Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
"Mimi niwaambieni ukweli, nimechoka kuwabembeleza ,mkiniletea madiwani na wabunge wa kutoka upande mwingine(wapinzani), siwaletei maji na huu ndiyo ukweli sipendi kuwaficha, nimechoka kuwabembeleza"
Magufuli (1/Oktoba/2020, Tunduma)
Hisia za ubaguzi wa kimaendeleo zilianza mara tu Rais Magufuli alivyoapishwa mwaka 2015 ambapo majimbo, mikoa na nyanda zilizomnyima kura zikaonekana kutengwa kimakusudi katika mipango ya kimaendeleo na utekelezaji wa kibajeti. Kadri muda ulivyozidi kusogea hisia zikaanza kuonekana kuwa ni kweli baada ya JPM mwenye kukiri hivyo (kwa majivuno) wakati akifanya ziara za kitaifa.
Na sasa sio siri tena hii ni mojawapo ya sera yake rasmi ya kuombea kura katika uchaguzi huu mkuu 2020, maana karibu kila mahali ambapo CCM ilipoteza Ubunge mwaka 2015 amekuwa akirudia kuyasema hayo hayo.
Sina uhakika kama hii ni sera rasmi ya CCM au kama ipo kwenye ilani yake ya uchaguzi 2020, lakini kwa kuwa inasemwa na mwenyekiti wa CCM huku viongozi na wanachama wake wakikaa kimya au kushangilia ina maana ni sera ya CCM.
Nini mantiki ya Magufuli kuikumbatia sera ya ubaguzi wa kimaendeleo ?