Nini maana ya Allah? Je, huyo Allah ni nani?

Rough player

Member
Joined
May 26, 2018
Posts
39
Reaction score
120
Natumai wote ni wazima humu jamvini

Baada ya kusoma baadhi nyuzi zinazojumuisha masuala ya kiimani nimeona baadhi ya maneno yakikebehi hili jina/neno (ALLAH)
Kwa hiyo baada ya kuona hili ni tatizo nimeonelea bora nitoe ufafanuzi kidogo ambao unaweza kutupa faida sote

Kwanza kabisa kwenye upande wa fasihi na lugha ALLAH haimaanishi mungu kama kwa kiingereza tunavyosema GOD na kiarabu ILAH,, je kwanini ALLAH maana yake sio mungu na waislamu wanasema mungu? Maswali kama hayo watu tunajiuliza vichwani mwetu

Majibu ya maswali yetu ni haya tunavyosema MUNGU ni inategemea na imani ya mtu,, mwengine atasema sanamu ndiyo mungu wake,, wengine mizimu na wengine mwezi na wengine jua,, ila unavyosema ALLAH unazungumzia mungu mmoja anayepaswa kuabudiwa na kuombwa hakika yeye ndiye mkuu na muweza wa yote.

Wengine watauliza kwanini wakristo hawasemi kama ALLAH ndiye mungu wao ??
Hii ni kwasababu ya lugha husika katika lugha ya kiingereza hakuna tafsiri au neno linalo simama kwa (mungu mmoja anayepaswa kuabudiwa muweza wa yote) ila kunatafsiri ya MUNGU wa kawaida ambaye kila mtu anaweza mfanya kwa mtazamo wake

Na kuhakikisha hilo ukija kuchukua biblia ya st james iliyo katika lugha ya kiarabu utakuta neno hilo ALLAH lipo katika biblia

Dhumuni la huu uzi lilikua ni kutoa ufafanuzi wa hili neno kwa kifupi kama kuna sehemu nimekosea wajuzi zaidi mtarekebisha maana tupo humu kujifunza

Nawasilisha
 
Mkuu asante kwa ufahamu.
Ila tambua kuwa wewe unayemwita Mungu wengine wanamuita "laws of physics" kwa hiyo jina ni kama recognition tu.. ila source itabakia kuwa vilevile.
Katika haya mambo huwa nashangaa kitu kimoja "Tunabishana na kushindwa kuelewana kwa jambo moja ila tunachokimanisha ni kilekile"
Je, ulishaskia kitu kinaitwa DOG WISDOM?
Ni kwamba hata uvae vipi mbwa wako hawezi kukusahau.
Binadamu tunafeli kujua source,creator,energy etc ni kile kile kwenye mavazi tofauti.
Amani iwe juu yako.
 
Mleta uzi umefafanua vizuri kimuonekano. Ila mi naomba niwe mpole kwa kuwa nina uelewa mdogo juu ya upande ulio uzungumzia kwa kina ktk uzi wako.
 
Mleta uzi umefafanua vizuri kimuonekano. Ila mi naomba niwe mpole kwa kuwa nina uelewa mdogo juu ya upande ulio uzungumzia kwa kina ktk uzi wako.
Thanks mkuu ila unaweza ukazungumzia kwa upande mwingine ambao unauelewa nao ili tupate maarifa zaidi mkuu itakua bora zaidi
 
Thanks mkuu ila unaweza ukazungumzia kwa upande mwingine ambao unauelewa nao mkuu itakua bora zaidi
Mi nijuavyo ni kwamba jamii fulani ktk eneo fulani hutumia jina fulani ila jina hilo humaanisha Mungu. Ndio maana kabla ya kuja kwa kristo (kwa wenye iman ya ki_kristo) tunaamin watu walikuwa wanatoa sadaka za kuteketezwa ili kufanya ibada na toba n.k, mfumo ambao hata watu toka nje ya bara la africa waliukuta huku africa kipindi walipo kuja.

Majina aitwayo Mungu ktk makabila mbalimbali yanaashiria kuwa ni Mungu muweza wa yote muumba wa vyote (ki_imani).
 
Asante mkuu umeeleza kwa jinsi unavyofahamu barikiwa kwa hilo
 
Talizo Allah lilitumika na wapagani wa macca kabla ya uislam wakimwita ndio mungu wao.

Baada ya Muislam wa kwanza Muhammad kuuanzisha uisam nae akaendelea kulitumia jina lilelile lililotumika na wapagani kumuita mungu wao!
 
Kwa lugha ya kiarabu mungu ndiyo huitwa ILAH ila sio Allah mbona mtoa mada ameelezea vizuri
Kuhusu chanzo kuna maelezo mengi yanapingana . Wengine wanasema ALLAH chanzo ni "al ilah" "the god".
Wananzuoni wanatofautiana mkuu. Ambaye ni moja ya miungu ya waarabu hapo Maka kabla ya uislam. Mkuu angetoa chanzo ili tuivishwe vizuri ndio maana ya intelligentsia. Ingekuwa dini tungemeza Bila kuhoji. Ila humu lzm utikiswe kidogo Ila kwa Nia chanya na ya kujenga sio kupondana . Ingawa maelezo aliyoyatoa ni msimamo wa kiimani kuhusu hilo jina.
 
Wataniuliza unaitwa nani, niwajibuje? - Musa

Waambie MIMI NIPO AMBAYE NIPO. - Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo.
 
Kwa mujibu wa jamaa mmoja niliwahi kumsikiliza akitoa ushuhuda yeye alikuwa ni Naibu Katibu wa Wachawi Duniani, by the time anafanya hiyo kazi yake alikuwa ni Sheikh akasema, Allah ni jina la 66 la Shetani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…