Nini sababu ya Migogoro ya Ndoa/Wapenzi kuongezeka sana siku za hivi karibuni?

Nini sababu ya Migogoro ya Ndoa/Wapenzi kuongezeka sana siku za hivi karibuni?

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
1690102305774.png
Takwimu za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu zinaonyesha migogoro 28,773 ya wanandoa imepokewa kati ya Julai, 2022 na Aprili mwaka huu.

Kati ya migogoro hiyo, 22,844 ilisuluhishwa, huku 5,929 ikikosa usuluhishi licha ya kukatiwa rufaa ngazi ya Mahakama.

Kutokana na migogoro hiyo, watoto 18,922 waliathiriwa katika malezi, baadhi wakikimbilia mitaani, kuingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya au ndoa za utotoni.
 
Wanandoa wa siku hawana uvumilivu na wana tamaa ya fedha na mali, wana ubinafsi, unakuta mmoja ana mshahara mwingine hana anadharaulika na kunyanyaswa. Mwingine akiona jamaa yake kafulia anaachana naye na kwenda kwa msela mwingine asiyetaka watoto wa baba mwingine. Wale watoto inabidi waende kwa babu/bibi kulelewa huko, na hao vikongwe uwezo ukiwaishia watoto wanakimbilia mitaani. Kingine ni usaliti kunapelekea ndoa kuvunjika na watoto kukosa matunzo ya wazazi wote wawili. Kwa ujumla maadili ya ndoa yameporomoka kwa kiwango cha kutisha
 
Kila mtu kujifanya kambale , hayo mengine yanaongezea tuu ..!!
Asante
Samahani/nisamehe
Pole
Msingi mkuu.
 
Back
Top Bottom