Nini madhara ya kuweka "N" wakati gari inatembea?

Nini madhara ya kuweka "N" wakati gari inatembea?

hakuna madhara katika gari, mtindo huu unabana mafuta pia unapunguza uchakavu wa gears. Labda kiusalama wa barabarani inaweza kuwa na madhara hasa kama wewe simtundu wa mambo haya.
 
Nilipata shida sana siku hiyo mkuu
Yawesekana gari yako silencer yake ilikua chini sana mkuu af we baada ya kutupia N ukakanyaga mafuta likazima
Hua ni atari sana maana mifumo yote inayotegemea engine kujiendesha husimama aswa break hua ngumu .
 
Yawesekana gari yako silencer yake ilikua chini sana mkuu af we baada ya kutupia N ukakanyaga mafuta likazima
Hua ni atari sana maana mifumo yote inayotegemea engine kujiendesha husimama aswa break hua ngumu .
Ni kweli nilikanyaga mafuta tena niliyakanyaga hasa maana nilikuwa nje ya wakati, sikulijua hilo.
 
Huwa sielewi logic ya kuweka FREE wakati injin inawaka kwani injin inawaka na maji...pili madhara yake unaua meno ya gear box shaft au needle bearing iliyopo kwenye fylwheel au kwenye automatic inakuwa kwenye toque convecter sababu inapokuwa free ukaachia na mafuta engine inarud kwenye silencer ila gear box inakuwa speed unapounganisha gear kunakuwa hakuna ratio ya mwendo unayotakiwa kati ya engine na gearbox kwa wale waliowahi kufanya change down wanajua ninachokisema ila hili madhara yanakula pole pole na kuna siku litakubumia...ili usiharibu hakikisha unazoefu na gari ujue RPM ikiwa ngapi uingize gear gan ili kuwrka ratio sawa ila kwa auto matic unaitesa zaid gearbox kuliko engine.!
0 genious. .... ulichoandika sidhani km unakielewa # own fantasy .....
 
Gari inapokua kwenye motion ukaweka N then urudi D... kuna madhara makubwa saana kwenye Gia box ila madhara hayo yanajijenga taratibu kwa kuua meno ya gia box...
 
Nini utokea endapo ukaweka N then ukajisahau na kukanyaga mafuta
 
Kwenye mteremko geer ni muhimu ili emergence ikitokea uweze kutawala gari. Hata hivyo ni faida kwa wapiga nyoka .
 
Niliwahi soma sehemu kwamba gari ikiwa N halafu inaenda hata mzunguko wa oil kwenye engine unakuwa mdogo hivyo kupelekea kuichosha engine pia.
Na mimi nilikuwa na mtindo huo hasa kwenye mtelemko ila kuna siku nikajisahau badala ya kurudisha kwenye D nikapandisha juu kwenye R kilichotokea sitaki kukumbuka toka siku hiyo sifanyi ujinga huo
Hii jib ndo nilikua nalitaka,daah nashkuru kiongoz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom