Nini Maana ya Kila Silaha Itakayofanyika Juu Yako Haitafanikiwa

john achila mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
142
Reaction score
281
Nini Maana ya Kila Silaha Itakayofanyika Juu Yako Haitafanikiwa

Neno la Mungu

Katika Isaya 54:17, Neno la Mungu linasema, “kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa, na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana”.

Tuzingatie kuwa hapo Neno linasema “kila silaha itakayofanyika haitafanikiwa” na SIYO “kila shambulizi halitafanikiwa”. Maana yake ni kuwa wakati tu wa maandalizi ya silaha, mwanzo huo ndio hautafanikiwa.

Maana yake ni nini?
Silaha za zamani zilikuwa ni mikuki, panga na mishale, na nyinginezo. Nyingi ya hizo zilikuwa zinatengenzwa kwa vyuma na wahunzi. Hivyo, wahunzi walikuwa wanayeyusha chuma, kisha wanakitengeneza kwa umbile la silaha waitakayo, kama ni panga, au kisu au mkuki.
Biblia inasema, silaha yo yote inayotaka kutengenezwa na hawa wahunzi, haitafanikiwa.

Hii maana yake ni kuwa, wahunzi wakiwa katika zile hatua za kuyeyusha chuma, basi hawafanikiwa kufikia hitimisho la kuikamilisha ile silaha. Shughuli yao itaishia katikati na hakuna silaha yoyote itakayotengenezwa. Aidha, wakiwa katika utengenezaji wataungua moto, au watapungukiwa na malighafi, au watapata hitilafu nyingine yoyote ambayo itawafanya wasimalize ile kazi. Watabaki na chuma kisicho na umbile lolote la kisu, au sime, au panga au mkuki.

Isaya 54:16-17 inasema: “Tazama, nimemwumba mhunzi avukutaye moto wa makaa, akatoa silaha kwa kazi yake; nami nimemwumba mharibu ili aharibu. Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa”.

VILE VILE, NA AGANO MUNGU ANALOINGIA NA WATUMISHI WAKE NI AGANO LA NAMNA HIYO HIYO.

Maana yake ni kwamba hawataona hata dalili ya silaha juu ya maisha yao, kwani Bwana ataziharibu silaha kabla hazijakamilika. Kama ni uchawi ndio silaha ya adui, basi wakati tu uchawi unapikwa huko kwenye vibuyu na miti, na makaburini na baharini au katika madhabahu za baali, basi uchawi huo utaungua moto kabla haujakamilika, na wala hutajua kama kuna mashambulizi yalikuwa yameandaliwa dhidi yako. Hutaona hata hiyo dalili. Mambo yanaharibika kabla hayajakamilika. Baadaye sana, ndiyo unaweza kusikia (kama Bwana ataruhusu ujue), ushuhuda kwamba kuna njama zilipangwa juu yako na zikashindikana.

Kama magonjwa ndiyo silaha ya adui anayoisuka juu yako, akiwa katika kiwanda chake cha kukutengenezea hayo, Bwana atasimama kinyume chake na kuziharibu hizo hila, na hutaona chochote na wala kujua chochote kwani hata dalili haitaonekana.

Kama ni kuondolewa kazini ndiyo silaha ya adui, basi kabla hata hiyo mipango haijakamilika, itafutwa na kuharibiwa na Bwana. (Unaweza kujua baadaye, kama Bwana ataruhusu ujue).

Na hapo ndipo kuna umuhimu wa kumshukuru Mungu kila wakati, kwani kuna vitu vingi sana Bwana anatuepusha navyo pasipo kujua au hata kuona dalili yake.

Kama ni visa ndiyo silaha ya adui ili upoteze haki yako, au hiki na kile Bwana alichokupa, basi kabla hivyo visa havijakamilika, Bwana ataviharibu.

HIYO NDIYO MAANA YA “KILA SILAHA ITAKAYOFANYIKA JUU YAKO HAITAFANIKIWA”.

Hata hivyo, tuelewe kuwa hali hiyo hutokea kama wewe ni mtumishi wa Mungu. yaani, unampendeza Mungu na kuyafanya mapenzi yake.
Isaya 54:17 “silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana”.
Kama upo nje ya Kristo, basi fahamu kuwa kila silaha itakayofanyika juu yako itafanikiwa na itakudhuru. Hivyo usiruhusu silaha yoyote ifanikiwe juu yako. Ni sharti iharibiwe ikiwa katika hatua zake za matengenezo, na nguvu za kuweza kuharibiwa silaha hizo, ziko tu kwa wale walio ndani ya imani ya Kristo.

Swali: je umempokea Bwana Yesu? Kama bado, huu ni wakati wa kujiokoa nafsi yako. Siyo wakati wa kutazama nyuma, kama mke wa Lutu alivyogeuka nyuma, akawa jiwe la chumvi, bali ni wakati wa kupiga mbio na kuikimbia Sodoma. Maana yake ni kuacha kutenda mabaya, na kutenda mema machoni mwa Bwana Yesu.

Luka 17:32 “Mkumbukeni mkewe Lutu. 33 Mtu ye yote atakaye kuiponya nafsi yake, ataiangamiza; na ye yote atakayeiangamiza, ataiponya”.

Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa. Maana yake ni kuwa, tukiwa na ulinzi wa Mungu, hakuna adui anayeweza kutudhuru kwa hila wala ubaya wo wote.

Tunachotakiwa kufanya ni kujiunga na Bwana Yesu. Tufanye matendo mema yanayompendeza Mungu. Kwa kufanya hivyo, Mungu atatumia uweza wake kuharibu MIPANGO, SILAHA na NJAMA zote zitakazoandaliwa juu yetu.

Ni sisi wenyewe KUAMUA kujiunga na Bwana Yesu na kutekeleza Neno la Mungu.
 
Amen
 
Ahsante. Ubarikiwe mkuu
 
Back
Top Bottom