Nini mtazamo wako juu ya kauli ya Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso?

Mnachotafsiri ni huko kujiondoa kwenye hao wanaoweka vikwazo hata mashoga wao wakikataliwa, kama alivyowekewa Zimbabwe hadi leo. Hao wakubwa wana 'values' zao wanazotaka ku-'impose' kwa nchi zingine.
Why kila kitu mnaingiza ushoga, kwamba kufanya biashara na western countries ndio ushoga? Unadai Zimbabwe waliwekewa vikwazo kisa ushoga unasahau Tanzania tulinyimwa pesa za MCC kisa..... uchaguzi mbovu wa 2015!! So unafanya cherry picking ili kufit narrative.
 
Maneno ya aina hii hapa kwetu sijui tunayaandika tukiwa na maana gani hasa!
At least bongo on paper mtu anaweza hata ripotiwa na CAG na bunge likiamua kukomaa kama enzi za Sitta basi anachukuliwa hatua. Sasa huko Burkina Faso wanajeshi wanachukua tu pesa kwenye akaunti za mashirika ya umma na hakuna wa kuwahoji maana serikali yao haiwajibiki kwa bunge au mahakama wao ndio kila kitu.
 
Maneno tu hayo ushujaa kwenye njaa hahudumu ni swala la muda..
 
Kama kauli yake imetoka moyoni na sio kututia Moyo Wafrika basi ni jasiri kama akina Nkrumah na Mandela hizi ndizo zilikuwa sera zao kuwa Wafrika ifike siku moja tujitawala na Kujiongoza kwa kila kitu.
Mie binafsi namuunga mkono
Mandela ? Hivi katika list unamuweka Mandela kama angekuwa ni MJAPANI angeuliwa
GADAFI IDDI AMINI MUGABE MAGUFURI NYERERE LUMUMBA hao kwangu ndio wazarendo wa kweli wa AFRCA ambao hawakutaka na hawakuwahi kulamba MIGUU ya mabeberu
Huyo DOGO kama aloyasema ni kutoka moyoni basi anafuata NYAYO za hai miamba
 
Aliingia madarakani September 22, hii taarifa ni ya February 23, inawezekana iliandaliwa wakati wa utawala wa kabla yake. Acha porojo.
 

..hapana, anamzungumzia Shujaa aliyekuwa akiishi kwa msaada wa kidubwasha kwenye moyo kilichotengenezwa na wazungu / mabeberu.
 
Nayajuwa yote hayo mkuu 'zitto jr', asante kwa kuyataja . Huo mfano wa 'ushoga' ndio unaoonyesha ujinga mkubwa sana wa hao watu wanaotaka ku'impose values' zao kwa wengine. Itakuwa ni mjinga tu asiyeweza kuelewa mfano kama huo.
Zimbabwe ni mfano mzuri sana katika ujinga wa hao wazungu. Pamoja na kwamba msukumo wa kuwekewa vikwazo ulihusiana na walowezi, ndugu zao, lakini vikwazo hivyo vilikolezwa zaidi Mugabe alipokomaa kuhusu ushoga, au hukumbuki?
Leo hii Mugabe alisha ondoka, lakini Zimbabwe bado ipo kwenye vikwazo pamoja na kujtafuta 'favor alikokufanya Mnangwaga aliposhika madaraka. Zimbabwe wanahatarisha maslahi yapi ya hao watu hadi raia waadhibiwe kwa vikwazo visivyo koma.

Tanzania na "uchaguzi wa 2015"? Mkuu 'zitto jr.' hapa ndipo huwa napata mashaka juu ya ukomavu juu ya mambo haya. Baada ya uchaguzi huo Magufuli angejipeleka kwa hao watu unadhani hiyo hela ingeacha kutolewa? Ni kiburi tu cha Magufuli ndicho kilicho sababisha hela isitolewe. Ni madikteta wangapi duniani wamefaidika kutoka kwa hao hao, kwa kulinda maslahi yao?
 
Mambo ya kizamani hayo, “live your life and do the right thing “. Haya maneno nimeyasikia tangu nakua na sasa uzee unakuja na waumiaji ni sisi walala hoi.

Wanaishi ikulu kila kitu bure ndiyo maana wanaongea huu upuuzi. Waende kuishi Manzese ndiyo waseme hivyo.

Kukicha bakuli wanaanza kutembeza huko huko
 
Dua la kuku.
Afrika inaumizwa na demokrasia ya magharibi.
 
Binadamu huwa tunategemeana vivyo hivyo mataifa yanategemena, ila inapifika mahala baadhi ya mataifa kujiona wao ndio bora kuliko wengine na bila wao wengine hawatoboi na kuanza kujiona kama vile mataifa yao ni pepo hapo ndipo napongeza msimamo wa Ibrahim Traore.

Mimi binafsi huwa sipendi tabia ya kujipendekeza na vijitabia vya uwizi. Kuna faida gani ya kwenda kuweka hela kwenye account huko ulaya wakati nchini kwako kuna benki, kuna sababu zipi za kwenda kushangaa mamiundombinu huko ulaya wakati na sisi tunaweza kujenga. Traore ni kijana mwenye akili sana Mungu hamlinde maana kuwa mzalendo kuna gharama kubwa na mara nyingi utapewa majina mabaya ili wakuloge.

Africa hasa viongozi no ngumu sana kuwaelewa, sijui akili zetu nani kaondoka nazo au kazifunga. Miaka nenda rudi hapo Congo vita vita haiishi na watu wanauwawa lakini wameshindwa kuungana kupeleka jeshi likawafute hao waasi, hivi kweli waasi wanapata nguvu ya kupigana na serikali muda wote huo na AU wapo tu.
 
Unataka uongozi utambulike kwako? We kama nani hasa, akili kama hizi bado zinaishi ni ajabu sana
 
Hawa ndio viongozi tunao wataka, pelekeni democracia yenu huko acheni kucheza na hisia za wanachi, muda wote mnawaza vyeo tu kupitia democracia badala yakuendeleza nchi. Mnafanananisha democracia ya Africa ni lazima ifanane na ya Ulaya. Africa ili itoke hapa ilipo hahihitaji democracia ya kuachian madaraka inahitaji kiongozi mzalendo atawale haijalishi kaingiaje na atakaa muda gani. Na ukiona kiongozi anachukiwa na wanasiasa halafu anapendwa na wananchi huyo ndio anafaa.
 
Dua la kuku.
Afrika inaumizwa na demokrasia ya magharibi.

Umeelewa hata nilichokiandika kweli?

Nnachosema uchoyo, ulafi, uchu wa Madaraka na kukosa uzalendo wa kweli ndio kinachotumaliza wa Afrika. Hapo sijataja usimamizi mbaya na kukosa mipango na uongozi.

Wakati yeye anajitahidi kuipigania nchi yake Kwa dhati, maadui watawatumia wenzake wa nchi hiyo hiyo kufanya utawala wake uwe mgumu na ikiwezekana atolewe madarakani.
 
Role model ni Magufuli!
 
Si muda mrefu sisi wenyewe tutashirikiana na wazungu kwa kupewa vipande vya fedha ili kumuua mzalendo kama huyu. Yameshawahi kutokea nchi fulani.
 
Anachonishangaza anatumia lugha ya Kifaransa kuwasiliana na hadhira yake, kama kweli amejinasua na makucha ya mabeberu kwanini asizungumze kwa Kiburkinabe?

Anachonishangaza anatumia lugha ya Kifaransa kuwasiliana na hadhira yake, kama kweli amejinasua na makucha ya mabeberu kwanini asizungumze kwa Kiburkinabe?
Wewe kichwani hazimo hakuna lugha inaitwa ya kiburkinabe Burkina Faso Wana tofauti za makabila 66 kifaransa ndio lugha inayowaunganisha wote
Pili ujue hakuna nchi duniani yenye hati miliki ya Lugha ndio maana kiingereza kinatumika nchi nyingi duniani kama lugha

Hata Kiswahili hakuna nchi yenye hati miliki nacho ndio maana unakuta Kenya,Congo ,Uganda kiswahili kipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…