The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
Wanasubiri tufungue accounts za benki kwao (Ulaya) ili siku moja watwambie fanyeni hiki, fanyeni kile, vinginevyo tunawafungia. Sisi hatujali… Hatuna accounts huko na hatuhitaji kuwa na accounts… Hatuna chochote huko na haitokaa itokee tukamiliki chochote huko.
Kila tunachokifanya ni kwa ajili ya Burkina Faso. Sisi hatuhitaji hata kutoka nje ya Burkina Faso yetu. Tuna amani hapa… Tukihitaji kwenda kutalii nje ya nchi, tutakwenda Bamako (Mali), Niamey (Niger) au miji mingine… Hatuna sababu ya kwenda huko kwao… Tupo vizuri hapa kwetu.
Kuhusu uoga, hatuna uoga… Tunafahamu athari zinazotuzunguka… Tumeamua kulitumikia taifa letu, tume-sacrifice maisha yetu kwa taifa hili Kwa nini tuwe waoga? Tumeweka kando ujana wetu, kwa lengo la kulitumikia taifa, kwa hiyo hatuna uoga wowote, ondoeni shaka!… Uoga sifuri.