Nini mtazamo wako baada ya kurudi nyumbani?

Jamani,
Tunaposema Wabeba box haina maana kama mnavyofikiria..Huku majuu kazi zote za kuajiriwa tunaita kubeba box haina maana zaidi ya msemo tu.. sawa na Bongo mnaposema Walalahoi haina maana kila mtu asiye kiongozi ni Mlala hoi na alala hoi kweli!
 

Mkuu
Sio uhuni ni ushauri tuu hata hivyo bado nashawishika kuona hujasoma maelezo mengi na bado naamini umejibu kulingana na posts mbili ama moja ambazo nilikuwa wenda najibu hoja fulani.

Hoja yangu hapa toka awali nikuwa kama una kazi nzuri hapo marekani,ujerumani,uingereza n,k si busara kuicha kazi yako na kurudi nyumbani bali ninachosema ni kuwa hizo fedha zako zisaidie kule nyumbani kutengeneza kitu cha maendeleo kusomesha ama kujenga vyuo ama miundo mbinu n.k hii ni kutokana na mkono wako unapokomea.

Lakini kwa wezangu na mimi walio maliza masters Ukraine hawana kitu na uwezekano wa kupata kazi haupo kwanini ang'ang'anie kupigwa baridi huko?

Ukweli tuambiane ukweli na isichukuliwe kama dharau ama nini hata sisi tunaobeba Mabox tuyabebe tukiwa na malengo yalale na mtazamo ulele wa kwamba baada ya miaka kadhaa kazi hii nitastaafu ya kubeba box na nitakuwa nimejikusanyia kiasi kadhaa ili nikafanye kitu fulani nyumbani (labda kama wewe ni raia wa nchi hiyo hapa ni stori nyingine)ni ukweli usiopingika kuwa kazi ya mtulinga hawezi kudumu miaka mingi wewe na mimi ni binadamu itafikia mahala tuta kubali matokeo ya kwamba kazi hii hatuziwezi tena.

Narudia tena wewe kama una kazi hapo ulipo sikushauri kurudi unless unaenda Tz kama mwekezaji.Na wewe mwezangu na mimi kwanini uendelee kupigwa baridi ? Pesa unazitafuta ili zikusaidie sio kutafuta pesa ili uzisaidie.
 
YNIM,Mkandara,MkamaP,B-A-K,....

..nadhani kinachopaswa kufanyika ni MAANDALIZI.

..mtu usirudi kwa haraka na pupa, kama kawaida ya wengi walivyoondoka bongo.

..cha msingi ni kuwa na mahali pa kufikia na kuwa na uhakika wa mlo, na fedha ndogo-ndogo kama ya usafiri, matibabu, etc. baada ya hapo ndiyo unaweza kufikiria kuwa na mradi au biashara kubwa.

..kitu kingine ni kuepuka mashindano na pressure; kwamba wewe umetoka nje hivyo, unapaswa kuishi maisha ya aina fulani, na kuwa juu ya wale uliowaacha bongo.

..mwisho, test 'zali' kwanza. nimeshuhudia wa-Tanzania wanaorudi hatua kwa hatua.
 
Wajamani
Maana ya mbeba box.
Mimi ninavyoelewa na ninavyolitumia neno Mbeba box ni Mtu yeyote asiye Raia wa nchi husika anafanya kazi kiujanja ujanja mfano anajiandikisha yeye ni mwanafunzi ili apate kibali cha kuishi na kufanya kazi and the like ,Mara nyingi lakini si mara zote hatma ya mtu huyu ni tete tena kwa nchi kama uingereza mtu unaogopa hata kwenda kusalimia ndugu zako bongo maana ukienda tu wanaweza kugeuzia uwanja wa ndege.

Mtu mwenye nafasi.
Ni wale waliomaliza shule kwa bahati nzuri akaajiliwa ktk kampuni lamaana kwa kupitia kwake ikampatia haki zote za kufanya kazi.Ama kaajiliwa moja kwa moja kutoka TZ ktk makampuni husika ama ana uraia wa nchi husika.
 

Naamini tupo pamoja ila hatuelewani lugha.
 


Nadhani unafikiri box ni literally kubeba box tu.Kwangu mimi mtu akisema kupiga box ni hata pale anapofanya kazi ambayo si ya taaluma aliyosomea na mara nyingi ni blue color.
Kwa mfano wewe ni Daktari lakini unakosa kazi hospitali kwa kipindi kile wanakwambia ukalee wazee kwenye nursing home.
Na hata hivyo usiwadharau wabeba box na kuwataka warudi nyumbani,wengi wanatengeneza pesa nzuri tu.Inategemea akili yako katika kazi yoyote ile unayofanya na ndiyo mana mnaweza kupokea mshahara sawa kazini au wewe ukapokea kidogo lakini ukafanya mambo ya maana kuliko mwenzako.
Kwa mfano huo wa nursing home niliokupa Jamaa wanakula 12$ per hr huku ukivuta uzoefu na kuchakarika kutafuta kibarua cha taaluma yako.Je ni sawa na kwenda kutupwa hospitali ya wilaya Kigonsera kwenda kupiga mzigo 24/7 na kuambulia kamshahara kiduchu kasikokutoa hata katika matumizi yako mwenyewe kwa mwezi?Kuna wengine kwao kitu cha kwanza ni maslahi.Kama box linalipa kuliko kazi ya ofisini ya taaluma yake anaona bora apige box tu,sasa kwanini huyu naye useme 'wale wenzangu na mimi wabeba box turudi nyumbani'?
Halafu kuna swala la mazingira mazuri ya kazi na nafasi za kujiendeleza zaidi kielimu.Je huyo mbeba box unayemtaka arudi utampatia hizo nafasi na hiyo mikopo yenu ya mizengwe Chukulia kuwa huyo mbeba box ni form 4/6 leaver kwa mfano na pale alipo kama ana nia ya kusoma anaweza ku save 1000$ na kulipa community college na kuendelea kukata msuli huku akipiga box?
 
Jamani,
Tunaposema Wabeba box haina maana kama mnavyofikiria..Huku majuu kazi zote za kuajiriwa tunaita kubeba box haina maana zaidi ya msemo tu.. sawa na Bongo mnaposema Walalahoi haina maana kila mtu asiye kiongozi ni Mlala hoi na alala hoi kweli!
Wengine wanajua ni hasa kubeba mabox mabegani au zile kazi za kibega.......BTW wabeba box is a kind of Blue collar jobs thats all huitaji ujuzi husika kuweza kuifanya...

Tuendelee.......
 


Wazee mmeua!!
 

Mkuu
Mtazamo wangu ni kuwa, wanaotaka kutorudi wasirudi na zaidi wanaotaka kutoka watoke. Dunia ni kubwa sana, Watanzania wanahaki ya kukaa na kufanya kazi wanakotaka, cha msingi waridhie na wafurahie maisha. So if one decides to come back or opt not to go abroad, he/she is doing that at his/her own risk!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…