Habari zenu wana Jamii Forums.
Niende kwenye mada moja kwa moja, nimekua kwenye wakati mgumu kimtazamo kutokana na mambo yanavyoenda kwenye Nchi yetu, na moja ya jambo ambalo limekua likinipa ukakasi ni juu ya swala la NACTVET kulazimisha wanafunzi wanaotaka kusoma hatua ya Degree kununua namba ambayo waniita AVN Number ili waweze kufanya Application
Swala hili binafsi naona ni kama njia nyingine ya kumnyonya mwananchi wa kitanzania,fikiria mzazi amepambana kwa kuungaunga maisha ili aweze kulipa Ada na gharama zingine za Chuo,alafu baada ya mtoto kumaliza chuo na kufahulu masomo yake eti kuna watu wa NACTVET wanakuja kumlazimisha alipie 15,000/= ili aweze kupata iyo AVN.
Hii si haki ni kuwaongozea wananchi mzigo, kuna sababu gani ya kuwalipisha wanafunzi pesa ili kupata iyo AVN yani mwanafunzi asome baada ya kuhitimu Chuo kimempatia hati yake ya matokeo (Trascript) alafu eti NActVET waje wawatake walipe 15,000/= kwa ajili ya kupata AVN Number?
Binafsi naona hili ni tatizo kubwa na Wizara ya Elimu kama Msimamizi wa Elimu Nchini waliangalie hili,kama NACTVET wanatafuta pesa waangalie namna nyingine ya kupata izo pesa lakini sio kwa utaratibu huu, na kibaya zaidi wameanza kupandisha gharama ya kulipia mwaka jana na miaka ya nyuma ilikua 10,000/= mwaka huu ni 15,000/= sasa unajiuliza hiki ni nini au na wao kunagharama za uendeshaji wa mfumo zimeongezeka?
Watanzania tuache kuumizana wenyewekwawenyewe hakuna sababu ya kutozana pesa, AVN itolewe bure.