Fedor von Bock
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 2,321
- 2,157
Ila atakula hata bokoboko...!Kiswahili kigumu kweli....mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
Kiswahili kigumu kweli....mgaagaa na upwa hali wali mkavu.
[emoji122][emoji122]Upwa ni sehemu ya bahari na mgaagaa ni mtu anayezurula maeneo ya upwa, maana yake ni kuwa mgaagaa hawezi kosa samaki hata Wa kupewa ndio maana hali wali mkavu. Tafsiri yake ni kuwa MTU anayejishughulisha hawezi kosa chochote hata Kama ni kidogo.
Mkimaliza hiyo kuna hii 'Kata pua uhunge wajii' sina uhakika kama nimepatia 'spelling' za kila neno ila ndiyo sielewagi kabisaa
Nimepata,nashukuru sana mzee MTU KITU" Kata pua uunge wajihi "
Chagua moja kati ya mawili / mengi lililosahihi ili ulifanye. Mfano , unataka kufanya biashara Ila mzee wako anaumwa , itabidi ukate pua na kuunga wajihi .....
Nahisi itakuwa umefahamu kidogo Gaspare Mbile
Dahh... Shukran mkuuTezi ni upande wa mbele wa meli ilhali Omo ni upande wa nyuma na ngamani ni katikati.
Hivi Chambilecho maana yake nini ?
Wengi wanadhani UPWA linatokana na neno MPWA ambalo unaweza kulitafsiri kama MTOTO WA NDUGU. Hivyo ukihangaika kulea watoto wa ndugu, hawatakutupa au hawatakusahau na vijizawadi.Upwa ni sehemu ya bahari na mgaagaa ni mtu anayezurula maeneo ya upwa, maana yake ni kuwa mgaagaa hawezi kosa samaki hata Wa kupewa ndio maana hali wali mkavu. Tafsiri yake ni kuwa MTU anayejishughulisha hawezi kosa chochote hata Kama ni kidogo.
Hivi Chambilecho maana yake nini ?