Nini mamlaka ya Mo Dewji ndani ya Simba?

Nipende kutoa pole zangu za dhati kwa Watanzania wote pamoja na Waafrika kwa kupoteza Kiongozi jasiri na shupavu, Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikuwa ni Rais wa Tanzania awamu ya tano.

Lakini tukiwa bado kwenye mwendelezo wa maombelezo ya siku 21 ya kitaifa ndipo anaibuka Mdhamini wa Klabu ya Simba ambaye nguvu yake ya kimkataba wa mahusiano yao ni umiliki wa hisa wa asilimia 49 huku Wanamsimbazi ikibakiwa na asilimia 51.

Napenda tuanzie hapa kwenye hisa kwani hizo namba 51 na 49 si namba tu bali zina maana kubwa sana ikiwa pamoja na nguvu ya kimamlaka, uamuzi na mapendekezo katika kuenenda ili kufanikisha mambo baina ya pande mbili husika.

Katika hali ya kawaida Klabu ya Simba wana nguvu kubwa kwani wao ndio wana sehemu kubwa ya umiliki ikiwa ni zaidi ya nusu ukiangalia kwa namba.

Hivyo napenda kwa pamoja tujiulize Mo Dewji anapoibuka na kuanza kudhihaki udhamini wa Sportpesa na Simba; tena amefanya hivyo tena kienyeji kabisa kwa kutumia ukurasa wake binafsi huku akiwa si Mwenyekiti wa Simba. Unajiuliza hiyo nguvu ameitoa wapi?

Katika hali ya kawaida na kiungwana udhamini wa Simba na Sportpesa umedumu kwa zaidi ya miaka mitano sasa huku Sportpesa wakihusika katika kulipa mishahara na huduma zingine za kiuendeshaji na kupata nafasi ya kuweka tangazo lao katika jezi za klabu husika.

Uwepo wa Sportpesa umesaidia mengi kwenye maendeleo ya Klabu ya Simba jambo ambalo ni la kushukuriwa hata kama kuna maeneo yana upungufu.

Katika kipindi hiki ambacho mkataba huo unaelekea ukingoni ilikuwa ni wasaa wa pande mbili kwa maana ya Simba na Sportpesa kukaa mezani na kujadiliana na kuona namna ya kuboresha ama laah, na endapo wasipofikia makubaliano basi kupitia Mwenyekiti wa klabu ambao ndiyo wenye hisa 51 ndio wangetoa mwelekeo tena kwa utaratibu maalumu, lakini cha ajabu anaibuka mdhamini ambaye naye ni mshindani wa kibiashara na Sportpesa na kutoa kauli yenye dhihaka kitu ambacho hakitoi taswira nzuri kwa wadhamini wengine na kunaweza kuweka mazingira magumu kwa wadhamini wengine kuja kuwekeza kwenye klabu ya Simba.

Lakini kwa dhihaka ambazo Mo Dewji amezitoa kwa Sportpesa kwa udhamini wao je yeye ambaye ameendelea kutumia nembo ya Simba na kuweka matangazo yake kwenye jezi za Msimbazi kila kona, ameifaidisha klabu kwa kiasi gani?

Udhamini wa MO EXTRA na MO HALISI unatoa tija kiasi gani kwa Simba SC. Je kinachotolewa na SPORTPESA kinafanana na wanachokipata Simba SC kupitia hizo bidhaa mbili ambazo Mo Dewji anazitangaza kupitia na nembo na jezi za Simba SC?

Leo atoke hadharani atuambie kila bidhaa anayoitangaza kupitia Simba SC kwa mwaka klabu inafaidika vipi na wanapata kiasi gani na kipo wapi?

Vilevile Wanasimba na Watanzania wanatakiwa waelewe kuwa Mo Dewji na makampuni yao sio wenye dhamana ya uongozi.

Hii ni kwa sababu wakati wowote na kwa sababu yeyote wanaweza kujitoa Simba kuamua kuingia ubia na kampuni yeyote hivyo kutumia nafasi yake ya udhamini wa asilimia 49 na kujivika nafasi ya Simba SC ni kosa na kuidhalilisha klabu kwani inaonekana haina nguvu na ule umiliki wa asilimia 51 hauna kitu wala tija ilihali wametoka kuchagua mwenyekiti mpya hivi karibuni.

Kwa alichokifanya Mo Dewji leo, Je ni makubaliano baina ya makampuni yake na Simba?

Au ni utashi wake? Kama ni utashi wake maana yake hatambui mipaka yake na yule Mwenyekiti wa Simba aliyepewa dhamana ya kulinda umiliki wa asilimia 51 yupo kama picha tu.

Biashara ni makubaliano inapofikia mmeshindwa kukubaliana ni vema mkaachana kwa amani huku kila mmoja akilinda heshma yake na heshma ya upande wa pili.

Leo kuja kuidhihaki Sportpesa ni sawa na si uungwana yapo mengi wameyafanya kwa klabu ya Simba.

Hili swala si la kiushabiki ni vema wanasimba mkaanza kuona namna ambavyo klabu yenu inavyokwenda kutaifishwa na kuwa timu ya familia na niliandika hili.

Leo hii zile shilingi Bilioni 20 zimebaki hadithi isiyokwisha wala hasemi ataziweka lini?

Amebaki anaruka kama maharagwe ya Mbeya na kuanza kuchokonoa wadhamini wengine ambao wanafanya kazi na Simba huku mkataba ukiwa bado upo na kuonesha dhihaka na dharau.

Najua wenye uwelewa na mapenzi mema na Simba watakuwa wamenielewa ila wale wachumia tumbo vichawa vya Mo Dewji watatafuta majibu rahisi juu ya hili, lakini pia wanachama ni wakati wa kujitafakari huku mkihoji mwenyekiti wenu mmemchagua kwa kazi gani?

Njia niliyotumia kwenda ndio nitakayorudia

Msemakweli wa haki

NimemalizaView attachment 1732281
Yote hii ni ile kunyimwa ule mkopo wa pikipiki ndiyo umeamua kutumika kiboya hivi.
 
Mbumbumbu fc wasicho elewa hakuna kinachoitwa mfumo mpya wa uendeshaji Klabu ya Simba mbaka Sasa. MO anaiendesha Simba Kama ilivyokua Manji kwakua mchakato hauja kamilika, Ila kwakua MO ananguvu ya pesa ndio maana anaisemea Klabu.
Simba ki uhalisia ipo vile vile haina uwezo wa kujiendesha bila wadhamini mbalimbali, mfumo mpya wa uendeshaji Klabu haujawa tayari na aijulikani Kama ukianza kazi rasmi itachukua muda gani Klabu kujiendesha yenyewe kwa mapato yake.
MO akiondoka Leo Simba itabaki Kama ilivyokua apo awali, Pesa anazoweka MO ni mapenzi yake binafsi. CEO ni cheo Cha mfumo mpya, Mkurgenzi ni cheo katika mfumo mpya Ila mfumo wenyewe mpya haujatambuliwa na Serikali kwaiyo hakuna jipya Ila Mambo yanafanyika kinadharia.
Kwanini msijipe homework kidogo?!kuliko kukulupuka na kuandika chochote!! Simbasc ni club ya wanachama,kwa umoja wao kupitia mkutano mkuu,wanachama walikubali kuanza mchakato wa mabadiliko ya katiba kupitia taratibu zote,
Baada ya kuunda rasimu ya katiba,wanachama wote kupitia mkutano mkuu wakaipitisha rasimu ya katiba,ikiwa na mabadiliko,wakaipeleka (serikalini) kwa msajili wa vyama vya michezo,ikapitishwa na kuwa katiba rasmi ya simbasc.hivyo Simba moja kwa moja ikabadilika na kuwa kampuni,ikapata na usajili brella,na kwa mujibu wa katiba iliyopitishwa Simbasc inamtambua mwekezaji na asilimia zake,na pia katiba inatambua kuwepo kwa bodi ya wakurugenzi,na pia inaeleza kutakuwa na secretarieti ya timu ambayo itakuwa inafanya kazi za kila siku za uendeshaji wa timu,ambayo itaongozwa na mtendaji mkuu,ambae atawajibika kwa bodi ya wakurugenzi!!na katiba ya Simbasc inaeleza mwekezaji ndie atakuwa mwenyekiti wa bodi ya timu,kwa mujibu wao walivyo amua.hizi taratibu nyingine sijui FCC ni taratibu tu za serikalini za kutoa miongozo na wala hazina uwezo wowote wa kuzuia maamuzi ya wenye timu yao ambao ndio wanachama.
Hivyo ukimuona MO anazungumza,ujue anazungumza kama mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi,na pia kama mwanachama wa Simbasc, ambae nae ana haki zote kama wanachama wengine.
 
Simba SC ni kama daladala na Mo ndio mmiliki wake. Imeisha hiyo. Mwenye daladala akisema naliuza au sitengenezi, ndiyo imetoka tena.
 
Wewe inaonekana ni mmoja wa wanufaikaji wa uwepo wa MO pale msimbazi, Simba Ina secretariet, bodi ya wakurugenzi n.k nieleze kampuni iyo ya Simba na uyo mwekezaji mbaka Sasa Wana fanya biasharagani, uwekezaji katika iyo biashara inayofanywa ni upi na unathamani gani na Kama FCC si lolote wala chochote katika mabadiliko ya Simba.

Nini kinakwamisha mbaka mwekezaji anasita kuweka mzigo wakati Katiba ya Simba ilisha pitishwa kwa msajili na kampuni imesha sajiliwa brela? Yaani wewe mshauri wa MO unahisi watu wote ni ma Mbumbumbu sio?
 
Ulitaka kuwekeza simba afu MO akakuzuia, au ndo ujuaji wa wa kiboya tu?
 
Umeandika utopolo kabisa MO ni mdhamini,lakini pia ni mwenyekiti ndani ya bodi ya wadhamini au wawekezaji

Kama vipi nyinyi komaeni na sporti pesa tu Simba imekuwa next level.

Msifosi tufanane
 
Ulitaka kuwekeza simba afu MO akakuzuia, au ndo ujuaji wa wa kiboya tu?
Wewe uoni Kama Sports pesa wanafukuzwa, MO hataki ushindani. yeye ndie mkurgenzi wa bodi na yeye ndie anaye miliki biashara zote zinazo husiana na timu.
 
Simba SC ni kama daladala na Mo ndio mmiliki wake. Imeisha hiyo. Mwenye daladala akisema naliuza au sitengenezi, ndiyo imetoka tena.
Hivi huko Utopolo kuna mwenye akili timamu kweli? Mbona mpo kinyani nyani hivi?
FB_IMG_1610796811518.jpg
 
Wewe inaonekana ni mmoja wa wanufaikaji wa uwepo wa MO pale msimbazi, Simba Ina secretariet, bodi ya wakurugenzi n.k nieleze kampuni iyo ya Simba na uyo mwekezaji mbaka Sasa Wana fanya biasharagani, uwekezaji katika iyo biashara inayofanywa ni upi na unathamani gani na Kama FCC si lolote wala chochote katika mabadiliko ya Simba.

Nini kinakwamisha mbaka mwekezaji anasita kuweka mzigo wakati Katiba ya Simba ilisha pitishwa kwa msajili na kampuni imesha sajiliwa brela? Yaani wewe mshauri wa MO unahisi watu wote ni ma Mbumbumbu sio?
Hivi GSM alishaweka 20B ?
 
Ndio shida ya kuwaongoza mbumbumbu wao wanaona sawa ili mradi ushindi unapatikana yule mwenyekiti ni picha tu pale we unafikiri kwanini mwenyekiti wa zamani alifukuzwa na Mo haina shaka Mo atatuchezea mpaka tukome
 
Hivi mkishaandika mnapitia tena maandishi yenu, nyie wakati manji kajiuzulu si mligoma kufanya uchaguzi kila siku mnadanganyana anarudi.
Kwa sababu mwakalebela keshawajua ndio maana anawadanganya kamfungulia kesi Morison cas na nyie.mnabaki mkisubiria
 
Nipende kutoa pole zangu za dhati kwa Watanzania wote pamoja na Waafrika kwa kupoteza Kiongozi jasiri na shupavu, Hayati Dk. John Pombe Joseph Magufuli ambaye alikuwa ni Rais wa Tanzania awamu ya tano.

Lakini tukiwa bado kwenye mwendelezo wa maombelezo ya siku 21 ya kitaifa ndipo anaibuka Mdhamini wa Klabu ya Simba ambaye nguvu yake ya kimkataba wa mahusiano yao ni umiliki wa hisa wa asilimia 49 huku Wanamsimbazi ikibakiwa na asilimia 51.

Napenda tuanzie hapa kwenye hisa kwani hizo namba 51 na 49 si namba tu bali zina maana kubwa sana ikiwa pamoja na nguvu ya kimamlaka, uamuzi na mapendekezo katika kuenenda ili kufanikisha mambo baina ya pande mbili husika.

Katika hali ya kawaida Klabu ya Simba wana nguvu kubwa kwani wao ndio wana sehemu kubwa ya umiliki ikiwa ni zaidi ya nusu ukiangalia kwa namba.

Hivyo napenda kwa pamoja tujiulize Mo Dewji anapoibuka na kuanza kudhihaki udhamini wa Sportpesa na Simba; tena amefanya hivyo tena kienyeji kabisa kwa kutumia ukurasa wake binafsi huku akiwa si Mwenyekiti wa Simba. Unajiuliza hiyo nguvu ameitoa wapi?

Katika hali ya kawaida na kiungwana udhamini wa Simba na Sportpesa umedumu kwa zaidi ya miaka mitano sasa huku Sportpesa wakihusika katika kulipa mishahara na huduma zingine za kiuendeshaji na kupata nafasi ya kuweka tangazo lao katika jezi za klabu husika.

Uwepo wa Sportpesa umesaidia mengi kwenye maendeleo ya Klabu ya Simba jambo ambalo ni la kushukuriwa hata kama kuna maeneo yana upungufu.

Katika kipindi hiki ambacho mkataba huo unaelekea ukingoni ilikuwa ni wasaa wa pande mbili kwa maana ya Simba na Sportpesa kukaa mezani na kujadiliana na kuona namna ya kuboresha ama laah, na endapo wasipofikia makubaliano basi kupitia Mwenyekiti wa klabu ambao ndiyo wenye hisa 51 ndio wangetoa mwelekeo tena kwa utaratibu maalumu, lakini cha ajabu anaibuka mdhamini ambaye naye ni mshindani wa kibiashara na Sportpesa na kutoa kauli yenye dhihaka kitu ambacho hakitoi taswira nzuri kwa wadhamini wengine na kunaweza kuweka mazingira magumu kwa wadhamini wengine kuja kuwekeza kwenye klabu ya Simba.

Lakini kwa dhihaka ambazo Mo Dewji amezitoa kwa Sportpesa kwa udhamini wao je yeye ambaye ameendelea kutumia nembo ya Simba na kuweka matangazo yake kwenye jezi za Msimbazi kila kona, ameifaidisha klabu kwa kiasi gani?

Udhamini wa MO EXTRA na MO HALISI unatoa tija kiasi gani kwa Simba SC. Je kinachotolewa na SPORTPESA kinafanana na wanachokipata Simba SC kupitia hizo bidhaa mbili ambazo Mo Dewji anazitangaza kupitia na nembo na jezi za Simba SC?

Leo atoke hadharani atuambie kila bidhaa anayoitangaza kupitia Simba SC kwa mwaka klabu inafaidika vipi na wanapata kiasi gani na kipo wapi?

Vilevile Wanasimba na Watanzania wanatakiwa waelewe kuwa Mo Dewji na makampuni yao sio wenye dhamana ya uongozi.

Hii ni kwa sababu wakati wowote na kwa sababu yeyote wanaweza kujitoa Simba kuamua kuingia ubia na kampuni yeyote hivyo kutumia nafasi yake ya udhamini wa asilimia 49 na kujivika nafasi ya Simba SC ni kosa na kuidhalilisha klabu kwani inaonekana haina nguvu na ule umiliki wa asilimia 51 hauna kitu wala tija ilihali wametoka kuchagua mwenyekiti mpya hivi karibuni.

Kwa alichokifanya Mo Dewji leo, Je ni makubaliano baina ya makampuni yake na Simba?

Au ni utashi wake? Kama ni utashi wake maana yake hatambui mipaka yake na yule Mwenyekiti wa Simba aliyepewa dhamana ya kulinda umiliki wa asilimia 51 yupo kama picha tu.

Biashara ni makubaliano inapofikia mmeshindwa kukubaliana ni vema mkaachana kwa amani huku kila mmoja akilinda heshma yake na heshma ya upande wa pili.

Leo kuja kuidhihaki Sportpesa ni sawa na si uungwana yapo mengi wameyafanya kwa klabu ya Simba.

Hili swala si la kiushabiki ni vema wanasimba mkaanza kuona namna ambavyo klabu yenu inavyokwenda kutaifishwa na kuwa timu ya familia na niliandika hili.

Leo hii zile shilingi Bilioni 20 zimebaki hadithi isiyokwisha wala hasemi ataziweka lini?

Amebaki anaruka kama maharagwe ya Mbeya na kuanza kuchokonoa wadhamini wengine ambao wanafanya kazi na Simba huku mkataba ukiwa bado upo na kuonesha dhihaka na dharau.

Najua wenye uwelewa na mapenzi mema na Simba watakuwa wamenielewa ila wale wachumia tumbo vichawa vya Mo Dewji watatafuta majibu rahisi juu ya hili, lakini pia wanachama ni wakati wa kujitafakari huku mkihoji mwenyekiti wenu mmemchagua kwa kazi gani?

Njia niliyotumia kwenda ndio nitakayorudia

Msemakweli wa haki

NimemalizaView attachment 1732281
Mkuu hata kama hujui kusoma inamaana picha huoni? Hiyo sportspesa hata yanga wanayo jiulize yanga wamefikia wapi kimafanikio, nakuhakikishia bila Mo simba isingeachieve kile ilichonacho sasa
 
Wewe uoni Kama Sports pesa wanafukuzwa, MO hataki ushindani. yeye ndie mkurgenzi wa bodi na yeye ndie anaye miliki biashara zote zinazo husiana na timu.
Sportpesa wafike dau tu, kama watataka kutulipa pesa sawa na wanayowalipa Utopolo,bora waende tu.
 
Hivi mkishaandika mnapitia tena maandishi yenu, nyie wakati manji kajiuzulu si mligoma kufanya uchaguzi kila siku mnadanganyana anarudi.
Kwa sababu mwakalebela keshawajua ndio maana anawadanganya kamfungulia kesi Morison cas na nyie.mnabaki mkisubiria
Yaani huko Utopolo yamejaa mazezeta tupu
 
Back
Top Bottom