Nini mamlaka ya Mo Dewji ndani ya Simba?

Mbumbumbu fc wasicho elewa hakuna kinachoitwa mfumo mpya wa uendeshaji Klabu ya Simba mbaka Sasa. MO anaiendesha Simba Kama ilivyokua Manji kwakua mchakato hauja kamilika, Ila kwakua MO ananguvu ya pesa ndio maana anaisemea Klabu.
Simba ki uhalisia ipo vile vile haina uwezo wa kujiendesha bila wadhamini mbalimbali, mfumo mpya wa uendeshaji Klabu haujawa tayari na aijulikani Kama ukianza kazi rasmi itachukua muda gani Klabu kujiendesha yenyewe kwa mapato yake.
MO akiondoka Leo Simba itabaki Kama ilivyokua apo awali, Pesa anazoweka MO ni mapenzi yake binafsi. CEO ni cheo Cha mfumo mpya, Mkurgenzi ni cheo katika mfumo mpya Ila mfumo wenyewe mpya haujatambuliwa na Serikali kwaiyo hakuna jipya Ila Mambo yanafanyika kinadharia.
hivi mmeshajiuliza mamlaka aliyopewa GSM ya kusajili wachezaji na kufukuza makocha, hebu toeni mwiko nyuma mpate akili.
 
GSM ni mdau katika biashara na anayo yafanya nje ya mkataba ni kwa mapenzi yake binafsi kwa Yanga.
 
Mtoa maada yuko sahihi, Mo alipaswa kusubiri mkataba uishe kwanza, afu kingine kipindi mkataba wanasaini Simba ilikua na hali mbaya
 
Mkwabi ni mwanasimba mwenzangu tunaweza kujadiliana kama wanasimba ila kichekesho ni utopolo kufungua thread kuhusu Simba wakati haiwahusu.

Tofauti ya Nkwabi na utopolo, Nkwabi hawezi kuihujumu Simba wala hawezi kufurahia anguko la Simba lakini nyinyi upotolo mnalala mkiwaza namna gani Simba iporomoke
Wew jamaaa unaongea kishabiki Sana,kweli yule aliye leta hoja nishabik wa uto ila mjibu hoja yake n Wal xio ushabik wake..... Mathalan kuna kipindi cha karibun kuliibuka tetes za Chelsea kuudhwa na 1 wa watu walio kuwa wanahitaj kununua alikuwa tajir ambaye ni shabik wa man u, ni kiwa na Maan toka mchakato wa simba uanze ni zaid ya miaka 4 Sasa lkn hakuna maendeleo yanayo letwa kwa wanachama na mashabik wa simba au wa mpira hap nchin kutoka kwa uongoz wa simba ila kwa kuwa sas timu inafany vzr hatuwez kuangalia kasoro zilizopo kwa sas ila linapokuja kutokea huk mbelen tunakuwa tumechelewa
 
Utopolo angaikeni na timu yenu mpaka sasa hivi hamna kocha mkuu, mlianza kupokea timu za nje lakini hamna mluchopata pamoja na tofauti zilizopi Simba lakini sasa hivi tuna mashindano makubwa tunahitaji mshikamano lakini nyie kila mkiamka mnaiwaza simba au mmesahau mlianzisha thread ngapi kabla Simba hajacheza na As Vita au kabla Simba hajacheza na Al haily leo hii mnajifanya malaika kutupa ushauri.
 
Ikitokea MO amefariki ,je huu mchakato unaendelea au ndio basi tena
 
Utopolo angaikeni na timu yenu mpaka sasa hivi hamna kocha mkuu, mlianza kupokea timu za nje lakini hamna mluchopata pamoja na tofauti zilizopi Simba lakini sasa hivi tuna mashindano makubwa tunahitaji mshikamano lakini nyie kila mkiamka mnaiwaza simba au mmesahau mlianzisha thread ngapi kabla Simba hajacheza na As Vita au kabla Simba hajacheza na Al haily leo hii mnajifanya malaika kutupa ushauri.
Kwanza mpira wa bongo xio mpenz San kwa sas, Labd dhami nilikuwa kindakinda ila leo hata wachezj 4 siwez taja, iwe simba au yanga, ila jambo nalo muunga mkono mtoa Mada ni kule kuwa na mtu ambaye ananufaika Zaid na simba kuliko simba inavyo faidika na yeye, leo watu wanasema MO kaifanya simba inacheza makundi ila wanasahau simba Aliya fanya hayo miak kumi nyuma tena ikiwa ungaunga mwana kipind cha mwina kaduguda Kam sijakosea (naruhusu kukosolewa)... Ila sas simba bado haina vyanzo vyak kama simba hapo ndo tu nakuja kumsakama MO ambay yy ni manji aliye changamka
 
Nipende kutoa pole zangu za dhati kwa Watanzania wote pamoja na Waafrika kwa kupoteza Kiongozi jasiri na shupavu, Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikuwa ni Rais wa Tanzania awamu ya tano.

Lakini tukiwa bado kwenye mwendelezo wa maombelezo ya siku 21 ya kitaifa ndipo anaibuka Mdhamini wa Klabu ya Simba ambaye nguvu yake ya kimkataba wa mahusiano yao ni umiliki wa hisa wa asilimia 49 huku Wanamsimbazi ikibakiwa na asilimia 51.

Napenda tuanzie hapa kwenye hisa kwani hizo namba 51 na 49 si namba tu bali zina maana kubwa sana ikiwa pamoja na nguvu ya kimamlaka, uamuzi na mapendekezo katika kuenenda ili kufanikisha mambo baina ya pande mbili husika.

Katika hali ya kawaida Klabu ya Simba wana nguvu kubwa kwani wao ndio wana sehemu kubwa ya umiliki ikiwa ni zaidi ya nusu ukiangalia kwa namba.

Hivyo napenda kwa pamoja tujiulize Mo Dewji anapoibuka na kuanza kudhihaki udhamini wa Sportpesa na Simba; tena amefanya hivyo tena kienyeji kabisa kwa kutumia ukurasa wake binafsi huku akiwa si Mwenyekiti wa Simba. Unajiuliza hiyo nguvu ameitoa wapi?

Katika hali ya kawaida na kiungwana udhamini wa Simba na Sportpesa umedumu kwa zaidi ya miaka mitano sasa huku Sportpesa wakihusika katika kulipa mishahara na huduma zingine za kiuendeshaji na kupata nafasi ya kuweka tangazo lao katika jezi za klabu husika.

Uwepo wa Sportpesa umesaidia mengi kwenye maendeleo ya Klabu ya Simba jambo ambalo ni la kushukuriwa hata kama kuna maeneo yana upungufu.

Katika kipindi hiki ambacho mkataba huo unaelekea ukingoni ilikuwa ni wasaa wa pande mbili kwa maana ya Simba na Sportpesa kukaa mezani na kujadiliana na kuona namna ya kuboresha ama laah, na endapo wasipofikia makubaliano basi kupitia Mwenyekiti wa klabu ambao ndiyo wenye hisa 51 ndio wangetoa mwelekeo tena kwa utaratibu maalumu, lakini cha ajabu anaibuka mdhamini ambaye naye ni mshindani wa kibiashara na Sportpesa na kutoa kauli yenye dhihaka kitu ambacho hakitoi taswira nzuri kwa wadhamini wengine na kunaweza kuweka mazingira magumu kwa wadhamini wengine kuja kuwekeza kwenye klabu ya Simba.

Lakini kwa dhihaka ambazo Mo Dewji amezitoa kwa Sportpesa kwa udhamini wao je yeye ambaye ameendelea kutumia nembo ya Simba na kuweka matangazo yake kwenye jezi za Msimbazi kila kona, ameifaidisha klabu kwa kiasi gani?

Udhamini wa MO EXTRA na MO HALISI unatoa tija kiasi gani kwa Simba SC. Je kinachotolewa na SPORTPESA kinafanana na wanachokipata Simba SC kupitia hizo bidhaa mbili ambazo Mo Dewji anazitangaza kupitia na nembo na jezi za Simba SC?

Leo atoke hadharani atuambie kila bidhaa anayoitangaza kupitia Simba SC kwa mwaka klabu inafaidika vipi na wanapata kiasi gani na kipo wapi?

Vilevile Wanasimba na Watanzania wanatakiwa waelewe kuwa Mo Dewji na makampuni yao sio wenye dhamana ya uongozi.

Hii ni kwa sababu wakati wowote na kwa sababu yeyote wanaweza kujitoa Simba kuamua kuingia ubia na kampuni yeyote hivyo kutumia nafasi yake ya udhamini wa asilimia 49 na kujivika nafasi ya Simba SC ni kosa na kuidhalilisha klabu kwani inaonekana haina nguvu na ule umiliki wa asilimia 51 hauna kitu wala tija ilihali wametoka kuchagua mwenyekiti mpya hivi karibuni.

Kwa alichokifanya Mo Dewji leo, Je ni makubaliano baina ya makampuni yake na Simba?

Au ni utashi wake? Kama ni utashi wake maana yake hatambui mipaka yake na yule Mwenyekiti wa Simba aliyepewa dhamana ya kulinda umiliki wa asilimia 51 yupo kama picha tu.

Biashara ni makubaliano inapofikia mmeshindwa kukubaliana ni vema mkaachana kwa amani huku kila mmoja akilinda heshma yake na heshma ya upande wa pili.

Leo kuja kuidhihaki Sportpesa ni sawa na si uungwana yapo mengi wameyafanya kwa klabu ya Simba.

Hili swala si la kiushabiki ni vema wanasimba mkaanza kuona namna ambavyo klabu yenu inavyokwenda kutaifishwa na kuwa timu ya familia na niliandika hili.

Leo hii zile shilingi Bilioni 20 zimebaki hadithi isiyokwisha wala hasemi ataziweka lini?

Amebaki anaruka kama maharagwe ya Mbeya na kuanza kuchokonoa wadhamini wengine ambao wanafanya kazi na Simba huku mkataba ukiwa bado upo na kuonesha dhihaka na dharau.

Najua wenye uwelewa na mapenzi mema na Simba watakuwa wamenielewa ila wale wachumia tumbo vichawa vya Mo Dewji watatafuta majibu rahisi juu ya hili, lakini pia wanachama ni wakati wa kujitafakari huku mkihoji mwenyekiti wenu mmemchagua kwa kazi gani?

Njia niliyotumia kwenda ndio nitakayorudia

Msemakweli wa haki

NimemalizaView attachment 1732281
Anataka kuweka bidhaa yake pale mbele
 
mara ya mwisho simba kuingia makundi kabla ya mwaka juzi na huu chini y aMO ilikuwa 2003 na mwezeweshaji alikuwa huyohuyo MO zaidi ya hapo ni fainali ya CAF 1993 chini ya ucle wake Mo azim dewji na nusu fanali ya club bingwa 1974 ilikuwa chini ya wazawa weusi
 
Kwanza mpira wa bongo xio mpenz San kwa sas, Labd dhami nilikuwa kindakinda ila leo hata wachezj 4 siwez taja, iwe simba au yanga, ila jambo nalo muunga mkono mtoa Mada ni kule kuwa na mtu ambaye ananufaika Zaid na simba kuliko simba inavyo faidika na yeye, leo watu wanasema MO kaifanya simba inacheza makundi ila wanasahau simba Aliya fanya hayo miak kumi nyuma tena ikiwa ungaunga mwana kipind cha mwina kaduguda Kam sijakosea (naruhusu kukosolewa)... Ila sas simba bado haina vyanzo vyak kama simba hapo ndo tu nakuja kumsakama MO ambay yy ni manji aliye changamka
Kama sio mpenzi wa mpira tuachie sisi tunaojua kuhusu simba na yanga. Simba ni taasisi inayojitegemea wala haiitaji ushauri toka upotolo.
Kama utopolo waliweza kupokea timu pinzani na Simba pamoja na kwamba mafanikio ya Simba kimataifa yanawabeba na wao leo wamepata uchungu gani kuhusu Simba hadi watuanzishie thread.
Kuna mgogoro ulitokea kati ya gsm na baadhi ya wajumbe wa kamati wa utendaji wa upotolo wajiuzulu ulisikia Simba wakiongea popote.
Utopolo wanaishi kwa migogoro na wanatamani na sisi tuwe kama wao.
 
Tatizo aliyeleta hii mada ni utopolo. Na hakuna utopolo anauetaka maendeleo ya mnyama. Ataendelea kupata kiungulia tu. Atulie dawa ifanye kazi. Mo ametoa tu mawazo yake. Amabauo ni ua kweli. Sasa eti anataka sportpesa eti waonewe huruma kisa waliisaidia Simba. Kwenye biashara hakuna huruma. Huruma apeleke kwenye wenye mahitaji maalum.
 
Kama amefanya hivyo huku akiwa si mwenyekiti wa Simba, basi haina madhara yoyote, ni maoni ya mshabiki tu kwa hiyo isikusumbue. Uzi ufungwe
Hapana aisee, tukubali tu kibiashara hapa Mudi ametoa boko.
 
Nipende kutoa pole zangu za dhati kwa Watanzania wote pamoja na Waafrika kwa kupoteza Kiongozi jasiri na shupavu, Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikuwa ni Rais wa Tanzania awamu ya tano.

Lakini tukiwa bado kwenye mwendelezo wa maombelezo ya siku 21 ya kitaifa ndipo anaibuka Mdhamini wa Klabu ya Simba ambaye nguvu yake ya kimkataba wa mahusiano yao ni umiliki wa hisa wa asilimia 49 huku Wanamsimbazi ikibakiwa na asilimia 51.

Napenda tuanzie hapa kwenye hisa kwani hizo namba 51 na 49 si namba tu bali zina maana kubwa sana ikiwa pamoja na nguvu ya kimamlaka, uamuzi na mapendekezo katika kuenenda ili kufanikisha mambo baina ya pande mbili husika.

Katika hali ya kawaida Klabu ya Simba wana nguvu kubwa kwani wao ndio wana sehemu kubwa ya umiliki ikiwa ni zaidi ya nusu ukiangalia kwa namba.

Hivyo napenda kwa pamoja tujiulize Mo Dewji anapoibuka na kuanza kudhihaki udhamini wa Sportpesa na Simba; tena amefanya hivyo tena kienyeji kabisa kwa kutumia ukurasa wake binafsi huku akiwa si Mwenyekiti wa Simba. Unajiuliza hiyo nguvu ameitoa wapi?

Katika hali ya kawaida na kiungwana udhamini wa Simba na Sportpesa umedumu kwa zaidi ya miaka mitano sasa huku Sportpesa wakihusika katika kulipa mishahara na huduma zingine za kiuendeshaji na kupata nafasi ya kuweka tangazo lao katika jezi za klabu husika.

Uwepo wa Sportpesa umesaidia mengi kwenye maendeleo ya Klabu ya Simba jambo ambalo ni la kushukuriwa hata kama kuna maeneo yana upungufu.

Katika kipindi hiki ambacho mkataba huo unaelekea ukingoni ilikuwa ni wasaa wa pande mbili kwa maana ya Simba na Sportpesa kukaa mezani na kujadiliana na kuona namna ya kuboresha ama laah, na endapo wasipofikia makubaliano basi kupitia Mwenyekiti wa klabu ambao ndiyo wenye hisa 51 ndio wangetoa mwelekeo tena kwa utaratibu maalumu, lakini cha ajabu anaibuka mdhamini ambaye naye ni mshindani wa kibiashara na Sportpesa na kutoa kauli yenye dhihaka kitu ambacho hakitoi taswira nzuri kwa wadhamini wengine na kunaweza kuweka mazingira magumu kwa wadhamini wengine kuja kuwekeza kwenye klabu ya Simba.

Lakini kwa dhihaka ambazo Mo Dewji amezitoa kwa Sportpesa kwa udhamini wao je yeye ambaye ameendelea kutumia nembo ya Simba na kuweka matangazo yake kwenye jezi za Msimbazi kila kona, ameifaidisha klabu kwa kiasi gani?

Udhamini wa MO EXTRA na MO HALISI unatoa tija kiasi gani kwa Simba SC. Je kinachotolewa na SPORTPESA kinafanana na wanachokipata Simba SC kupitia hizo bidhaa mbili ambazo Mo Dewji anazitangaza kupitia na nembo na jezi za Simba SC?

Leo atoke hadharani atuambie kila bidhaa anayoitangaza kupitia Simba SC kwa mwaka klabu inafaidika vipi na wanapata kiasi gani na kipo wapi?

Vilevile Wanasimba na Watanzania wanatakiwa waelewe kuwa Mo Dewji na makampuni yao sio wenye dhamana ya uongozi.

Hii ni kwa sababu wakati wowote na kwa sababu yeyote wanaweza kujitoa Simba kuamua kuingia ubia na kampuni yeyote hivyo kutumia nafasi yake ya udhamini wa asilimia 49 na kujivika nafasi ya Simba SC ni kosa na kuidhalilisha klabu kwani inaonekana haina nguvu na ule umiliki wa asilimia 51 hauna kitu wala tija ilihali wametoka kuchagua mwenyekiti mpya hivi karibuni.

Kwa alichokifanya Mo Dewji leo, Je ni makubaliano baina ya makampuni yake na Simba?

Au ni utashi wake? Kama ni utashi wake maana yake hatambui mipaka yake na yule Mwenyekiti wa Simba aliyepewa dhamana ya kulinda umiliki wa asilimia 51 yupo kama picha tu.

Biashara ni makubaliano inapofikia mmeshindwa kukubaliana ni vema mkaachana kwa amani huku kila mmoja akilinda heshma yake na heshma ya upande wa pili.

Leo kuja kuidhihaki Sportpesa ni sawa na si uungwana yapo mengi wameyafanya kwa klabu ya Simba.

Hili swala si la kiushabiki ni vema wanasimba mkaanza kuona namna ambavyo klabu yenu inavyokwenda kutaifishwa na kuwa timu ya familia na niliandika hili.

Leo hii zile shilingi Bilioni 20 zimebaki hadithi isiyokwisha wala hasemi ataziweka lini?

Amebaki anaruka kama maharagwe ya Mbeya na kuanza kuchokonoa wadhamini wengine ambao wanafanya kazi na Simba huku mkataba ukiwa bado upo na kuonesha dhihaka na dharau.

Najua wenye uwelewa na mapenzi mema na Simba watakuwa wamenielewa ila wale wachumia tumbo vichawa vya Mo Dewji watatafuta majibu rahisi juu ya hili, lakini pia wanachama ni wakati wa kujitafakari huku mkihoji mwenyekiti wenu mmemchagua kwa kazi gani?

Njia niliyotumia kwenda ndio nitakayorudia

Msemakweli wa haki

NimemalizaView attachment 1732281
Juzi kwenye mkutano wa Simba wamegoma kabisa kutusomea na kutupatia taarifa ya Fedha kwa kigezo eti tunawahi mechi ya Mpira sijui tulikuwa tunacheza nadhani na Azam.. wakatosomea summary ya jumla ya mapato na matumizi arafu kilichonishangaza wansema eti kwa mara ya kwanza tumetengeneza faida ya milioni 34 huku kati ya mapato yote tuliokusanya eti MO alitoa zaidi ya 2 billion msaada...kazi kweli kweli
 
Kumbe baadhi ya wanachama wa mbumbumbu fc Wana akili timamu. Najua wanasubiri wakati sahihi ufike washike nafasi kuonyesha umma wenye akili timamu Bado wapo pale umbumbumbuni.
 
Back
Top Bottom