I personally, nina marafiki wengi wa kiume kuliko wa kike lakini kuna coincidence zinatokea nikianzisha mazungumzo na msichana fulani hasa ya kimaisha, kijamii kwa ujumla basi msichana husika hujikuta amejenga mazoea zaidi baada ya hapo.
Baada ya kuchunguza zaidi nikagundua wengi wao wanapenda kile kitokacho kichwani mwangu kupitia kinywa changu
(note: zungumza kile wanachopenda kukisikia, fanya kile wanachopenda kukiona)
hii ilikuwa sana kipindi hiko cha chuo, lakini baada ya hapo niliamua kuachana au kuepuka utaratibu huo kwa sababu zifuatazo....
1. Wengi hutake advantage na kukufanya baba/kaka ushauri wao, hapa tegemea kuletewa kesi zao na wapenzi wao, vitimbwi na drama zao (hii kitu inaboa sana)
2.The more unavyokuwa na marafiki wengi wa kike hapa kuna ile kasumba tunasema kujizibia riziki, assume kuna mdada anakuhusudu lakini anashindwa kumake even a single move kwako akihisi either una mahusiano na wasichana hao etc.
3. Sikupenda michezo ya "friend zone" ,unakuta upo na mtoto wa kike as a friend lakini kama mwanaume uliekamilika unaanza kuingia na hisia za mapenzi, once you cross border na kumueleza ukweli, wengi hukufunga kwenye ile space ya friend zone (hapa sielezei sana najua wengi tunaelewa hii.)
Bottom line...siamini kama baadhi ya wachangiaji waliopita kwamba kuwa na marafiki wa kike basi ni 'ukike' lakini atleast kuwa nao ambao mtakuwa mnabadilishana mawazo ya kimaisha na mambo mengine ya kimaisha na isitokee muda mwingi ukatumia nao kuliko jinsia yako, ukiona muda mwingi upo na watoto wakike ujue kuna muda mtaacha kuongea mambo ya maana na kujikuta mnaanza kuchangia umbea pamoja.
Let's meet at the top, cheers 🥂