GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Naipenda sana asali, hasa asali mbichi. Ni tamu, na ina faida za kiafya. Je! Kuna ubaya endapo nitatumia kiasi kikubwa cha asli mbichi?
Nimejiwekea utaratibu wa kutumia asali mbichi mara kwa mara. Mwanzoni nilikuwa nikitumia Kwa siku chache mfululizo, kisha naacha kipindi kirefu kipite bila kuitumia. Lakini kwa siku za hivi karibuni, nimebadilisha utaratibu. Nimekuwa nikitumia kila siku, kiasi kwamba imeshakuwa kama moja ya viburudisho vyangu.
Kwa sasa, ninatumia Asubuhi mara tu ninapoamka, kabla ya kupiga mswaki, na Usiku muda mfupi kabla ya kulala!
Changamoto imekuwa kwenye kujipimia! Nilikusudia niwe natumia kijiko kimoja Asubuhi na kimoja Usiku, lakini mara nyingi nimekuwa nikitumia zaidi ya vijiko viwili kwa wakati mmoja. Kwa siku nzima, kuanzia Asubuhi mpaka Usiku, naweza nikatumia mpaka vijiko Sita vya chakula vilivyojaa asali.
Kuna siku nilitumia karibia nusu kikombe, kama si zaidi, ila kidogo kidogo. Niliiweka mezani nikawa naitumia kidogokidogo huku nikiendelea na shughuli zingine!
Je! Utumiaji wa aina hiyo unaweza ukawa na athari mbaya?