Nini kitatokea iwapo uko mbele ya hakimu aliyekushuhudia ukivunja sheria, ila ushahidi aliyoletewa kwa ajili ya kukuhukumu unaonesha hauna hatia?

Nini kitatokea iwapo uko mbele ya hakimu aliyekushuhudia ukivunja sheria, ila ushahidi aliyoletewa kwa ajili ya kukuhukumu unaonesha hauna hatia?

George Charles007

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2024
Posts
217
Reaction score
337
Mfano hakimu kakushuhudia ukiiba, alafu hakimu huyo huyo ndiye anayekuhukumu akapelekewa ushahidi unaosema huku husika na tukio hilo.

Nini kitatokea wana JF?
 
Mfano hakimu kakushuhudia ukiiba, alafu hakimu huyo huyo ndiye anayekuhukumu akapelekewa ushahidi unaosema huku husika na tukio hilo. Nini kitatokea wana JF?
Hawezi kuhusu kwa hisia zake hata kama aliona. Atahukumu kwa ushahidi usioshaka.
 
Badala ya kuwa Hakimu Kuhukumu atakuwa Shahidi ili kutoa Ushahidi hivyo atakayekuwa Hakimu ni mwingine....
 
Hawezi kuhusu kwa hisia zake hata kama aliona. Atahukumu kwa ushahidi usioshaka.
Hiyo imekaaje? Ni sawa?

Mfano umeshuhudia jitu limebaka mtoto hadi limeua alafu unaletewa ushahidi wa kulihukumu unaosema hana hatia. Utafuata ushahidi au macho yako? Hiyo ni kwa wewe ndo tutolee mfano?
 
Badala ya kuwa Hakimu Kuhukumu atakuwa Shahidi ili kutoa Ushahidi hivyo atakayekuwa Hakimu ni mwingine....
Bobu ndo kesi hiyo kashapangiwa aruke nayo na kashuhudia msala.

Labda aipige pige kalenda.
 
Bobu ndo kesi hiyo kashapangiwa aruke nayo na kashuhudia msala.
Unapangiwa Kesi kabla tukio halijatokea ? Niambie how is that Possible ?
Labda aipige pige kalenda.
Nope rahisi sana anajitoa tu kwa sababu zilizopo kwamba alishuhudia.., ni kama vile tu kuhumu mtu aliyemuua ndugu yake (itaonyesha Bias)
Justice must not only be done, but it must also be seen to be done.”
 
“What I believe and what I can prove are two different things”
 
Back
Top Bottom