Nini matatizo sugu ya mkoa wa Dar es Salaam?

Nini matatizo sugu ya mkoa wa Dar es Salaam?

ZINDAGI

JF-Expert Member
Joined
Dec 5, 2015
Posts
1,118
Reaction score
1,430
Sisi wakazi wa mkoa huu wa Darisalama na wageni wetu hebu tuorodheshe kero sugu zinazoukumba mkoa wetu huu ili kuwasaidia watatua kero wazisikie na kuzifanyia kazi.

Kwa kuwa hawawezi kufika ktk kila kona basi mimi na wewe ndio wawakilishi wazuri kuziorodhesha kero zetu.

1.Malori kuingia mtaani na kuharibu barabara
2.Njia mbovu
3.Mfumo wa maji taka
4.Garage bubu
5.Wizi wa magari na vifaa vya magari wakati wanunuzi wanajulikana
6.
7.
8
9.
10.

Haya tiririka ndugu
 
Hakuna kitu kinaudhi Kama uchafu na watu dar Ni wachafu Sana wanatupa taka hovyo
Uchafu umezidi sana siku hizi, na hii umechangiwa kwa kuvamiwa kwa jiji na baadhi ya wageni ambao sio wastaarabu
 
11. Mbanano wa kaya Kwamtogole
12. Taka kuachwa kandokando ya barabara hadi mwezi mzima
13. Madereva kutoheshimu vivuko vya waenda kwa miguu na hasa mitaa ya Kigogo hadi Mabibo
14. Madereva wa daladala kutotumia vema maegesho kwenye vituo na kufunga highway hasa Kimara Korogwe
15. Kelele za miziki kwenye makazi ya watu
16. Baadhi ya vibabu kutaka watoto wa shule
 
Madereva tumekuwa wengi sana kwa sababu ya magari automatic. Serikali ipige marufuku kuagiza magari automatic, yaagizwe manual tu!!
 
Madereva tumekuwa wengi sana kwa sababu ya magari automatic. Serikali ipige marufuku kuagiza magari automatic, yaagizwe manual tu!!
Magari sio mengi kiivyo sema barabara ni finyu na chache.
 
7. Kumwaga oil chafu chooni na kuachilia maji machafu ya chooni yenye oil chafu barabarani.

8. Majambazi

9. Mji hauna mfumo wa maji taka,, hivyo kulazimu watu kujenga mashimo ya kutunza maji machafu majumbani
 
Sisi wakazi wa mkoa huu wa Darisalama na wageni wetu hebu tuorodheshe kero sugu zinazoukumba mkoa wetu huu ili kuwasaidia watatua kero wazisikie na kuzifanyia kazi.

Kwa kuwa hawawezi kufika ktk kila kona basi mimi na wewe ndio wawakilishi wazuri kuziorodhesha kero zetu.

1.Malori kuingia mtaani na kuharibu barabara
2.Njia mbovu
3.Mfumo wa maji taka
4.Garage bubu
5.Wizi wa magari na vifaa vya magari wakati wanunuzi wanajulikana
6.
7.
8
9.
10.

Haya tiririka ndugu
Matatizo ya Dar
6. Wamachinga holela, mji hauna utaratibu
7. Kutopanga mji
8. Barabara hazina miundombinu ya maji
9.
10.
11.
 
Maji ....majiii yaaan dar maeneo mengi maji ni shida tena hasa maji safi na salama.Km sisi wana kigamboni maji kwa kweli ni mtihani mpaka bado tunatumia punda kubeba maji karne ya 21 ni aibu.
 
Back
Top Bottom