Nini maana ya Mwanadiplomasia?

MakaDik

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2019
Posts
239
Reaction score
136
Wapendwa nimekuwa nikilisikia mara nyingi hili neno lakini nashindwa kuelewa vema
 
Duh! Kwanini unajichosha sana kufikiria mkuu jibu mbona lipo wazi kabisa huyo ni mwana tu kama wana wengine
 
Wapendwa nimekuwa nikilisikia mara nyingi hili neno lakini nashindwa kuelewa vema
Ni Mbobevu / Mbobezi wa Masuala ya Kimataifa na Mahusiano yake kwa Ujumla.

Anaweza akawa ni Balozi au hata tu Mtumishi ila ni lazima awe chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na 99.9% huwa ni Manjagu ( Watu wa Usalama ) karibia katika Mataifa yote tu.

Ninawaachia Wengine Wakuelimishe.
 
Dah! Asante sana nimekuelewa vizuri.🙏🙏
 
Sio kweli
 
Dah! Asante sana nimekuelewa vizuri.🙏🙏
Karibu sana Ndugu. Na ukitaka Kuisomea hiyo Kozi Vyuo Vikuu inaitwa International Relations and Diplomacy na ukipata Kitengo utasafiri Ulaya, Marekani na Kote hadi uchoke Kupanda Ndege.
 
Sio kweli
Ungekuwa ni Intellectual hasa / kweli nadhani baada ya Kunipinga nawe ungekuja na Ufafanuzi wako ila tatizo lenu Wapumbavu na Waswahili kama Wewe ni kuwahi Kukosoa Jambo Kimajungu huku ukiwa huna Ufahamu wowote wa kile ulichokikataa.
 
Ok! Nimekusoma..asante kwa ushauri
 
Wapendwa nimekuwa nikilisikia mara nyingi hili neno lakini nashindwa kuelewa vema
Ni watu wanaowakilisha serikali za nchi zao katika nchi za nje. Hapo kuna balozi, mwakilishi, mfano wa umoja wa Afrika, Mataifa n.k.
 
Kwa Tz inaweza ikawa inapotoshwa (tunaona watu hata wa hovyo wanapewa ubalozi kama njugu) hasa hili la uana usalama, ila balozi hana vinasaba vya uana usalama. Kuna military attaché, muambata wa kijeshi katika balozi, Sina uhakika, pengine ndio anaweza akawa na majukumu ya usalama n.k.
Ila diplomats au wanadiplomasia ni mambo ya mahusiano (uwakilishi) zaidi
 
Karibu sana Ndugu. Na ukitaka Kuisomea hiyo Kozi Vyuo Vikuu inaitwa International Relations and Diplomacy na ukipata Kitengo utasafiri Ulaya, Marekani na Kote hadi uchoke Kupanda Ndege.
Hata ukisomea political science unaweza kufanya wizara ya mambo ya nje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…