Millionaire Mindset
Member
- Apr 19, 2018
- 83
- 115
Je, pesa ni bahati? hasa ya kuzaliwa nayo?
Je, pesa ni kitu kinachotafutwa?
Je, pesa ina thamani ile ile tunayoiamini?
Je, ni kwa nini walio wachache wanamiliki kiasi kikubwa cha pesa na kutuacha wengine tuking`ang`aniana “Vijisenti” vilivyobaki?
Hayo ni maswali yaliyowahi na yanaendelea kupita vichwani mwa watu wengi, hasa vijana wa kizazi hiki, ambao ndiyo nguvu kazi ya taifa.
Pesa ni bahati?
Wengine wanaamini kuwa na pesa ni bahati, na ndiyo maana wanakukuruka huku na kule, kucheza bahati nasibu mbalimbali kama betting, forex, n.k wakijaribu bahati zao; lakini wapo wengine wanaamua kwenda kusafishwa nyota zao kwa njia mbalimbali, wakiamini kuwa njia hizo zitawasafisha na kuwaletea hizo bahati.
Wengine wanafikiri kuwa pesa ni bahati ya kuzaliwa, kwa hiyo kama familia yenu hamko vizuri kifedha, basi maisha yako vile vile hayatabadilika, unaweza ukajitahidi kutafuta elimu au kufahamiana na kujiungamanisha na mtu aliyetoka kwenye familia kama hizo za wenye nazo na ndipo maisha yako yanaweza kuwa na unafuu.
‘Mindset’ hii ndiyo inayopelekea mtu kufanya juu chini ili aoe au aolewe na mtu mwenye nazo, la sivyo maisha yake hayawezi kufanikiwa.
Pesa inatafutwa?
Kundi lingine la watu wanaamini kuwa pesa inatafutwa, kwa hiyo wao wanaamini kuwa ni lazima mtu ujishughulishe na kujibidiisha na ndipo anaweza kuwa na pesa kibao kama waliofanikiwa wengine. Na ndiyo maana utamkuta mtu mwenye mtazamo wa aina hii yuko bize kweli kweli, mpaka kuna wakati anasahau ratiba ya kula, ili mradi tu, afanye kazi kwa bidii ili afanikiwe na kuwa na pesa nyingi.
Waliojiriwa na wana mtazamo wa aina hii, utawakuta wanajibidiisha kweli kweli, wengine wanarudi mashuleni na kuongeza elimu zao, wengine wanafanya kazi mpka masaa ya ziada. Yote hayo yanafanyika ili mradi wapande cheo na kuweza kukuza vipato vyao.
Maswali yanayofuata baada ya swali hili la pili, ndiyo haswaa yanayoibua mkanganyiko, kwenye “Mindset” hii. Kwa sababu licha ya kujibidiisha, watu wengi wa kundi hili bado wana “Struggle” kimaisha, mpaka wengine wanakata tamaa na kurudi kwenye kundi la kwanza kabisa hapo juu, la wale wanaowaza kuwa “Pesa ni bahati”.
Je, pesa ina thamani ile ile tunayoiamini? Pesa inalinganishwa na nini haswaa mpaka inakuwa ngumu kupatikana kiasi hiki? Bidii na jasho ndiyo vinavyotupatia pesa? Bahati ndiyo inayotupatia pesa?
Kabla ya kuendelea na Maada yetu, nataka nipate maoni yako, wewe unafikiri kipi ni kipi kuhusu pesa?