Nini kitatokea baada ya Papa Fransisko kufariki dunia leo 21 April, 2025?

Hata baadaye kufa sio hasara , hasara ni kwa walionizaa mimi naenda kupumzika milele ni safi tu.
Mimi nikajua ungeanza kuwaombea vifo huku ukitamani nao wafe mapema ili wasije wakafika umri mkubwa wa miaka 88 kama Pope.

Maana wangekuwa (kwa mujibu wako) wameishi sana.
 
Mimi nikajua ungeanza kuwaombea vifo huku ukitamani nao wafe mapema ili wasije wakafika umri mkubwa wa miaka 88 kama Pope.

Maana wangekuwa (kwa mujibu wako) wameishi sana.
Kufa ni uoga ila ni jambo zuri sana kwa mtu binafsi.
 
Kama zamani waligonga na nyundo paji la uso

Leo,sauti inayotumika kumwita ni sauti ya namna Gani(kubwasana) kama yakwenye gwaride la jeshi au sauti ipi

Na
kwann daktari hatumiki
 
1..Vipi makadinali wako wangapi jumla?

2. Makadinali wenye kupiga kura ni wale walio madarakani au hata wastaafu?

3. Je awamu hii Kadinali atatoka Afrika au Asia?
 
Ala pole sana
 
1..Vipi makadinali wako wangapi jumla?

2. Makadinali wenye kupiga kura ni wale walio madarakani au hata wastaafu?

3. Je awamu hii Kadinali atatoka Afrika au

1..Vipi makadinali wako wangapi jumla?

2. Makadinali wenye kupiga kura ni wale walio madarakani au hata wastaafu?

3. Je awamu hii Kadinali atatoka Afrika au Asia?
Kila nchi Ina kadinali , awamu hii inawezekana Africa pia ikapata mtu atakae ingia kwenye kinyang'anyiro hicho Cha uchaguzi wa papa.
 
Kama zamani waligonga na nyundo paji la uso

Leo,sauti inayotumika kumwita ni sauti ya namna Gani(kubwasana) kama yakwenye gwaride la jeshi au sauti ipi

Na
kwann daktari hatumiki
Hizo ni Imani zao mkuu
 
ULiza lolote kuhusu taratibu za mazishi ya papa ni kuelezea.

NINI HUTOKEA PAPA ANAPOFARIKI?

Pale Papa anapofariki dunia, mchakato maalum unaoitwa “sede vacante” (kiti tupu) huanza rasmi. Haya ndiyo yanayofanyika:

1. Uthibitisho rasmi wa kifo – Camerlengo (Kardinali Mkuu wa Masuala ya Ndani ya Vatican) hutangaza rasmi kifo cha Papa kwa kuita jina lake la ubatizo mara tatu na kugonga paji lake la uso kwa nyundo ya fedha.

2. Camerlengo hutangaza kifo cha Papa kwa dunia na huvunja Pete ya Mvuvi (Ring of the Fisherman) pamoja na muhuri wake wa risasi ili kuzuia ughushi wa nyaraka.

3. Mwili wa Papa huandaliwa kwa ajili ya kuagwa na umma, na huwekwa kwa heshima katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro kwa siku kadhaa.

4. Kipindi cha maombolezo cha siku tisa, kinachoitwa "novendiales," huanza ambapo misa za mazishi hufanyika kila siku.

5. Papa huzikwa, kwa kawaida katika pango lililo chini ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

6. Baraza la Makardinali hukutana katika kikao cha siri kilichofungwa (conclave) kuchagua Papa mpya. Makardinali walio na umri wa chini ya miaka 80 huingia ndani ya Kanisa la Sistine na kujitenga kabisa na ulimwengu wa nje.
7. Makardinali hupiga kura mara nne kwa siku hadi mmoja apate kura za theluthi mbili. Baada ya kila duru ya kura isiyofanikiwa, karatasi za kura huchomwa kwa kemikali zinazotoa moshi mweusi. Papa anapochaguliwa, moshi mweupe huashiria kuwa uamuzi umefanyika.

8. Papa mpya huchagua jina lake la kipapa, na kardinali mwandamizi hutangaza kwa dunia: "Habemus Papam" (Tunaye Papa) kutoka kwenye roshani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

9. Papa mpya hujitokeza kwenye roshani na kutoa baraka yake ya kwanza, inayoitwa “Urbi et Orbi” (kwa jiji na kwa dunia).

Mchakato mzima unachanganya mila za kale na mahitaji ya kisasa ili kuhakikisha kuwa uongozi wa kipapa unapitishwa kwa utaratibu mzuri.

UCHAGUZI WA PAPA

Uchaguzi wa Papa mpya hufanyika kati ya siku 15 hadi 20 baada ya kifo cha Papa aliyepita. Huu hapa ni muhtasari wa mchakato huo:

Baraza la Makardinali lazima lianze conclave (mchakato wa uchaguzi wa Papa) si mapema kuliko siku 15, na si baadaye ya siku 20 baada ya kifo cha Papa. Kusubiri huko hufanyika kwa sababu zifuatazo:

1. Kuwapa makardinali kutoka kote duniani muda wa kufika Roma.
2. Kutoa muda wa kufanya mazishi na ibada za heshima kwa Papa aliyefariki.
3. Kuwapa makardinali muda wa maombi na tafakari kabla ya kufanya uamuzi.
 
Je katika jopo la Makardinali this time kuna wakutoka Africa sita je kuna nafasi kupata papa wa kutoka Africa this time? Wengi ingini Novena tuombe tumpate wakutoka bara la Africa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…