Nini mtazamo wako juu ya kauli ya Ibrahim Traoré, Rais wa Burkina Faso?

Taarifa ya rushwa unaipata kutoka kwa wakoloni,(western media), hahaha,kalaghabaho
 
Anachonishangaza anatumia lugha ya Kifaransa kuwasiliana na hadhira yake, kama kweli amejinasua na makucha ya mabeberu kwanini asizungumze kwa Kiburkinabe?
Taarifa anayoitoa wakusudiwa ni hao wakoloni,(ufaransa),kwa kutulia
 
Kama kauli yake imetoka moyoni na sio kututia Moyo Wafrika basi ni jasiri kama akina Nkrumah na Mandela hizi ndizo zilikuwa sera zao kuwa Wafrika ifike siku moja tujitawala na Kujiongoza kwa kila kitu.
Mie binafsi namuunga mkono
Mandela
Kama kauli yake imetoka moyoni na sio kututia Moyo Wafrika basi ni jasiri kama akina Nkrumah na Mandela hizi ndizo zilikuwa sera zao kuwa Wafrika ifike siku moja tujitawala na Kujiongoza kwa kila kitu.
Mie binafsi namuunga mkono
Mandela mtoe kwenye hili kundi .. at last he dropped the struggle, surrendered and used by white monopoly.
 
kama huu ndio mtazamo wa expert member kazi ipo .. Una maono hafifu mkuu katika siasa za Africa na Pan Africanism
 
Chura wa Tanzania anasemaje?
 
Alishafeli huyo kiuchumi, Kuna vitu kama kiongozi wa nchi hutakiwi kuviongea hata kama una chuki na mabepari Kwa kiasi gani. wewe tekeleza kimya kimya maono yako bila kumnanga mtu Kwa sababu katika njia ya kuliinua taifa na watu wake utawahitaji wote hata wale waliokuumiza hapo mwanzo ili mradi tu unawatumia Kwa manufaa ya watu wako.

Kwa Sasa njia ya kujichomoa kutoka umaskini Kwa nchi zetu ambazo ni masoko ya wakubwa ni ngumu na haihitaji watu kama yeye bali ni wanafiki huku unajua wapi unataka kuwafikisha watu wako ama sivyo ataishi Kwa hofu kama digidigi
 
Yupo sahihi, Venezuela walihufadhi dhahabu zao Uk Nini kimetokea wametaifisha. Na sisi kwa sababu tuna viongozi vilaza tumeenda kuhifadhi huko huko.
 
Kabisa unajiona upo logical
Kwani kabla yake Burkina Faso haikuwahi kupinduliwa. Kilichotokea ni nini?

Kama mapinduzi yangekuwa ndio maendeleo Afrika ingekuwa inagawa misaada Ulaya. Sudan wana mapinduzi kuliko nchi zote Afrika na ni njaa kali Tanzania inawapita mbali.
 
Huyo Traore ana IQ ndogo na utoto huku akisindikizwa na sifa za kijinga. Hajui diplomasia kabisa.

Japan ilipigwa na Marekani kwenye WW2 na hadi mabomu ya kinyuklia. Immediately Japan imetoka vitani ikashirikiana na Marekani na mataifa makubwa kuinuka kiuchumi. Haikujifanya ina chuki na kujinunisha.

Ujerumani ilileta WW2 ikapigwa na kuingia hasara kubwa na kuleta hasara kwa wengine. Immediately vita imeisha ikagawanyika na kila upande ukapata support yake, baadae ikaungana. Hukusikia eti USSR haifanyi biashara na Ujerumani kisa iliua watu wake zaidi ya milioni 20 kwenye vita.

Sasa huyu Traore hata hajui soko la dunia, investors na watalii wanatoka wapi. Yeye anakariri kwamba wote ni "mabeberu". Alafu mtu anategemea maajabu hapo. Ngojeni muone kama ataambulia lolote mtu mwenye akili fupi vile. Tangu lini maskini jeuri akafanikiwa.

Mnyonge ili afanikiwe anabidi awe mnafiki. Sio kuleta ujuaji wa kijinga na kujitutumua wakati GDP yenyewe ni sawa na biashara ya kuzoa taka nchi nyingine.
 
Hayo maneno kayasema wapi kama hujitungii tu stori za kufurahisha kichwa chako! Wewe umeweka tafsiri yako ambayo ni potofu.
Aliyoyasema ni yapi, maana inaonekana unayajua yote na haya niliyoandika hapa sio maneno yake.
 
Unaonaje ukaacha kutumia teknojia za hao unaoita mashoga ili kuungana kauli na Traore na uungane na Urusi ambao sio mashoga na sio mabeberu.

Uanze kutumia gari za Lada ambazo hata ukute hujawahi kuziona, uondoke JF maana haina teknolojia ya Mrusi hii ni ya Mmarekani ambaye kwako ni shoga. Uachane na internet, uachane na banking system, uachane na kupanda ndege Tanzania hij hakuna ndege ya Mrusi kuna za unaoita mashoga.

Ili umaanishe Traore yuko sahihi inabidi tusikuone humu, uanze kujitenga kama anavyotaka kuitenga nchi yake. Ama ukubali wewe ni shoga ndio maana umeweza access huduma za unaoita mashoga.
 
Mandela yupi angekuwa Japan angenyongwa??

Emperor Hirohito kaongoza Japan kwenye WW2. Ikapigwa vibaya na Marekani hadi akatangaza kushindwa vita kwenye redio ya taifa jambo ambalo ni la aibu kwa tamaduni za Japan hadi majenerali wengine wakajiua. Hapo hapo Hirohito akakaribisha Wamarekani wafanye uwekezaji, wainue uchumi walioshiriki kuuua na kukuza sekta mbalimbali.

Aliyofanya Emperor Hirohito ni ya ajabu zaidi ya Mandela alafu unadai Mandela angenyongwa Japan, mbona Hirohito yuko respected kwa maamuzi yake. Nchi haziendeshwi kama chama cha VICOBA kwamba mtu asipolipa wanamvalia dela kwenda kumsuta.
Njaa haina baunsa, muache Traore ajifungie tumuone.
 
Kauli ya uoga hiyo kwa sisi wasomi ndo tumeelewa. Ukianza kusema nyumbani kwamba mimi ndo mwanaume hakuna mwanaume mwingine ujue unakaribia kufa. Hata Gadafi au jpm walianza hivyo hivyo kuuwadis wazunu mwisho ikabaki story
 
Taarifa ya rushwa unaipata kutoka kwa wakoloni,(western media), hahaha,kalaghabaho
Si ajabu hiyo taarifa hapo ameiotoa huko kwenye viwebsite uchwara ambavyo ukichunguza zaidi zimeandikwa na diaspora wale ambao wameikimbia nchi baada ya Traore kuingia madarakani..... na siku zote habari za kuwachafua hawa viongozi wanaonesha kuwa ni Pan-Africanist huwa zinaenea kwa kasi sana.

Usitegemee huyo mpenda demokrasia uchwara(afrika hatuna demokrasia bali tuna mwamvuli tu wa demokrasia) aone kama kuna jema kutoka kwa Traore.
 
Huyu ndio aina ya viongozi ambao hili Afrika isonge mbele inawahitaji.

-Muadilifu
-Shupavu
-Jasiri
-Mzalendo
-Mwenye maarifa.

Na sio viongozi washenzi walamba makalio ya wazungu, wanaoijifanya wapenda demokrasia halafu hata uzalendo wenyewe hawana na wanatumia mwamvuli wa diplomasia kuuza na kufanya udalali wa rasilimali za nchi.

Binafsi nawachukia sana hawa viongozi wanaojinasibu ni wana demokrasia kumbe ni majizi wakubwa.
 
Si muda mrefu sisi wenyewe tutashirikiana na wazungu kwa kupewa vipande vya fedha ili kumuua mzalendo kama huyu. Yameshawahi kutokea nchi fulani.
Na hapo ndipo hao wazungu wanapokuja kuthibitisha kuwa wafrika akili zao ni duni sana na hawajui kiongozi sahihi ni yupi wanapenda kuongozwa na vibaraka.
 
Afrika inahitaji vijana wenye mtazamo wa aina hii. Na siyo kama hizi takataka za kwetu zilizoamua kujiita majina ya wadudu wachafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…