Nini mpango wa serikali kuthibiti hoja zenye kuleta mgawanyiko hasa kutoka kwa Zanzibar?

Nini mpango wa serikali kuthibiti hoja zenye kuleta mgawanyiko hasa kutoka kwa Zanzibar?

Best home tutor

Senior Member
Joined
May 8, 2026
Posts
194
Reaction score
268
Salama.
Imekua too much sasa maana imefika hatua haiwezi kuvumilika hasa kauli za viongozi kutoka Zanzibar

Mwanzo walisema wawafurushe watu wanaofanya kazi mahotelini ambao sio wazanzibar

Leo tena kama sio mzanzibar hautatibiwa bure

Sasa hizi kauli zisipothibitiwa zinaongeza uhasama na chuki au ndio maelekezo wamepewa ili wachochee chuki Muungano uwe rehani?

Huu mwendelezo wa hizi kauli sio mzuri ukizingatia hii ni Nchi moja.
 
Serikali ndiyo inawatuma, huelewi wapi?
 
Xenophobia ilianza kupitia hisia za Wazanzibari sasa zinageuka kwa kasi kuwa matendo. Upendeleo unaofanyika hivi sasa wa kugawa sawa kwa sawa wa rasilimali za nchi ndio unaowapa kiburi.

Wananufaika sana na uchache wao kulinganisha na wingi wa Watanganyika, na hivyo kuanza kuwadharau wazi wazi na hata kuthubutu kumuita kiongozi mkuu kimamlaka wa Kitanganyika Yuda msaliti.
 
Labda ndiyo msimamo wa serikali, kwanini mwakilishi na tena mteule aliyeteuliwa na rais sjui rais atoe kauli hizo bila uoga?
 
Hata CCM inajua fika watu huku grassroot sio Zanzibar sio Tanganyika hawautaki muungano.
Wameukinai Muungano ila CCM inalazimisha.
Huu ni Muungano wa kimabavu sio hiari za watu...
Ndio maana wakiambiwa ipigwe kura ya maoni ya kuendelea au kusalia ndani ya Muungano hawataki.
Mbona Scotland walifanya referendum, na waka vote kubaki UK.

Senegal na Gambia waliachana salama..Leo ni majirani wema tu.
Tena wote wale ni waislamu.
 
Back
Top Bottom