Nini madhara ya kuwa mlevi wa asali?

Nini madhara ya kuwa mlevi wa asali?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Naipenda sana asali, hasa asali mbichi. Ni tamu, na ina faida za kiafya. Je! Kuna ubaya endapo nitatumia kiasi kikubwa cha asli mbichi?

Nimejiwekea utaratibu wa kutumia asali mbichi mara kwa mara. Mwanzoni nilikuwa nikitumia Kwa siku chache mfululizo, kisha naacha kipindi kirefu kipite bila kuitumia. Lakini kwa siku za hivi karibuni, nimebadilisha utaratibu. Nimekuwa nikitumia kila siku, kiasi kwamba imeshakuwa kama moja ya viburudisho vyangu.

Kwa sasa, ninatumia Asubuhi mara tu ninapoamka, kabla ya kupiga mswaki, na Usiku muda mfupi kabla ya kulala!

Changamoto imekuwa kwenye kujipimia! Nilikusudia niwe natumia kijiko kimoja Asubuhi na kimoja Usiku, lakini mara nyingi nimekuwa nikitumia zaidi ya vijiko viwili kwa wakati mmoja. Kwa siku nzima, kuanzia Asubuhi mpaka Usiku, naweza nikatumia mpaka vijiko Sita vya chakula vilivyojaa asali.

Kuna siku nilitumia karibia nusu kikombe, kama si zaidi, ila kidogo kidogo. Niliiweka mezani nikawa naitumia kidogokidogo huku nikiendelea na shughuli zingine!

Je! Utumiaji wa aina hiyo unaweza ukawa na athari mbaya?
 
Evsrything too much is harmful.
Fanya kwa kiasi mkuu.
Changamoto ni kwamba ni tamu! Naipenda sana ladha yake!

Halafu wakati mwingine, nikipnanga kutumia kijiko kimoja tu, nikimaliza naona kama vile nimeituma kidogo sana, naona kama vile haitakuwa na athari nikiongeza kidoogo, kakijiko kimoja.

Lakini pia kuna taarifa kuwa hapo zamani kuna mtu alikuwa akiishi kwa kula nzige na asali pekee, yeye aliwezaje? Kama kula asali kwa wingi ina madhara mabaya, mbona hakuna taarifa ya huyo mtu kuathiriwa na asali?
 
Usisahau kwamba asali ni chakula jamii ya Carbohydrate (Fructose & Glucose), madhara ya matumizi ya asali katika mwili yanafanana na madhara ya matumizi ya vyakula vingine vyenye sukari.
 
Kuna mdau alishasema sukari ya kwenye asali ni tofauti na ya kiwandani. Kwamba, yenyewe Haina madhara kama ya kiwandani. Ukweli ni upi?
 
Naipenda sana asali, hasa asali mbichi. Ni tamu, na ina faida za kiafya. Je! Kuna ubaya endapo nitatumia kiasi kikubwa cha asli mbichi?

Nimejiwekea utaratibu wa kutumia asali mbichi mara kwa mara. Mwanzoni nilikuwa nikitumia Kwa siku chache mfululizo, kisha naacha kipindi kirefu kipite bila kuitumia. Lakini kwa siku za hivi karibuni, nimebadilisha utaratibu. Nimekuwa nikitumia kila siku, kiasi kwamba imeshakuwa kama moja ya viburudisho vyangu.

Kwa sasa, ninatumia Asubuhi mara tu ninapoamka, kabla ya kupiga mswaki, na Usiku muda mfupi kabla ya kulala!

Changamoto imekuwa kwenye kujipimia! Nilikusudia niwe natumia kijiko kimoja Asubuhi na kimoja Usiku, lakini mara nyingi nimekuwa nikitumia zaidi ya vijiko viwili kwa wakati mmoja. Kwa siku nzima, kuanzia Asubuhi mpaka Usiku, naweza nikatumia mpaka vijiko Sita vya chakula vilivyojaa asali.

Kuna siku nilitumia karibia nusu kikombe, kama si zaidi, ila kidogo kidogo. Niliiweka mezani nikawa naitumia kidogokidogo huku nikiendelea na shughuli zingine!

Je! Utumiaji wa aina hiyo unaweza ukawa na athari mbaya?
Kisukari.
Glycemic index ya asali ni karibu sawa na ya sukari. Tumia kwa kiasi
 
Kuna mdau alishasema sukari ya kwenye asali ni tofauti na ya kiwandani. Kwamba, yenyewe Haina madhara kama ya kiwandani. Ukweli ni upi?
Kila kitu kina madhara kama kisipofanywa kwa kiasi.

sukari ya kiwandani inapandisha sukari kwenye damu kwa kiwango kikubwa kuliko asali.
 
Nashukuru. Kiasi gani kwa mkupuo? Ni sawa nikitumia alau vijiko viwili Usiku na viwili Asubuhi? (Vijiko vya chakula)
Si rahisi kusema utumie vijiko vingapi kwa sababu kiafya matumizi ya sukari ya ziada (added sugar/free sugar) unayoipata kwenye bidhaa zilizowekewa sukari, na asalli, yanatakiwa yasizidi gram 36 kwa mwanaume na gram 24 kwa wanawake na watoto, changamoto ni bidhaa zetu nyingi ikiwemo asali, soda n.k hawaandiki ina kiasi gani (gram ngapi za sukari).
 
Back
Top Bottom