Nini nifanye niweze kusahau makosa niliyofanya kwa kujitakia yanayonihukumu kila siku?

Nini nifanye niweze kusahau makosa niliyofanya kwa kujitakia yanayonihukumu kila siku?

Saint_Mwakyoma

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2019
Posts
865
Reaction score
1,208
Kwa miaka sasa ninatumia nguvu kubwa kutumia njia mbali mbali japo tu, nisahau makosa yangu yaliyo haribu njia ya maisha yangu lakini naishia kupata ahueni kwa muda tu na baadaye najikuta niko na yale maumivu.

Wakuu nisaidieni mbinu mbadala mlizotumia kusahau makosa yenu kwenye safari zenu za maisha.

" Let go of what was Accept what is Have faith in what will be"
 
Hii ni njia nziri ya kufanya reflection, rudisha mawazo nyuma na ujiulize ungefanya nini ingekua ni wakati huu. Kubali maumivu na uiambie akili yako kamwe hutarudia makosa yale tena.

Tunaishi leo hatuishi jana. Unaweza kuifanya leo iwe bora na kesho bora zaidi lakini huwezi kuifanya jana iwe bora.
 
Hii ni njia nziri ya kufanya reflection, rudisha mawazo nyuma na ujiulize ungefanya nini ingekua ni wakati huu. Kubali maumivu na hutarudia makosa yale tena.

Nielee kidogo zaidi mkuu kwaio ni Kama meditation au
 
Sasa bila Kutwambia Makosa gani Uliyofanya ...Unafikiri tutakuwa na njia bora ya kukushauri ?

Yaani tutakuwa tuna 'guess' Kwa mfano ... labda ulivunja glasi ya maji ambayo unachotakiwa

kufanya ni kufagia vipande vilivyovunjika na kuvitupa mbali halafu unanunua nyingine
maisha yanaendelea.

Kwa hiyo embu funguka ..Tukushauri cha Kufanya..!
 
Upe muda wakati .. Kwa nguvu yako mwenyewe hutaweza.

Fanya michakato ya kuomba radhi kama kuna uliowakosea kati ya hayo.. Anza kuishi positive.

Tumia tiba ya chumvi itakusaidia kukupa amani na utulivu
 
Sasa bila Kutwambia Makosa gani Uliyofanya ...Unafikiri tutakuwa na njia bora ya kukushauri ?

Yaani tutakuwa tuna 'guess' Kwa mfano ... labda ulivunja glasi ya maji ambayo unachotakiwa
kufanya ni kufagia vipande vilivyovunjika na kuvitupa mbali halafu unanunua nyingine
maisha yanaendelea.

Kwa hiyo embu funguka ..Tukushauri cha Kufanya..!
Mkuu nipo guilty kupitiliza mkuu inawaza kunicost kimaisha
 
Asante mkuu......tiba ya chumvi inauzwa wapi msaada tafadhali
 
Asante Sana nitalifanyia kazi
 
Mkuu nipo guilty kupitiliza mkuu inawaza kunicost kimaisha
Taja hayo makosa uliyofanya ili upate ushauri mzuri zaidi. Kama ulifanya jinai kubwa mfano kuua, kubaka, nk. basi ni vizuri ukajisalimisha kituo chochote cha polisi ili sheria ifuate mkondo wake.

Baada ya kuhukumiwa, naamini utapata wasaa mzuri wa kujutia hayo makosa yako huko gerezani, na mwisho utarudi katika hali yako ya kawaida. Kinyume na hapo, utaishi maisha ya majuto mpaka kifo.
 
Ulishaungama mara ngapi hizo dhambi zako kwa dhati mbele za Mungu wako, au hujui hakuna lisilowezekana kwa Mungu?

Mungu akishakusamehe tayari inatosha, lakini nawe pia uwe mwaminifu sana kitabia ili uruhusu Roho Mtakatifu awe ndani ya hekalu lake(mwilini mwako) akiwa Mshauri wa ajabu na Kiongozi bora katika maisha yako yote.
 
Hivyo unavyofanya kusahau kwa muda, fanya kutwa mara tatu kila siku. Au kubali tu ilishatokea na huwezi badilisha, maisha yasonge kama ulivyonukuu hapo mwisho.
 
Back
Top Bottom