Nini njia ya kuachana na huyu mwanamke anayenitesa kiasi hiki?

Nini njia ya kuachana na huyu mwanamke anayenitesa kiasi hiki?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kuna dada mmoja nahisi sijui kaniroga au vipi. Kwani kwa mwezi mmoja sasa katika mapenzi yetu keshanifanyia vitimbi 90 vya kila aina, lakini kila nikiwaza tu kumfukuza kesho yake basi nashangaa ghafla upendo unazidi maradufu kwake.
Na kuna siku nakumbuka nilimfukuza na kwenda kwao Kyaka Nkude kijijini na haikuzidi hata saa tano nikamfuata na kumrudisha hapa kwangu na juzi tu nimemfumania akifanya mapenzi" Live " na rafiki yangu wa karibu

Lakini nikashangaa badala ya kukasirika na kumpiga ndiyo kwanza nikajikuta namwambia amalize kufanya mapaenzi na huyo rafiki yangu kisha anipitie turudi wote nyumbani. Sasa hiyo tisa, kumi ni hii ya leo na sasa hivi nimerudi kutoka kazini nimekuta kafunga mlango wa chumbani anafanya mapenzi tena na mtu mwingine na kanitumia meseji katika simu kuwa nisubiri kwanza amalizane na jamaa.

Kisha ndipo atanifungulia mlango na cha kushangaza baada ya kuambiwa hivyo mimi ndiyo kwanza nipo zangu sebuleni nacheza video game na mwanangu Gentamycine Jr. Na kuna wazo linanijia kuwa akishamaliza tu na huyo mshikaji basi nimkodie jamaa teksi impeleke kwake kupumzika halafu na mimi baadae nitoke na mke wangu kwenda kumnunulia zawadi.
Jamani nifanyaje kwani nafanyiwa vitimbi vya kila aina lakini najikuta tu nashindwa kumwacha au kumfukuza. Je nina tatizo gani labda?

Naombeni mnipe basi mbinu za kunisaidia mimi niweze kumwacha na nitawashukuruni nyote.
 
Acha ujinga wa kudanganya wanajamii wa Jamii Forum.
 

Na juzi tu nimemfumania akibanduliwa " Live " na rafiki yangu wa karibu lakini nikashangaa badala ya kukasirika na kumpiga ndiyo kwanza nikajikuta namwambia AMALIZE KUBANDULIWA na huyo rafiki yangu kisha anipitie turudi wote nyumbani.

088f3a89d7637e432240650368825f7eb9ea7c951dc7df895b2a5e3db0eb65fe.jpg

 
Seriously!!!! Wanaorogwa ata uwa awajitambui we unatambua kabisa na unasema unazan ungekua umerogwa ata JF ungesema upuuzi huo yaan hapa ungemsifia tu.achaaa u. .........
 
Ndiye huyu huyu uliyeleta thread juzi hapa "Kwa nilichokiona usiku huu kwa huyu mwanamke nahairisha rasmi ndoa yangu ya Disemba 2015"?


Anyway, nilikuwa nikiheshimu "sredi", post zako sana jukwaani.
 
Ndiye huyu huyu uliyeleta thread juzi hapa "Kwa nilichokiona usiku huu kwa huyu mwanamke nahairisha rasmi ndoa yangu ya Disemba 2015"?


Anyway, nilikuwa nikiheshimu "sredi", post zako sana jukwaani.

Duh! Aisee Watu Inaonekana Mnanifuatilia Mno Hadi Kupita Kiasi. Mtanitisha Sasa!
 
Back
Top Bottom