Nini Nimejifunza kutoka Ze Utamu na RM/RA Saga

Mwanafalsafa;
Mimi bado mgeni hapa na pengine nimekosea. Samahani kwa hilo. Kuna hoja nyingi za kisiasa ndanimwe!
 
Mwanafalsafa;
Mimi bado mgeni hapa na pengine nimekosea. Samahani kwa hilo. Kuna hoja nyingi za kisiasa ndanimwe!

Mkuu hata kama mgeni hauoni majukwa yameandikwa siasa, entertainment, mahusiano nk? Anyway no big deal.
 
Wakubwa si ndio watawala wenyewe? Wao ni kama "wafalme wa mbingu ya duniani..." so, sisi "watwana" tulie tu? Mpaka lini?

Kuna mtu aliandika humu: Tutaendelea kuwavumilia viongozi wabovu mpaka lini?

Jibu mnalo!
 
Mimi nadhani system ya Rais ndio iliyofanya kazi yake katika kutimiza wajibu wa kumlinda kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sheria zote za nchi. Hakuna mwanasiasa yeyota alietakiwa kuwakumbusha UWT kuifanya kazi hiyo ambayo hufanyika automatically.

Kitu ambacho tunatakiwa kushinikiza kifanyike ni ulindaji wa haki za raia wote kutokana na uchafuzi unaofanywa na baadhi ya media kama ilivyofanywa na hao zeutamu. Nijuavyo mimi, kama mtu akipeleka malalamiko yake (based on facts) kuhusu kudhalilishwa, kutukanwa na kadhalika, vyombo husika vingechukua hatua na kutokana na uwezo wake, vingeweza kufanikiwa kuizima hiyo zeutamu siku nyingi tu. Lakini ifahamike kuwa mshughulikiaji masuala ya usalama wa Rais na msimamiaji wa masuala ya usalama wa Raia ni tofauti kabisa na hata bajeti zao ni tofauti sana. Usishangae kusikia kuwa UWT wanatengewa pesa nyingi zaidi (pamoja na uchache wao) kuliko jeshi la Polisi linalotakiwa kulinda watu wote ikiwa ni pamoja na mimi na wewe na kufanya uchunguzi wa yote yanayotakiwa kuchunguzwa.

Anyway, hivyo ndivyo tulivyo. Nadhani ndio maana inasemekana hadharani kabisa kuwa kuna wenye nchi na wananchi.
 
Karibu kwenye uwanja wa kupigana na jiunge kwenye kundi la watu mwenye msimamo wa dhati kama wakina Dr. Slaa na wengine, Kimbia kabisa huko ulipo na jitokeze hadharani na jiungeni nao
 

usidhani wanaweza chochote....hakuna sana sana wanategemea interpol.
 

Mhhh interesting
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…