offset Frankie
Member
- Dec 24, 2023
- 29
- 38
kuna mtu amekuelezea vizur hapo.Mimi ni Mkristo. Niaminivyo, chanzo cha ndoto inaweza ikawa:
1. Ujumbe kutoka kwa Mungu
2. Kazi ya Shetani kwa lengo la kuharibu
3. Uchovu wa mwili na aina ya mawazo uliyokuwa ukiyawaza kabla ya kulala.
Hivi karibuni, nimeota ndoto ambayo mpaka sasa bado sijapata tafsiri yake.
Niliota natembea njiani na vijana wawili, na ghafla , nikaona noti ya sh 1,000/= mbele yangu.
Nilipoiona, nilijisemea kuwa kama nimetegeshewa kichawi, basi itakuwa "imekula" kwao walioitegesha kwa sababu nitaichukua na kuitakasa kwa Jina la Yesu na kuitumia bila madhara yoyote. Niliamua kuchukua, na mara tu baada ya kuiokota, niliziona zingine nyingi, noti za shilingi 1,000/= na za 2,000/=. Niliendelea kuziokota, na nikawaambia vijana wawili niliokuwa nao kuwa na wao waokote.
Baada ya kuiokota kiasi kikubwa, ziliisha na hatimaye tukaendelea na safari kila mmoja akiwa na noti zake. Muda wote nilikuwa makini kuzishikilia huku nikiendelea kuziombea ili kama zilikuwa na nguvu za giza zisiweze kuwa na athari kwangu.
Baada ya kutembea kidogo, tuliwakuta askari watatu wa usalama barabarani wakiwa wamesimama pembezoni mwa barabara. Mmoja wao, akiwa katika sare za kazi, alinifuata na kuniambia hela tuliyoiokota ni ya kwake hivyo nimrudishie.
Kwanza, nilitaka kukataa kumpa. Lakini aliponiambia kuwa walituona tokea tulipokuwa tunaokota hizo fedha, nilipatwa na mshutuko, nikagundua kuwa huyo trafiki si binadamu wa kawaida. Aliwezaje kutuona wakati tulikookotea ni mbali?
Pale pale nilianza kumkemea kwa Jina la Yesu, na ghafla yule trafiki akaanza kubadilika kuanzia sura, umbo mpaka na mavazi.
Mavazi yake ya utrafiki (meupe) yalipoteza uweupe na kufanania kwa mbali sare za wafungwa. Na umbile la huyo askari lilibadilika kutoka wa kiume na kuwa wa kike.
Nilipoendelea kumkemea, alidondoka chini na kuwa kama anayegugumia kwa maumivu.
Vijana wawili niliokuwa nao waliondoka kwa muda na kuniacha peke yangu nikiandelea kupambana na hicho kiumbe. Ni kama vile niliwaagiza kufuata kitu.
Wakati nikiendelea kumkemea, nilimhoji sababu ya kunitegeshea pesa, akasema walinipenda. Nilipomwuliza kama hiyo hela ingewaathiri na hao vijana wawili waliookota, alisema ingewaathiri kama wangekubaliana nao.
Baada ya kusema hivyo, nilikazana kuomba kwa bidii, lengo sasa likiwa hicho kiumbe kipotee kwa kuyeyuka.
Hiyo ndoto inamaanisha nini?
Nini chanzo chake?
Asanteni.
tafasiri ya ndoto yeyote inatoka kwa Roho wa Mungu ( ikiwa ni ndoto ya kiMungu)
rejea mifano mingi kwny biblia ya watu wengi walio ota ndoto tafasiri nzur ya ndoto wote walirejea kwa Mungu.
mfano. Daniel anamwambia nebukadnezza. tupe mda tutakukumbusha ndoto na tafasiri yake daniel anarejea kwa Mungu kumuuliza na badae anapata majibu yalio sawa na maana halisi ya ndoto.
nini chakufanya sasa unapoota ndoto?. either ni nzur au mbaya?.
Omba Omba Omba piga magoti mbele za Mungu utapata tafasiri na hatua zakuchukua.
namna ya kuomba.
approach ndoto vile ilivyo (kwa maana ndoto ni ishara ya jambo kutokea katika ulimwengu wa roho). kumbuka jambo lolote kabla halijaanza kwny ulimwengu wa mwili linaanza kwenye ulimwengu wa roho kupitia ndoto na maono.
kwahio vile ulivyoota step moja baada ya nyingine kwny kukataa jambo likatae ambalo halina baraka kwako kwny kulikubali mshukuru Mungu na kulikubali ulinene linakuja katika ulimwengu wa mwili
Kumbuka laana na baraka zito kwny ulimi wako