Haujibiwi kwa sababu nia ni kiba kura,Zanzibar kuna vituo Vingi vya kupiga kura na kura tano kwa mpiga kura.Kwa bahati mbaya zaidi kila kituo kitakachopigiwa kura siku ya tarehe 27/10/2020,hakutakuwa na kura za Maalim.CCM wametengeneza mazingira ya kujizolea idadi kubwa ya kura Siku hiyo ili tarehe 28/10/2020 wanapiga fainali.Tangia tupate Uhuru/Mapinduzi/Muungani,hatujawahi kusikia/kushuhudia aina hii ya uhuni.Zanzibar ina wapiga kura wasiozidi laki 5, Tanzania bara ina wapiga kura takribani milioni 29.
Zanzibar yenye wapiga kura laki 5 watapiga kura kwa siku mbili yaani tarehe 27 na 28/10 wakati Tanzania bara yenye wapiga kura wengi 29mil. watapiga kura kwa siku moja trh 28/10 tu. Kwanini? Kuna sababu gani za msingi, kama ni Askari au watumishi wa NEC/ZEC hawaoni kura hiyo ingehitajika zaidi Bara ili waweze kusimamia vizuri.
Swali la nyongeza, Je, kura zitakazopigwa mapema nani atazilinda usiku wa kuamkia trh 28 au matokeo yake yatabandikwa siku hiyo hiyo au mawakala wa vyama wataruhusiwa kulala na madanduku ya kura zilizopigwa mapema?
Mwenye majibu tafadhali ili kuondoa dukuduku.
Watanzania tusipobadilika hakutakuwa na mabadiliko kwa ajili yetu,tumeliwa mchana kweupeee!