Nini mtazamo wako baada ya kurudi nyumbani?

Kurudi Tanzania inategemea umejiandaa vipi. Kama wewe ni mtoto wa kigogo, kuna opportunities nyingi tu na nzuri ambazo unaweza kuzipata kutokana na connections, kuna ujanja mwingi tu wa kuwakamua watanzania na ukawa na good life. Lakini kama wewe ni mtoto wa walala hoi na umesoma kwa jasho bila kulipiwa kwa hela za ufisadi, na kama huna connections na huko uliko una kibarua kizuri au hata kama sio kizuri ila kinakufanya uishi ni vyema ukabaki huko.
Huku uhalifu, kunyanyaswa, kupuuzwa, ufisadi, uonevu bado vipo na vinaendelea. Ukija tu kama ukija na kitu kwanza unaanza matatizo airport then yataendelea mpaka utajuta. Serikali za wenzetu zinajali watu bila kujali wao ni wageni au sio wageni, bila kujali wao ni wasomi au sio wasomi, maskini au matajiri una feel kabisa human dignity yako. Ukija huku ovyo utajuta sana na utatamani ungekuwa mbwa ughaibuni kuliko kuwa binadamu hapa. Haya ni maoni yangu tu, yanaweza yakawa na utata kwa wengine hasa wanaonufaika na nchi lakini kuna ukweli mwingi kwa niliyosema. Kama uko nje na unaendelea vizuri kaa huko huko, kama uko huko uko ovyo huku ni nyumbani rudi tu, lakini be ready.
 
Mimi naomba nitofautiane na wengi.
Maana ya kusoma na kuelimika ndiyo mategemeo ya serikali kwa wananchi wake,Hivyo serikali inatusomesha kwa namna moja ama nyingine ili tusiwe mzigo kwa serikali.Madhumuni ya serikali kutoka kwetu ni ili tuje tuwe JOB CREATER na sio matumaini ya serikali wewe msomi uje uwe JOB SEEKER

Hivyo basi kwangu mimi kurudi ama kutorudi nyumbani si hoja ,hoja ni je hapo ulipo utaitumia je kuwatenezea nafasi watanzania wengine ambao hawakuona elimu kama uliyonayo.Mfano mtu mwingine anaweza asirudi lakini akawatengenezea nafasi za ajira watanzania wanzake na mwingine akarudi akawa mzigo tu wa kugombania nafasi chache zilizopo .
japo natoka nje ya maada kidogo ningeomba tuangalie upya defination ya kuelimika na uzalendo.
 
Chukulia unatoka Ukraine umechoka na Masters yako mbuzi ya mkopo wa serikali ukarudi bongo.Huna mtu yeyote wa kukuunganisha kwenye system.Huo mtaji wa kuwatengenezea ajira watanzania utautoa wapi?
 
Swali zuri sana.
Hakuna mtaji mkubwa kama hiyo Masters yangu ya Ukraine ,ukilitambua hilo hutapata shida.Na hata hivyo kuwa na alternative ya kurudi ama kutorudi ni dalili tosha tayari huko uliko una kitu.

Kili kwanza hilo ama ukatae ili tupate mwelekeo sahihi.
 
Ndugu MkamaP heshima mbele,hili suala lina utata kidogo kwani uhalisia wakurudi nyumbani ukiwa hauna mtu wa kukupigia pande au kama wasemavyo wengi kama hauna ndugu fisadi au yupo kwenye nafasi nzuri ya kukuunganishia na hiyo Master ya Ukraine kazi ni ndoto.Mwishowe mtu utaishia kule kwetu uswahilini ukisubiria ngekewa ya kupata kazi bora nibaki huku nibebe hata boksi kuliko kwenda kuongeza mzigo na matatizo kwa familia uswahilini.
 
Nakuelewa mkubwa.
Unajuwa ni heri ukasote uswahilini kuliko kusota ukraine ama urusi teh teh teh teh.

Mkuu hata hivyo swali la mhusika nadhani limelenga zaidi ktk mtu mwenye nafasi huko aliko ama arudi nyumbani.Na ndiyo maana ktk maelezo yangu ya awali sijasema mtu arudi nimesisitiza ya kwamba kama ulipo bila kujali upo tz ama nje una uwezo wakutengenezea nafasi watanzania wezako ni swala la busara zaidi kubakia hapo ulipo.

Nakama uko huko juu ya mawe ni bora urudi bongo,bado naamini ukiwa na masters nzuri sio ya kuingia darasani mara mbili kwa week huko uliko tz kazi bado zipo.
 
Mtazamo wa wadau wengi ni kwamba bila kuwa na Uncle, Aunt, Jirani au Rafiki wa kukuwezesha na kukushika mkono life haitaenda, sasa ni kwa nini iwe hivi? Haiwezekani kwa mfano kwenda kuomba leseni bila kuzungushwa, kuunganishiwa umeme bila kuongea na vishoka, kuunganishiwa maji bila kujua mtu, kupata passport bila kumjua afisa uhamiaji?
Kuna correspondent wa NBC alikuwa anazunguka sehemu mbalimbali duniani mwaka jana kuangalia mazingira ya biashara na uwekezaji, alienda Hongkong incognito na kufungua biashara same day aliyotua, tena legally !! Je sisi tutafikia lini huko?
Sidhani pia kwamba lazima nije na mtaji na kuanzisha biashara ndiyo nitakuwa nimejenga nchi. Ninaweza kuja na idea [kama nina uzoefu na fani ya usafirishaji }za kuendesha kwa mfano TAZARA kwa ufanisi na kupata faida, au kulichukua shirika mfu la ATC na kulifanya liwe na wasifu wa kimataifa, kugeuza bandari na kuifanya iwe the best in Africa, kujenga barabara bila kusubiri wafadhili , kuzuia ujenzi holela wa makazi. Ninajenga nchi pia kwa kusomesha ndugu na jamaa, lakini kama nina uwezo zaidi wa kuchangia maendeleo ya nchi yangu, ni kwa nini nisifanye hivyo?
Kuna mdau pia ametoa wazo muhimu sana kwamba wengi waliosoma nje wanataka wakirudi tu nyumbani wapate u-bosi. Mimi nafikiri labda wanaona mambo hayaendi kama itakiwavyo na wanahoji, Sasa wanapokuwa wanahoji ndiyo hapo ngoma inaanza !!
 
Nakuunga mkono 100 kwa 100.
 
Mnaposema watanzania wanapomaliza shule nje wanapaswa kurudi nyumbani kujenga nchi hivi wakuu mnaamanisha mnachosema au mmekariri tu huo msemo?Hivi ukipata kazi nje hata isiwe nzuri sana lakini walau ukawa una save na kuwatumia kina mjomba na shangazi dola kadhaa kila mwezi ili wasomeshee watoto wao unakuwa hujengi nchi?Unakuwa siyo mzalendo mpaka nawe urudi ukanyanyaswe na mafisadi pamoja na taaluma yako safi?
Huko bongo tunasikia kila siku kuwa kazi ni za shida.Watu wanamaliza mlimani wanaendelea kula msoto,nyinyi mnasisitiza turudi.Sasa tukirudi wote patatosha hapo kweli?
Mimi nawashauri wabongo wote walioko nje kama una kazi ambayo inakuwezesha kusave na kufanya ka investment fulani bongo kama nyumba(for future)na kusaidia ndugu zako wala usikimbilie kurudi otherwise kama una godfather au baba ako fisadi fulani basi nenda manake uhakika wa kukamata kazi BOT unao!!

umeua mkuu!!!
 
Swali zuri sana.
Hakuna mtaji mkubwa kama hiyo Masters yangu ya Ukraine ,ukilitambua hilo hutapata shida.Na hata hivyo kuwa na alternative ya kurudi ama kutorudi ni dalili tosha tayari huko uliko una kitu.

Kili kwanza hilo ama ukatae ili tupate mwelekeo sahihi.

Sasa kama marekani unabeba box bongo utakuja kufanya kitu gani? Unaweza ukawa una kitu lakini bongo hakuna equivalent yake.
 
Kama unabeba mabox marekani na una kitu kidogo nafikiri kuendelea kukaa huko itakuwa hatari zaidi maana nguvu hizo za kubeba mabox itakwisha.

Lakini kama una kitu vitu vya kufanya bongo ni vingi mfano huko uliko nunua generator lako ,nunua misumeno ya umeme na randa zako za kutumia umeme,pia chukuwa gari yako cater ya bei rahisi naamini huko ni bei rahisi,shuka bongo chukuwa leseni yako pale mali asili nayo ni fedha kidogo nenda kule kahama ama iringa kakate miti ya bure Utashangaa kwanini ulikuwa mda wote unabeba mabox.

Ama hizo milion zako kadhaa nenda wilayani uwe unakopesha wafanyakazi wa halimashauri za wilaya yani ka (sacoss) na kwa asilimia kidogo pia utashangaa kwanini ulikuwa unabeba mabox.

Nakama unafedha tuseme una ml 100 Tsh unaweza kwenda kule wilayani ukawa unawajengea walimu nyumba ya m 1. Harafu kila mwezi wanakulipa kiasi fulani pia utashangaa kwanini uliendelea kubeba mabox.

teh teh teh teh Kazi inakuja tu pale unapokuwa na fikra za kuendeleza kazi yako uliyokuwa nayo huko us ili uje uindeleze TZ yani kubeba mabox.teh teh teh,kazi kweli kweli.

Ila kwa wasomi waliobobea ni shu nyingine.
 
Nakuelewa mkubwa.
Unajuwa ni heri ukasote uswahilini kuliko kusota ukraine ama urusi teh teh teh teh.

Mkuu hata hivyo swali la mhusika nadhani limelenga zaidi ktk mtu mwenye nafasi huko aliko ama arudi nyumbani.Na ndiyo maana ktk maelezo yangu ya awali sijasema mtu arudi nimesisitiza ya kwamba kama ulipo bila kujali upo tz ama nje una uwezo wakutengenezea nafasi watanzania wezako ni swala la busara zaidi kubakia hapo ulipo.

Nakama uko huko juu ya mawe ni bora urudi bongo,bado naamini ukiwa na masters nzuri sio ya kuingia darasani mara mbili kwa week huko uliko tz kazi bado zipo.

Kwanza ulizungumzia swala la kwenda kuwatengenezea ajira watanzania na si kwenda kugombea ajira chache zilizopo.Nilidhani labda ungeikomalia hii hoja yako lakini sasa naona umerudi palepale ukijiaminisha kuwa ukiwa na Masters basi bado kazi zipo tanzania.
Ndugu yangu kama nilivyosema mwanzo kurudi bongo lazima uwe na referee whether unataka kwenda kuajiriwa au kwenda kujiajiri mwenyewe.Unapowaza kwenda kuwatengenezea ajira watanzania wenzako in the first place lazima ujikite kwenye kujiajiri mwenyewe yaani manake ufungue ka biashara fulani,kampuni,uende ukajikite kwenye kilimo nk na hivyo vyote vinahitaji mtaji wa kuanzia.Ndiyo nikauliza-kama unatoka 'uchovuni' na huna mtu wa kukuonyesha njia,hiyo Masters yako utaitumiaje?
 
Mtazamo wa wadau wengi ni kwamba bila kuwa na Uncle, Aunt, Jirani au Rafiki wa kukuwezesha na kukushika mkono life haitaenda, sasa ni kwa nini iwe hivi? Haiwezekani kwa mfano kwenda kuomba leseni bila kuzungushwa, kuunganishiwa umeme bila kuongea na vishoka, kuunganishiwa maji bila kujua mtu, kupata passport bila kumjua afisa uhamiaji?
Kuna correspondent wa NBC alikuwa anazunguka sehemu mbalimbali duniani mwaka jana kuangalia mazingira ya biashara na uwekezaji, alienda Hongkong incognito na kufungua biashara same day aliyotua, tena legally !! Je sisi tutafikia lini huko?
Sidhani pia kwamba lazima nije na mtaji na kuanzisha biashara ndiyo nitakuwa nimejenga nchi. Ninaweza kuja na idea [kama nina uzoefu na fani ya usafirishaji }za kuendesha kwa mfano TAZARA kwa ufanisi na kupata faida, au kulichukua shirika mfu la ATC na kulifanya liwe na wasifu wa kimataifa, kugeuza bandari na kuifanya iwe the best in Africa, kujenga barabara bila kusubiri wafadhili , kuzuia ujenzi holela wa makazi. Ninajenga nchi pia kwa kusomesha ndugu na jamaa, lakini kama nina uwezo zaidi wa kuchangia maendeleo ya nchi yangu, ni kwa nini nisifanye hivyo?
Kuna mdau pia ametoa wazo muhimu sana kwamba wengi waliosoma nje wanataka wakirudi tu nyumbani wapate u-bosi. Mimi nafikiri labda wanaona mambo hayaendi kama itakiwavyo na wanahoji, Sasa wanapokuwa wanahoji ndiyo hapo ngoma inaanza !!

Mkuu hapo ndipo tunakuja kwenye swala lile lile la connection.Hayo mawazo yako ni mazuri lakini je ni nani atakayekupa hiyo nafasi?Unazungumza kwenda na mtaji wako siyo lazima halafu una mawazo wa kulichukua shirika mfu la ATC,sasa utalifufuaje bila kuwa na mtaji?
 
Kwanza ulizungumzia swala la kwenda kuwatengenezea ajira watanzania na si kwenda kugombea ajira chache zilizopo.Nilidhani labda ungeikomalia hii hoja yako lakini sasa naona umerudi palepale ukijiaminisha kuwa ukiwa na Masters basi bado kazi zipo tanzania.
Ndugu yangu kama nilivyosema mwanzo kurudi bongo lazima uwe na referee whether unataka kwenda kuajiriwa au kwenda kujiajiri mwenyewe.Unapowaza kwenda kuwatengenezea ajira watanzania wenzako in the first place lazima ujikite kwenye kujiajiri mwenyewe yaani manake ufungue ka biashara fulani,kampuni,uende ukajikite kwenye kilimo nk na hivyo vyote vinahitaji mtaji wa kuanzia.Ndiyo nikauliza-kama unatoka 'uchovuni' na huna mtu wa kukuonyesha njia,hiyo Masters yako utaitumiaje?

Nadhani aliongelea kwa nchi ambazo kupata kazi sio rahisi, na hauna hela ya kujianzishia biashara yako na kuwapa watu hizo kazi. Kwa hiyo ndio kasema kwamba ni bora urudi bongo na usote kidogo ila mwishowe utapata kazi. maana nina uhakika ukirudi Bongo utapata marafiki on the way na watakuwelea mambo sawa ili mradi uwe na skills za kuongea na watu. Simple as that. Yaani ni kwa nini uhangaike nje ya Tanzania wakati una masters? ni bora ukahangaike Bongo na siku unaweza kupata kazi (Na ukishapata ya kwanza unaweza ukaanza kutafuta nyingine.) Safari moja huanzisha nyingine.
 
Kwanza ulizungumzia swala la kwenda kuwatengenezea ajira watanzania na si kwenda kugombea ajira chache zilizopo.Nilidhani labda ungeikomalia hii hoja yako lakini sasa naona umerudi palepale ukijiaminisha kuwa ukiwa na Masters basi bado kazi zipo tanzania.
Ndugu yangu kama nilivyosema mwanzo kurudi bongo lazima uwe na referee whether unataka kwenda kuajiriwa au kwenda kujiajiri mwenyewe.Unapowaza kwenda kuwatengenezea ajira watanzania wenzako in the first place lazima ujikite kwenye kujiajiri mwenyewe yaani manake ufungue ka biashara fulani,kampuni,uende ukajikite kwenye kilimo nk na hivyo vyote vinahitaji mtaji wa kuanzia.Ndiyo nikauliza-kama unatoka 'uchovuni' na huna mtu wa kukuonyesha njia,hiyo Masters yako utaitumiaje?

Ndiyo mkuu.
Naamini unaweza kutengeneza ajira ukiwa ndani ya system ama nje ya system,kama huna kitu unaweza fanya kama mkuu mmoja aliyebainisha hapo juu,na hiyo ya kutengeneza ajira sio lazima urudi nyumbani unaweza ukawa hapo ulipo ukatengenezea ajira watanzania wengi .

Na hata hivyo bado nadhani falsafa ya kuelimika ni kutengenenza kisichokuwepo na kiwepo(yani huna kitu na kuweza kuwa nacho) kwa kutumia maarifa uliyoyapta
 
Personally nadhani kurudi na kuingia Serikalini ni mistake, lazima uende private sector. Pia kuna tofauti kama unarudi straight ukimaliza masomo na kurudi una experience sana, ukiwa una experience unaweza ukajikuta kazi za huku hazikuchalenge na hazipo as fulfilling.

Also a lot of times its who you know, not what you know.

this is one problem that young people hawataki kurudi nyumbani, na hawa young people are full of knowledge ambazo wanaenda kujenga nchi ya wenzetu. Tanzania need to change and the atitute of who you know, not what you know has to be destroyed! kama sivyo tutaendelea kuwa masikini milele
 
Kama unabeba mabox marekani na una kitu kidogo nafikiri kuendelea kukaa huko itakuwa hatari zaidi maana nguvu hizo za kubeba mabox itakwisha.

Lakini kama una kitu vitu vya kufanya bongo ni vingi mfano huko uliko nunua generator lako ,nunua misumeno ya umeme na randa zako za kutumia umeme,pia chukuwa gari yako cater ya bei rahisi naamini huko ni bei rahisi,shuka bongo chukuwa leseni yako pale mali asili nayo ni fedha kidogo nenda kule kahama ama iringa kakate miti ya bure Utashangaa kwanini ulikuwa mda wote unabeba mabox.

Ama hizo milion zako kadhaa nenda wilayani uwe unakopesha wafanyakazi wa halimashauri za wilaya yani ka (sacoss) na kwa asilimia kidogo pia utashangaa kwanini ulikuwa unabeba mabox.

Nakama unafedha tuseme una ml 100 Tsh unaweza kwenda kule wilayani ukawa unawajengea walimu nyumba ya m 1. Harafu kila mwezi wanakulipa kiasi fulani pia utashangaa kwanini uliendelea kubeba mabox.

teh teh teh teh Kazi inakuja tu pale unapokuwa na fikra za kuendeleza kazi yako uliyokuwa nayo huko us ili uje uindeleze TZ yani kubeba mabox.teh teh teh,kazi kweli kweli.

Ila kwa wasomi waliobobea ni shu nyingine.

Umefanya haya? Au unafanya consultancy ya bure kwa wananchi?
 
Kurudi Tanzania inategemea umejiandaa vipi. Kama wewe ni mtoto wa kigogo, kuna opportunities nyingi tu na nzuri ambazo unaweza kuzipata kutokana na connections, kuna ujanja mwingi tu wa kuwakamua watanzania na ukawa na good life. Lakini kama wewe ni mtoto wa walala hoi na umesoma kwa jasho bila kulipiwa kwa hela za ufisadi, na kama huna connections na huko uliko una kibarua kizuri au hata kama sio kizuri ila kinakufanya uishi ni vyema ukabaki huko.
Huku uhalifu, kunyanyaswa, kupuuzwa, ufisadi, uonevu bado vipo na vinaendelea. Ukija tu kama ukija na kitu kwanza unaanza matatizo airport then yataendelea mpaka utajuta. Serikali za wenzetu zinajali watu bila kujali wao ni wageni au sio wageni, bila kujali wao ni wasomi au sio wasomi, maskini au matajiri una feel kabisa human dignity yako. Ukija huku ovyo utajuta sana na utatamani ungekuwa mbwa ughaibuni kuliko kuwa binadamu hapa. Haya ni maoni yangu tu, yanaweza yakawa na utata kwa wengine hasa wanaonufaika na nchi lakini kuna ukweli mwingi kwa niliyosema. Kama uko nje na unaendelea vizuri kaa huko huko, kama uko huko uko ovyo huku ni nyumbani rudi tu, lakini be ready.

Naam karaha na maudhi ya bongo, uliyoyaandika ni kweli tupu. Pia kuna matatizo ya maji na umeme yasiyokwisha miaka nenda miaka rudi. Sasa hivi makusanyo ya kodi yameongezeka mno lakini cha kushangaza baadhi ya mapato hayo hayaelekezwi katika kumaliza kabisa matatizo ya upatikanaji maji safi na umeme Dar na mikoa mingine. Si kitu cha kushangaza kusikia jiji la Dar halina umeme au maji kwa wiki au hata zaidi.

Pia unaomba mungu usiugue maana ikibidi kulazwa unaweza ukaambiwa ulale sakafuni au kupewa godoro lililo chafu mpaka linatisha hata kuliangalia tu achilia mbali kuweka kiwili wili chako. Pia unaweza ukakwaa gonjwa lingine hapo hospitali zaidi ya ule uliosababisha ulazwe. Nakumbuka jamaa yangu alinihadithia alipokuwa anaondoka bongo yeye na mkewe kurudi maskani yao, wakati wako ndani ya ndege mume akamwambia mkewe nashukuru kweli tunaondoka salama akamwambia hata mimi nashukuru sana. Mume akamuuliza unajua nashukuru nini? akamwambia kwamba mungu katujalia wote na watoto hatukuugua. Mume akamwambia hilo ndilo nililokuwa nashukuru.

Hawa vingunge kila siku wanapokutana na Watanzania wanaoishi nchi za nje hutoa ahadi za "Tunaweka mazingira mazuri ili mvutiwe na kuamua kurudi nyumbani." lakini miaka nenda miaka rudi hakuna lolote linalofanywa na hizo ahadi zao bado zinazidi kutolewa kila wanapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Kama umeamua kurudi bongo jiandae kikamilifu pia usifikirie tu kuajiriwa bali fikiria pia kujiajiri mwenyewe hili linahitaji mtaji mkubwa na mafanikio yapo kama ukiamua kujituma kwa juhudi zako zote.
 
Umefanya haya? Au unafanya consultancy ya bure kwa wananchi?

Ni consultancy ya bure tu ,Na mimi binafsi bado naamini tanzania ni nchi wenda pekee ambayo ina fursa nyingi sana za kujikwamuwa hasa kwa watu ambao tayari wanavijimilio vya ma box.

Tatizo kubwa kwa Tz ni mwananchi wa kawaida fursa anaziona zilee lakini kwake elfu hamsini tu yani dola 40 ni hajawahi kuzikamata mkononi karne kadhaa.

Mfano wewe unaji vimilioni vya mabox ukienda pale Nzega kuanzia mwezi wa tano utakusanya mpunga kutoka kwa mkulima kwa bei ya bure sasa ashumu umenunua zile mashine za kukoboa kubwa kubwa ,basi ikifika mwezi wa nane unaanza kukoboa unazipaki ktk vijimifuko kuanzia kilo moja hadi 20 unauza sehemu wanapohitaji utafaidika mno tofauti nakuendelea kubeba mabox.
 
Naam karaha na maudhi ya bongo, uliyoyaandika ni kweli tupu. Pia kuna matatizo ya maji na umeme yasiyokwisha miaka nenda miaka rudi. Sasa hivi makusanyo ya kodi yameongezeka mno lakini cha kushangaza baadhi ya mapato hayo hayaelekezwi katika kumaliza kabisa matatizo ya upatikanaji maji safi na umeme Dar na mikoa mingine. Si kitu cha kushangaza kusikia jiji la Dar halina umeme au maji kwa wiki au hata zaidi.

Pia unaomba mungu usiugue maana ikibidi kulazwa unaweza ukaambiwa ulale sakafuni au kupewa godoro lililo chafu mpaka linatisha hata kuliangalia tu achilia mbali kuweka kiwili wili chako. Pia unaweza ukakwaa gonjwa lingine hapo hospitali zaidi ya ule uliosababisha ulazwe. Nakumbuka jamaa yangu alinihadithia alipokuwa anaondoka bongo yeye na mkewe kurudi maskani yao, wakati wako ndani ya ndege mume akamwambia mkewe nashukuru kweli tunaondoka salama akamwambia hata mimi nashukuru sana. Mume akamuuliza unajua nashukuru nini? akamwambia kwamba mungu katujalia wote na watoto hatukuugua. Mume akamwambia hilo ndilo nililokuwa nashukuru.

Hawa vingunge kila siku wanapokutana na Watanzania wanaoishi nchi za nje hutoa ahadi za "Tunaweka mazingira mazuri ili mvutiwe na kuamua kurudi nyumbani." lakini miaka nenda miaka rudi hakuna lolote linalofanywa na hizo ahadi zao bado zinazidi kutolewa kila wanapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Kama umeamua kurudi bongo jiandae kikamilifu pia usifikirie tu kuajiriwa bali fikiria pia kujiajiri mwenyewe hili linahitaji mtaji mkubwa na mafanikio yapo kama ukiamua kujituma kwa juhudi zako zote.

Mkuu heshima yako.
Mimi bado naamini jukumu la kurekebisha hayo yote ni jukumu letu sote si jukumu la serikali tu.

Pia kujituma,ubunifu kama ulivyo nena ndiyo siri ya mafanikio mtu akiamuwa kujituma bongo kama anavyojituma kubeba ma box kwa kulala saa mbili masaa 22 yuko kazini basi Hakuna sehemu yoyote atakayopata mafanikio makubwa tofauti na Tanzania.
 
Back
Top Bottom