Mimi ni mkristo... Nimejitahidi sana kutafuta mstari unaonipa uhakika wakuwa nikifanya hivyo nimeokoka ila nimeukosa... Yote inayoelezea wokovu ipo katika wakati ujao. Je, Ni Mstari gani au andiko gani linalotuthibitishia.. nikifanya hivi au vilw nitakua nimeokoka na sio nitakuja kuokoka?
Namaanisha... Kwanini tuseme tumeokoka wakati maandiko yanatuambia Tutaokoka.?
Halafu tusipende kulazimisha udini katika mada zilizo wazi. Swali ni nini maana ya Kuokoka. wewe imekuja na habari za Wokovu... kitu ambacho nakuona umenasa kwenye mtego wa mtoa mada.
Ulichokiandika sio sahihi kwa 100% kibiblia. Nitaweka ufafanuzi hapa.
Kwanza, huwezi kutenganisha Wokovu na kuokoka, kama usivyoweza kutenganisha Imani na kuamini, kifo na kufa, maisha na kuishi, ufufuo na kufufuka, chakula na kula nk. Wokovu ndio unazaa kitendo cha kuokoka.
Pili, Kibiblia, kiujumla, Kuokoka ni kumwamini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako. (MATENDO YA MITUME 16:30-31 (.....Yanipasa nifanye nini ili nipate kuokoka? Wakamwambia, Mwamini Bwana Yesu, nawe utaokoka pamoja na nyumba yako)
Tatu, yapo maandiko mengi kwenye Biblia yenye kueleza tukio la kuokoa katika wakati uliopita, na hapa kwa uchache nitakuwekea kwa mifano.
-ISAYA 45:20 (Jikusanyeni mje, na kukaribia pamoja, ninyi wa mataifa MLIOOKOKA)
-WAEFESO 2:5 (Hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na kristo, yaani, TUMEOKOLEWA kwa neema)
-WAEFESO 2:8 (Kwa maana MMEOKOLEWA kwa neema, kwa njia ya amani, ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu)
Nne, kuweka kumbukumbu sawa hawa JF, kimsingi tukio la wokovu (kuokoka) ni sasa (2Korintho 6:2) ukiwa unaliendea (bado hujaokoka) litakuwa kwa wakati ujao na ukiwa ulishafikia (tayari umeokoka) utalizungumzia katika wakati uliopita.
Mwisho,kibiblia hakuna wokovu (kuokoka) nje ya Yesu kristo (MATENDO YA MITUME 4:12 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwako)