Nini sababu hasa za Mwl Nyerere na Karume kuunganisha nchi zao?

God'sBeliever

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
5,788
Reaction score
3,033
Salau ndugu zangu.

Watu wataweza kunihisi vibaya hapa ila sina jambo baya napenda tuu kufahamu historia ya muungano wetu. Napenda munielezee kwa nini hawa marais waliamua kukaa chini na kuungana na kuunda taifa la muungano yani tanzania?

Kwa muliokuwepo/mnaojua background tujuzeni jamani tutambue historia ya taifa letu.
Wapo wanaodharau muungano hasa upande wa zanzibari, wanasema wanatawaliwa na tanganyika, wanasema wananyonywa n.k

Lakini upande wangu umoja thabiti ni mafanikio, umoja ni nguvu. Kusaidiana ni muhimu kwa mataifa yetu machanga hasa pale yalipokua yanafukuza ukoloni. Napenda kuwe na free movement ya hizi sehemu mbili (tanganyika na bara).

Napenda tuwe wamoja tuweke juhudi zetu pamoja, wanaotaka kuja bara waje na wanaotaka kwenda kule waende mradi tuu ni watanzania.

Tu shee resource zetu bwana.
Tuchukulie mfano USA(United states of america) tunaweza kujifunza jambo kwao.
 
Wala hawakukaa chini, walikurupuana tuu na mmoja akamzidi mwenzake ujanja ndio unaona kuna yale makero ya Muungano kila kukicha,

Mengine naacha, maana yanakera sana na kuudhi sana,
 
Karume hakutaka waarabu warudi kwa nguvu za kijeshi hivyo alikuwa anatafuta taifa kubwa la kumlinda.

Nyerere na marekani hawakutaka warusi waweke silaha zao zanzibar, walijua karume ni rahisi kudanganyika. Kumbuka sakata la "cuban misile crisis" la 1962 lilikuwa bado gumzo duniani na liliwaogofya viongozi wengi wasiofungamana na urusi.

Hivyo basi kwa ushawishi wa Marekani nyerere alimshawishi karume kuunganisha nchi mpaka akakubali kwa kigezo cha kupewa ulinzi, bila kuingiliwa masuala ya kiutawala (udikteta wa kimapinduzi).

Ili kuua moyo wa kimapinduzi nyerere alimshawishi jumbe kuunganisha vyama, kwa ahadi kwamba kitaitwa "chama cha mapinduzi".

Matokeo yake sasa zanzibar imekuwa koloni la waafrika ngozi nyeusi wa bara. Bora wangebaki kuwa koloni la mwarabu au wangefungamana na mrusi hadi miaka ya tisini. Wangekuwa mbali kimaendeleo.
 
"kwaheri ukoloni, kwaheri Uhuru" tafuta hicho kitabu utapata mawili matatu.
nishakipata mkuu ngoja nitafute siku nikisome. ila karume alikua mpuuzi sana ndio maana alipigwa risasi halafu nashangaa watanzania wanamuenzi kweli! lakin nyerere nae namponda kwani baada ya kuona huyu mtu hajatyulia si angevunja tuu huo muungano?
 
Yes mwenyewe nimeona karume alikua anatafuta sapoti tuu kwa sababu alikua dhaifu wana hakukuwa na lengo lolote.
Ila nyerere alikua mjanja sana huyu mtu, apumzike salama
 
nishakipata mkuu ngoja nitafute siku nikisome. ila karume alikua mpuuzi sana ndio maana alipigwa risasi halafu nashangaa watanzania wanamuenzi kweli! lakin nyerere nae namponda kwani baada ya kuona huyu mtu hajatyulia si angevunja tuu huo muungano?
Mkuu, unadhani wale jamaa wanahaja ya Muungano basi?
Si kweli hata kidogo, ni sisi tu ndio tunahaja nao maana ni hatari kwa...yetu,hiyo ni kauli ya mmoja katika viongozi wa Serikali yetu tukufu akiwa sehemu moja ya nyumba ya Bwana.
 
kinachonikwaza hawa wazanzibafr wanalalamika sana hata kwa vitu vidogo, sijui wanataka nini. Basi kama wanaona tunawanyinya ruksa waje bara kusaka maisha na wahamie kabisa kwa sababu bado nchi ni kubwa mno, mapori kibao na sehemju nyingine hawa watu wanaweza kuanza maisha huko.
 
Namimi kinachonishangaza Mkuu, ni kwanini na sisi wabara tuung'ang'anie Muu ngano ambao wenzetu hawatutaki au hawautaki?!!!
 
Kiukweli hakuna tunachofaidi kutoka kwao kama wanavyolalamika ila naona tu uzalendo na desturi aliyotujengea nyerere ndio inatufanya tuendelee kuupigania muungano na umoja ila hauna lolote hata tukiuvunja leo.
 
Labda mkuu, lakini kweli sisi ni wazalendo kwa namna tulivyo sasa au unafiki nao umetujaa na kipo kinachotufaidisha?
 
Hakuna kinachotufaidisha kikubwa tunauenzi ule umoja tulioachiwa na nyerere na kwa kweli umoja ni nguvu bwana, karume asingeweza kusimama mwenyewe kipindi kile, lazima waarabu wangerudi tuu.
Ila wazanzibari waache lawama za kijinga kama wanaona hawanufaiki na muungano basi waje bara kutafuta maisha.
 
Mkuu naona tupo pamoja lakini tusijekuitwa wachochezi, maana hizi keyboards wengine nikiwemo mimi naziheshimu sana katika matumizi,

Lakini maneno ya sisi Wabara au Watanganyika kupitia kwa kiongozi mmoja mkubwa wa Wizara ni miaka michache tuu alitoa kauli ambayo naamini hata yeye hakupenda ivuje, kauli hiyo au ile uliwahi kuisikia mkuu wangu?
 
mkuu sikupata kuisikia hiyo kauli, naomba uni pm nitambue aliyoyasema
 
mada kama hizi ukitaka kuziongelea kiukweli unaweza ukapotezwa ni yakuachana nayo
 
Mkuu naona unahasira kama mimi, lakini sio vibaya tukizipapasa papasa kama hivi ili wenzetu nao wahisi kitu fulani na wakatafute ukweli.
 
Back
Top Bottom