Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuoa:
Utafute m/ke.
Akukubali.
Umtolee mahari then umuoe!
...
Kujenga nyumba:
Uwe na kiwanja.
Uwe na hela ya kununulia vifaa, ya usafiri na hela ya fundi!
Then unajenga!
...
Nipe mantiki ya maswali yako.
sasa huu utakuwa muungano gani? nadhani hata nchi za wenzetu watahoji uwezo wa akili zetu tutakapokuwa tukijitambulisha kama united republic of tanzania. watahoja what is united kama kila nchi iko kivyake?
Hahahahahaaa!
Ivi kwa nini muungano wa Nchi za America ya juu wanajiita United States of America?
...
Ivi unajua kuna aina ngapi za Muungano?
mantiki ya maswali yangu ni kwa vile watu wanafikiri kuna jipya la kiuchumi litatokea kama tukiwa na serikali 2 au 3 kumbe ni vile vile tu.ukitaka maendelea fanya kazi jitume ,zalisha bizaa uza,au toa huduma, serikali tatu au mbili zitaongeza au kupunguza ajira ziszozidi 100 tu.
Kwaiyo wewe unahisi kukiwa na serikali 2, or 3 hakutakuwa na mabadiliko yoyote! Si ndio?
...
Kukiwa na serikali 3 kutakua na ushindani wa kimaendeleo btn Z,bar and Tg! Hiyo ni mzuri kwa maendeleo ya nchi!
...
Ndani ya serikali mbili hilo haliwezekani!
Kwa mfano Zanzibar inakopa or inagaiwa hela kutoka nchi jirani, hiyo hela inapigwa pasu kwanza na ukizingatia Zanzibar haina Benki inayotambulika kimataifa, hela yoyote ni kutoka nje kabla ya kufika Z,bar ni lazima ipitie BOT!
...
Wakiweka serikali tatu litatatulika hili na ushindani wa kimaendeleo utakuwepo!
Kilichopo sasa ivi ni WIZI MTUPU!
united states, wameunganisha na kufanya nchi moja na kuacha serikali za majimbo kwa ajili ya maendeleo ya jimbo na serikali ya majimbo hazitambuliki kimataifa wala kuwa na marais,n kama local govement tz,tuna serikali za wlaya kwa maendeleo ya milaya -tamisemi,lakini hazijiti nchi wala kutambulika hivyo nje na ndani. ndio tulichotaka na znz iwe hivyo.
Yap! Kwa ufafanuzi tu U.S.A ni federal state!
Kwa vile kuna aina mbili za muungano, Unitary (eg UK) na Federal (eg U.S.A na Nigeria) labda tu ujiulize huu Muungano wa Tz wa sasa unaingia wapi kati ya hizo mbili?
...
Serikali tatu itakua ni federal, ukumbuke hata huko U.S.A hawakuungana kwa vitu vyote! Na ushindani wa kimaendeleo upo sana ktk vile vijistates ambapo raisi wake wanamuita gavana! Ukumbuke hawa wanakua tu magavana ktk bunge kuu (cöngres) wakiwa ktk mabunge yao wanastand kama maraisi na wanapawa zote dhidi ya maeneo yao!
kama kweli tunataka muungano usio na kero ni serikali moja.muungano mwingine ni uswahili tu,tunajdhalilisha bure.
usidanganyie hicho kitu hakipo ni propaganda tu, mimi nimeishi tanganyika na zanzibar naelewa yote hayo wala hakutakuwa na ushindani unaofikiri wewe maana hakuna cha kushindaniwa.
pili kupitisha pesa bot hakuna effect yeyote hata kutuma pesa benki moja kwenda nyingine pesa hupita bot hiyo sio kwamba pesa inakatwa ni kuwasaidia wao kujua tu m kuzunguko, ziko pesa nyingi zinaingi kwa smz kutoka ulaya na nchi za kiarabu haziguswi hata za jamuhuri hupita bot, sasa kutokana na kupita huko ndio bot huweza kujua mzunguko wa pesa eneo fulani na gdp na mambo kama hayo.kwa hiyo bot kutolewa znz au kubaki haina signifikant beneft kwa tanganyika wala znz labda ni vi benk charges tu.
mashaxino hakutakuwa na ushindani wowote kimaendeleo maana mode of production kati ya zanzibar na tanganyika ni tofauti kabisa.
zanzibar wanalima karafuu na ,utalii na uvuvi, na bandari. sasa huko tanganyika bandari iko kubwa mno,utalii wa kilimanjaro pekee umeshavuka wa znz achana na mambuga mengine yote,uvuvi nao mkubwa kwanzia tanga mpaka mtwara.
sasa kwenye bandari ni kuwa tu znz soko lake ambalo ni tanganyika linaweza pungua kama serikali ya tanganyika itafanya kodi moja ya bizaa sawa na smz na huko haitakuwa tena ushindani na znz bali kukomeshana.
Mkuu kwa hili jaribu kufuatilia!
Ivi wewe unahisi Zanzibar kuja na hoja ya kutaka hela yao nje ya muungano imetokana na nini?
Mkuu naongelea ushindano wa kimaendeleo kwa mfano miundo mbinu, huduma za kijamii na ajira! Ukizingatia Zanzibar itakuwa huru kuchimba mafuta! Na sio ushindani wa kibiashara kutokana na hizo sababu ulizoziweka!