Fedor von Bock
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 2,321
- 2,157
Mkuu, hii maana yake ukienda mbele au nyuma lazima utarejea nyumbani. Kama mdau hapo juu alivyofafanua, kuwa "tezi" ni mbele ya chombo na "omo" ni nyuma ya chombo, na "ngamani" ni katikati ya chombo. Kwa hiyo, ili uweze kwenda mbele ya chombo, lazima upite katikati ya chombo [ngamani], na ukitaka kwenda nyuma ya chombo, utapita pia katikati ya chombo [ngamani].