Katika hali yoyote ile ze utamu ife kabisa!! Ninachosikitika sana ni kwa kuwa ni wengi wameumizwa sana na hiyo website lakini hakuna lilifofanyika. Ninachofahamu usalama wa taifa una kila idara, sasa hiyo idara ya IT ilikuwa haipitii ze utamu ikaona maporomoko hayo na kuyafanyia kazi au nao walikuwa wanapita huko na kujichekea au kujifunza style za ngono na kuona miili ya watoto, marafiki, ndugu na majirani ikisanifiwa katika photoshops? na kubandikwa pale na mtu anaamini ni kweli. Ni vigumu kumwelimisha mke/mume/fiancee/gilrfriend/boyfriend/hawara kuwa picha iliyopo si halisi bali ni ya kuengeneza kama ile ya mkuu wa kaya!!! Maumivu mengi yameipata jamii!!!
Sasa basi na hili ni fundisho kwa serikali kuwa wanatakiwa kuwa makini na kufuatilia immorals hata kama ni za maskini wa kawaida na watu wa class ya chini, sasa hao walioko juu wakiguswa tu mara hili mara lie.
Sasa basi ze utamu itarudi kwa jina lingine na mambo yale yale. Owners wanajipanga, ule ni mtandao, wa owners ambao hawalali wanapanga mipango mathubuti. Sasa sisi wabongo tunajituma kiasi gani watumishi wa serikali ili basi tuweze kupambana na ze utamu, hatuwawezi!!! Kama kupeleka tu basic human needs (chakula, malazi na mavazi) kwa wahanga wa mabomu je tunaweza kushindana na ze unini??? Thubutu!!!