Hawa wanajifungia ndani ya Kanisa la Sistine,na hakutakuwepo na simu, waandishi wa habari, hata mawasiliano na dunia ya nje hayatakuwepo.
Makadinaki Hawa watapiga kura kwa siri, wakirudia mara kadhaa hadi mmoja wao atakapopata 2/3 ya kura.
Baada ya kura, kinachofuatia ni cha kusisimua zaidi, Kila baada ya mzunguko wa kura, makaratasi yanayotumiwa katika uchaguzi huchomwa moto.
Moshi mweusi ukitoka, inamaanisha hakuna maamuzi bado. (Makaratasi ya kura huchomwa pamoja na kemikali maalum zinazozalisha moshi mweusi.
Kemikali zinazotumika mara nyingi kitaalamu huitwa Sulphur na Resin, ambazo huleta moshi mzito na mweusi unaoonekana kwa mbali).
Moshi mweupe ukitoka, inamaanisha Papa mpya amechaguliwa! (Makaratasi ya kura huchomwa pamoja na kemikali zinazozalisha moshi mweupe.
Kwa kawaida, kemikali hizi ni potassium chlorate, lactose, na pine resin, ambazo husaidia kuchoma karatasi kikamilifu bila kutoa moshi mweusi).
Mara baada ya Papa mpya kuchaguliwa, anatangazwa kwa dunia kwa maneno haya maarufu.
" HABEMUS PAPAM "( Tuna Papa mpya!)
Hapo ndipo ulimwengu mzima husherehekea na safari mpya ya Kanisa Katoliki huanza upya.
Licha ya kifo cha Papa kuwa pigo kubwa kwa waumini wake, mfumo wa Kanisa Katoliki umejengwa kwa namna ya kipekee inayohakikisha kuendelea kwa uongozi bila mgogoro.
Na hiki ndicho kinachokifanya Kanisa Katoliki kuwa moja ya taasisi imara zaidi duniani.
Kwa hivyo BAADA YA kiti Cha Papa Francis kutagzwa rasmi na Vatican Leo , dunia haitasimama. Kanisa litaomboleza, lakini taratibu zake zitahakikisha mrithi wake anapatikana na Kanisa linaendelea kusimama.
Huo ndio uzuri wa historia, taratibu na imani vyote vikifanya kazi kwa usawa.
LIDUMU KANISA TAKATIFU KATOLIKI LA MITUME.
" SANCTAM APOSTOLICAM CATHOLICAM VIVAT"
RAHA YA MILELE UMPE EE BWANA NA MWANGA WAMILELE UMWANGAZIE PAPA FRANCIS APUMZIKE KWA AMANI.
REQUIES AETERNA DA SIBI DOMINE, AC PERPETUA LUMINIS PAPAE FRANCISCI REQUIESCAT.
Ala pole sanaMiye ntaenda na binti yangu
Hapa juzi nilipata changamoto ya kuvunja ndoa na mke wangu
Nilipata stress kidogo nijiue
Ila huyu binti alifunga kwa Resima kwa ajili yangu na akasali Novena
Ilinisaidia sana
Kidogo akasomee Usista na kuna Padri alishajitolea kumsomesha Usista na Unesi(she dreams of being a nurse one day)
Ila kwa kuwa nampenda na ninataka aniletee wajukuu nimemwambia aaihirishe
Unesi unamtosha
Ameniokoa na Suicide acha nimtimizie ndoto yake ya kwenda Hija Takatifu
1..Vipi makadinali wako wangapi jumla?
2. Makadinali wenye kupiga kura ni wale walio madarakani au hata wastaafu?
3. Je awamu hii Kadinali atatoka Afrika au
Kila nchi Ina kadinali , awamu hii inawezekana Africa pia ikapata mtu atakae ingia kwenye kinyang'anyiro hicho Cha uchaguzi wa papa.1..Vipi makadinali wako wangapi jumla?
2. Makadinali wenye kupiga kura ni wale walio madarakani au hata wastaafu?
3. Je awamu hii Kadinali atatoka Afrika au Asia?
Hizo ni Imani zao mkuuKama zamani waligonga na nyundo paji la uso
Leo,sauti inayotumika kumwita ni sauti ya namna Gani(kubwasana) kama yakwenye gwaride la jeshi au sauti ipi
Na
kwann daktari hatumiki
Huyo wa Tanzania wa sasa anaonekana yuko Smart sanaKila nchi Ina kadinali , awamu hii inawezekana Africa pia ikapata mtu atakae ingia kwenye kinyang'anyiro hicho Cha uchaguzi wa papa.
Je katika jopo la Makardinali this time kuna wakutoka Africa sita je kuna nafasi kupata papa wa kutoka Africa this time? Wengi ingini Novena tuombe tumpate wakutoka bara la Africa.ULiza lolote kuhusu taratibu za mazishi ya papa ni kuelezea.
NINI HUTOKEA PAPA ANAPOFARIKI?
Pale Papa anapofariki dunia, mchakato maalum unaoitwa “sede vacante” (kiti tupu) huanza rasmi. Haya ndiyo yanayofanyika:
1. Uthibitisho rasmi wa kifo – Camerlengo (Kardinali Mkuu wa Masuala ya Ndani ya Vatican) hutangaza rasmi kifo cha Papa kwa kuita jina lake la ubatizo mara tatu na kugonga paji lake la uso kwa nyundo ya fedha.
2. Camerlengo hutangaza kifo cha Papa kwa dunia na huvunja Pete ya Mvuvi (Ring of the Fisherman) pamoja na muhuri wake wa risasi ili kuzuia ughushi wa nyaraka.
3. Mwili wa Papa huandaliwa kwa ajili ya kuagwa na umma, na huwekwa kwa heshima katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa siku kadhaa.
4. Kipindi cha maombolezo cha siku tisa, kinachoitwa "novendiales," huanza ambapo misa za mazishi hufanyika kila siku.
5. Papa huzikwa, kwa kawaida katika pango lililo chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
6. Baraza la Makardinali hukutana katika kikao cha siri kilichofungwa (conclave) kuchagua Papa mpya. Makardinali walio na umri wa chini ya miaka 80 huingia ndani ya Kanisa la Sistine na kujitenga kabisa na ulimwengu wa nje.
7. Makardinali hupiga kura mara nne kwa siku hadi mmoja apate kura za theluthi mbili. Baada ya kila duru ya kura isiyofanikiwa, karatasi za kura huchomwa kwa kemikali zinazotoa moshi mweusi. Papa anapochaguliwa, moshi mweupe huashiria kuwa uamuzi umefanyika.
8. Papa mpya huchagua jina lake la kipapa, na kardinali mwandamizi hutangaza kwa dunia: "Habemus Papam" (Tunaye Papa) kutoka kwenye roshani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.
9. Papa mpya hujitokeza kwenye roshani na kutoa baraka yake ya kwanza, inayoitwa “Urbi et Orbi” (kwa jiji na kwa dunia).
Mchakato mzima unachanganya mila za kale na mahitaji ya kisasa ili kuhakikisha kuwa uongozi wa kipapa unapitishwa kwa utaratibu mzuri.
UCHAGUZI WA PAPA
Uchaguzi wa Papa mpya hufanyika kati ya siku 15 hadi 20 baada ya kifo cha Papa aliyepita. Huu hapa ni muhtasari wa mchakato huo:
Baraza la Makardinali lazima lianze conclave (mchakato wa uchaguzi wa Papa) si mapema kuliko siku 15, na si baadaye ya siku 20 baada ya kifo cha Papa. Kusubiri huko hufanyika kwa sababu zifuatazo:
1. Kuwapa makardinali kutoka kote duniani muda wa kufika Roma.
2. Kutoa muda wa kufanya mazishi na ibada za heshima kwa Papa aliyefariki.
3. Kuwapa makardinali muda wa maombi na tafakari kabla ya kufanya uamuzi.